Mkuu
wa Wilaya ya Karatu Mhe. Theresia
Mahongo akifuatilia hotuba ya Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo wakati wa kikao cha viongozi wa dini pamoja na
wazee wa Karatu.
|
Na Nteghenjwa Hosseah, Arusha
Serikali Mkoani Arusha imesema busara ilipaswa kutumika zaidi
katika Utekelezaji wa Agizo la Waziri Mkuu Mhe.
Majaliwa Kassim Majaliwa alilotoa wakati wa ziara yake Wilayani Karatu
katika Bonde la Eyasi kuhusu kusogezwa kwa Mashine za kuvuta maji Umbali wa
Mita 500 kutoka chanzo cha Maji.
Katika Agizo lake Mhe. Waziri Mkuu aliagiza kusogezwa kwa
mashine za za kuvuta maji kutoka chanzo cha maji cha bonde la Eyasi ambapo
akati mchakato wa utekelezaji ukiendelea baadhi ya wakazi wa eneo hilo
walizichoma moto mashine hizo ambazo kwa wakati huo zilikuwa zimesogezwa umbali
wa mita 60 ambazo zinaruhusiwa kisheria.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo akiwa katika ziara
ya Kikazi Wilayani Karatu amesema kutokana na umuhimu wa bonde la Eyasi katika
uzalishaji wa Chakula haikuwa busara kwa wananchikuchoma mashine hizo bila
kujali mazao ambayo tayari yameshaoteshwa katika eneo hilo na gharama
zilizotumika kununua mashine hizo.
Aliongeza kuwa wananchi hao walienda mbali zaidi kwa kujichukulia
sheria mikononi na kuharibu mali mbalimbali ikiwemo nyumba za wamiliki wa
mashine hizo hali iliyopeleka kuleta hofu, usumbufu na sintofahamu kwa wananchi
wa maeneo hayo.
“Vyombo vya ulizni na usalama vupo kwanini wananchi hawa
wasiende kuripoti tatizo hilo kwenye vyombo vinavyohusika na badala yake
wanaamua kujichukulia sheria Mkononi, Kisheria hairuhusiwi kwa mtu yeyeote
kuharibu mali ya mwananchi ilikua ni lazima tuwachukulie hatua wote waliofaya
uharibifu ule” Alisema Gambo.
Mhe. Gambo aliongeza kuwa haikuwa rahisi kwa wananchi wa
Mang’ola kuamua kufanya zoezi lile pekeyao inaonekana kuna viongozi wa Kisiasa
ambao wako nyuma ya vurugu zile na sisi kama Serikali tunaamini jukumu la
kiongozi ni kuleta Amani na sio uvunjifu wa Amani na ukienda kinyume sheria
inafuata mkondo wake.
“Hivyo katika kudhibiti vurugu zile wananchi wote na viongozi
wao waliohusika kwa namna moja ama nyingine kufanya uharibifu wa mashine na
mali za wananchi tuliwakamata na kuwapeleka Mahakama ili iwe fundisho katika
maeneo mengine” Alisem Gambo.
Kwa kuwa sasa wahusika wamekwisha tambua makosa yao tunaweza
kukaa pamoja na kuangalia namna gani bora ya kutumia maji ya bodne hili bila
kusababisha vurugu za aina yeyote ili kila mtuamiji aweze kunufaika na maji ya
bonde hilo.
Bonde hilo linatumiwa na wananchi zaidi ya elf 20
wanaojishughulisha na shughuli za Kilimo cha mazao mbalimbali kwa njia ya
umwagiliaji hutegemea maji yanayotoka katika Bonde la Eyasi .
No comments:
Post a Comment