Wednesday, January 25, 2017

ASKOFU DK. MALASUSA AZINDUA TAWI LA MAENDELEO BANK KARIAKOO JIJINI DAR ES SALAAM

WEK
  Askofu wa Dayosisis ya Mashariki na Pwani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa akiweka fedha mara baada ya kuzindua tawi jipya la benki ya Maendeleo la Kariakoo, jijini Dar es Salam, nyuma yake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Ibrahim Mwangalaba akifuatiwa na Mwenyekiti wa Bodi hiyo, Amulike Ngeliama (kulia). 
WEK 1
Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Banki Ibrahim Mwangalaba akiteta jambo na baadhi ya wateja wa kwanza waliyohudhuria ufunguzi wa tawi jipya la Kariakoo. 
WEK 2
Askofu wa Dayosisis ya Mashariki na Pwani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa  akiweka wakfu na kuzindua tawi jipya la Maendeleo banki, Kariakoo wakati wa hafla hiyo. Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi, Amulike Ngeliama, na kushoto ni Mkuu wa Jimbo la Kati Mch. Frank KImambo
WEK 3
Mkurugenzi mtendaji wa Maendeleo Bank, Ibrahim Mwangalaba akizungumza jambo wakati wa uzinduzi wa tawi la Kariakoo.
WEK 4
Baadhi ya Viongozi wa Maendeleo Bank wakiwa katika picha ya pamoja watatu kutoka kushoto ni Meneja wa Tawi Nuru Shadrack katika uzinduzi uliofanyika Kariako na kuzinduliwa na Baba Askofu Dkt Alex Malasusa.
BAKO
Meneja wa Tawi la Maendeleo Bank Nuru Shadrack akiwa anaongea na waandishi wa habari hawapo pichani katika uzinduzi wa bank hiyo iliyozinduliwa na Askofu wa Dayosisis ya Mashariki na Pwani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa
BAK KARI
Askofu wa Dayosisis ya Mashariki na Pwani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa akiwa anazindua Maendeleo bank jiji Dar es salaam akianza kwa Maombi ili bank hiyo iwe na neema kwa watumiaji
BAK KARI 2
Baadhi ya Wafanyakazi wa Maendeleo bank wakiwa pamoja na wateja waliojitokeza katika uzinduzi huo jijini Dar es salaam wakiwa tayari kuanza kuweka pesa zao
BAK KARI 3
…………….
Na.Alex Mathias,Dar es salaam.

  Askofu wa Dayosisis ya Mashariki na Pwani ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Dk. Alex Malasusa amezindua Maendeleo Bank Kariakoo jijini Dar es salaam huku akitoa pongezi kwa watumishi wa Kanisa kwa kuweza kuamua kuwasaidia Watanzania katika kuweka pesa zao katika bank hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari pamoja na wadau mbalimbali waliohudhulia uzinduzi huo Askofu Dkt.Alex Malasusa,amesema kuwa ni wakati wa Watanzania kuacha kufisha pesa nyumbani na kuweka kwenye vibubu kwani bank hii itaweza kuwasaidia katika kazi zao pindi wanapokuja kuweka pesa au kuomba mkopa.

“Hii Maendeleo bank ni ya watu wote haichague dini kwa hiyo mtu yoyote anweza kufungua Account kwa lengo la kutunza pesa zao na pia amewaasa watanzania kuwa na nidhamu ya pesa kwani wataweza kufanya shughuli zao kwa kufuata misingi ya dini pamoja na sheria za nchi”amesema Askofu Dkt.Alex Malasusa

Kwa Upande wa Mkurugenzi Mtendaji Mr.Ibrahim Mwangaleba amesema kuwa Maendeleo bank ni ya watu wote wa dini zote na inawakaribisha wateja waje kuweka pesa zao katika mahali salama na haitakuwa na ubanguzi wowote japokuwa ni ya Kikristo.

“Sisi tumeamua kufungua tawi la Maendeleo bank katika eneo la Kariakoo na tunaamini kwa imani kuwa hii itakuwa bank kubwa kuliko tawi lolote hapa jijini Dar es salam na itakuwa bega kwa bega na wateja watakaokuja kuchukua mkopo kwani hapa Fedha zitakuwa na maombi kwa lengo la wateja kwenda kuwa na maendeleo ya hali ya juu”amesema Mwangaleba

No comments: