Friday, December 9, 2016

Zoezi la huduma ya macho lafana mjini Dodoma

Zoezi la huduma ya macho linaendelea katika Shule ya Darul Muslemeen ambapo mpaka sasa mchana  huu wamejitokeza wananchi 3224. Katika zoezi hili  kila MWananchi Mwenye tatizo  anapatiwa bure miwani,dawa, ushauri. Na mpaka sasa wananchi zaidi ya 100 wameshaanza kufanyiwa upasuaji katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
Mbunge wa Dodoma mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde  amewashukuru sana wananchi wa Dodoma kwa kujitokeza kwa wingi sana kushiriki katika huduma hii ambayo ni ya bure isiyo na gharama yoyote iliyoratibiwa na Ofisi ya Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mjini na Taasisi ya Bilal Muslim Mission.  
"Shukran  sana kaka yangu Ridhiwan Kikwete kwa kusaidia kwa nafasi yako jambo hili kufanikiwa...Mungu akubariki sana", amesema  Mhe. Mavunde 

 Mbunge wa Dodoma mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde akisalimiana na wananchi waliojitokeza kupata huduma za bure za macho
  Mbunge wa Dodoma mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde akilaki  wananchi waliofika  kupata huduma za bure za macho
  Mbunge wa Dodoma mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde akisalimiana na wananchi waliojitokeza kupata huduma za bure za macho
 Baadhi ya wananchi waliojitokeza kupata huduma za bure za macho
 Mbunge wa Dodoma mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde akiangalia  wananchi waliojitokeza kupata huduma za bure za macho. Kushoto ni Bw. Ain wa Taasisi ya Bilal Muslim Mission.
 Wataalamu wa macho kutoka Taasisi ya Bilal Muslim Mission wakihudumia wananchi
  Mbunge wa Dodoma mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde akisalimiana na wananchi waliojitokeza kupata huduma za bure za macho
  Mbunge wa Dodoma mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde akiangalia  wananchi waliojitokeza kupata huduma za bure za macho. Kushoto ni Bw. Ain wa Taasisi ya Bilal Muslim Mission.
  Mbune wa Dodoma mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde akilaki  wananchi waliofika  kupata huduma za bure za macho

No comments: