Tuesday, December 20, 2016

Yaliyojiri Katika Vituo Mbalimbali vya Televisheni


SIMU TV:: Waziri wa mambo ya ndani auagiza uongozi mkoani Pwani kuwatafuta haraka  watu wanaofanya mauaji ya viongozi ; http://simu.tv/LpCrkLP

SIMU TV:: Waziri wa katiba na sheria Dkt. Harrison Mwakyembe amesema atashirikiana na ofisi ya mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam kujenga mahakama 20 za mwanzo; https://youtu.be/YxgOIvgMc2Y

SIMU TV:: Benki ya maendeleo ya Afrika AFDB yaipatia Tanzania mkopo wa dola milioni 164 kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kimaendeleo; https://youtu.be/en_3ruJd9O0

SIMU TV:  Hisa za kampuni ya simu ya mkoni ya Vodacom zitaanzwa kuuzwa katika soko la hisa la DSE mwishoni wa mwezi Januari mwaka 2017; https://youtu.be/Ljj4_A-l1sA

SIMU TV:: Vijana wameshauriwa kujiajiri katika ujasiriamali ili kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajira; https://youtu.be/xjgdA8j8jOY

SIMU TV:: Wasanii visiwani Zanzibar wametakiwa kusajili kazi zao ili kuiwezesha serikali kusimamia kazi zao vilivyo; https://youtu.be/OxRMulP64pY

SIMU TV:: Timu ya Azama FC yawatoa kwa mkopo wachezaji wake saba wa timu ya vijana katika timu zinazoshiriki ligi daraja la kwanza; https://youtu.be/925c44ycnqo

SIMU TV:: Mrembo kutoka nchini Puerto Rico, Stephanie Del Valle atwaa taji la mrembo wa dunia kwa mwaka 2016; https://youtu.be/0hfLuCpnq4E

SIMU TV: Mwanzilishi wa mtandao wa kijamii Jamii Forum Maxence Melo, amefanikiwa kupata dhamana kwenye mahakama ya Kisutu dhidi ya kesi inayomkabili; https://youtu.be/t1jXPYJ-mhA

SIMU TV: Wizara ya katiba na sheria imesema imeandaa muswada wa sheria ambao utawawezesha wananchi kupata huduma za kisheria bure bila malipo; https://youtu.be/P6kXHV8kbGU

SIMU TV: Serikali imewahimiza wananchi kutunza miundombinu ya barabara ambayo imejengwa kwa fedha nyingi za umma iweze kutumika kwa muda uliopangwa; https://youtu.be/yuZ70-gOhNA

SIMU TV: Baadhi ya wanasiasa nchini wametajwa kutumia nafasi zao kuwahimiza wananchi kuacha kulipia gharama za usafi katika maeneo yao; https://youtu.be/Y3tzXxc7YcI

SIMU TV: Jamii imeombwa kujitolea kuwatunza watu wenye mazingira magumu kama vile yatima ili kuwasaidia kupata huduma mbalimbali za msingi; https://youtu.be/DDspPY0Ialg

SIMU TV: Chama kikuu cha ushirika Liwale AMCOS, kimefanikiwa kuzindua mizani mkubwa unaotumika kupimia mazao ya wakulima ambao utasaidia kudhibiti mapato; https://youtu.be/swZY9_r-W6I

SIMU TV: Serikali imewataka wafanyabiashara wadogo maarufu kama Machinga kuhakikisha wanatunza mazingira pindi wafanyapo shughuli zao; https://youtu.be/-LfjrC8bCiw

SIMU TV: Yanga imepangwa kundi B katika michuano ya kila ya Mapinduzi visiwani Zanzibar ambapo wamepangwa kundi moja na timu ya Azam; https://youtu.be/JidFaQLS4iE

SIMU TV: Wajumbe wa mkutano mkuu wa chama cha mpira wa miguu mkoani Ruvuma FARU wamefanya uchaguzi wa kupata uongozi mpya; https://youtu.be/Trij_yt1cPI 

SIMU TV: Katika anga za kimataifa siku ya leo, wachezaji wa timu ya Liverpool wamesema ni lazima wapate ushindi katika mchezo wao mgumu utakaopigwa usiku huu dhidi ya Everton; https://youtu.be/rB8KzvCaHpk

SIMU TV: Mwanariadha wa mbio ndefu kutoka kijiji cha Msimbati mkoani Mtwara Dennis Mathias amesema ataitangaza vyema nchi ya Tanzania endapo ataungwa mkono; https://youtu.be/QvbxcOCFHu4

No comments: