Saturday, December 17, 2016

WAZIRI MKUU MAJALIWA AENDELEA NA ZIARA HALMASHAURI YA ARUSHA,AHUTUBIA MKUTANO WA HADHARA NAMANGA NA KUKABIDHI PIKIPIKI KWA VIJANA WA BODABODA

WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema Serikali itawanyang’anya ardhi wamiliki wote wa mashamba makubwa wilayani Arumeru ambao hawajayaendeleza kwa sababu wamekiuka mkataba wa umiliki.
Amesema Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa William Lukuvi atakuja mkoani Arusha kwa ajili ya kufanya mapitio ya mashamba yote makubwa ambayo hayajaendelezwa na kuyarudishwa Serikalini.
Waziri Mkuu ametoa kauli hiyo leo (Jumamosi, Desemba 17, 2016) wakati akizungumza kwa nyakati tofauti na watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Arumeru na wananchi wa kijiji Bwawani na kitongoji cha Mapinu katika kata ya Nduruma akiwa katika ziara yake ya kikazi mkoani Arusha.
“Tufanya mapitio ya kila shamba ili kujua linamilikiwa na nani na alipewa lini na tangu alipokabidhiwa amefanya nini. Shamba lisiloendelezwa litarudisha kwa wananchi. Kama mtu ameshindwa kupata mtaji kwa muda wa miaka 10 atapata leo,” amesema.
Amesema Serikali haiko tayari kuona wananchi wakinyanyaswa kwa kukosa ardhi ya kilimo kwa sababu ya watu wachache kumiliki maeneo makubwa bila ya kuyaendeleza..
"Ninataarifa kwamba hapa Arumeru kuna baadhi ya wawekezaji wanamiliki mashamba makubwa na hawajayaendeleza. Wengine wanakodisha kwa wananchi ili kujipatia fedha kinyume na mikataba yao ya umiliki. Hatutawavumilia,” amesema.
Amesema wilaya ya Arumeru inaongoza kwa migogoro ya ardhi na maeneo mengi yametwaliwa na mtu mmoja mmoja na baadhi yao wamekuwa wakilitumia vibaya Jeshi la Polisi kwa kuwanyanyasa wananchi wanaokatiza au kulima kwenye maeneo hayo.
“Kuanzia leo marufuku Jeshi la Polisi kutumiwa na mtu binafsi kuwanyanyasa wananchi. Mtafanya hivyo kama kuna uvunjifu wa amani na si vinginevyo,” amesema.
Awali, akisoma taarifa ya wilaya mkuu wa wilaya ya Arumeru Bw. Alexander Mnyeti  alimweleza Waziri Mkuu kwamba wilaya hiyo ina mashamba makubwa yanayomilikiwa na wawekezaji ambayo hayajaendelezwa.
Mkuu huyo wa wilaya amesema kitendo cha kutoyaendeleza mashamba hanayo kisababisha wananchi kuyavamia hali inayochangia kushamiri kwa migogoro ya ardhi katika wilaya hiyo.
Amesema tayari ofisi yake imefanya uhakiki wa mashamba hayo na kumuomba Mheshimiwa Rais, Dk. John Magufuli kufuta hati za mashamba 12 ambayo hayajaendelezwa kwa muda mrefu.
Katika hatua nyingine Waziri Mkuu amesema Serikali imepeleka sh. bilioni 800 katika halmashauri mbalimbali nchini kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu.
Waziri Mkuu alitoa kauli hiyo wakati akizindua nyumba ya walimu na vyumba vinne vya madarasa katika shule ya sekondari ya Orjolo, hatua ambayo inalenga kuboresha mazingira ya kufanyiakazi na kupunguza changamoto ya makazi kwa walimu.
Amesema changamoto ya makazi imekuwa ikiwakabili walimu kwa mrefu hivyo  Serikali imeamua kujenga nyumba za gharama nafuu ambazo zinawezesha familia sita kuishi pamoja.
Pia amewataka wazazi kuunga mkono jitihada za Serikali kwa kuboresha miundombinu ya shule na kuhakikisha wanafuatilia miendendo ya elimu kwa watoto wao.
“Tumeondoa ada na michango yote iliyokuwa inawakera na kusababisha mshindwe         kuwapeleka watoto shule. Jukumu lenu kwa sasa ni kufuatilia mienendo ya watoto wenu hadi kwa walimu ili kuhakikisha wanaingia darasani na wanasoma,” amesema.
Awali, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Dk, Wilson  Mahera alisema mpango wa maendeleo ya elimu ya sekondari ya awamu ya pili (SARPCCO II) umewezesha ujenzi wa vyumba vya madarasa 4,vyoo 20 pamoja na vyumba vya madarasa 6 vyenye jumla la Sh. milioni  289.52.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Ngaraseru- Usa River wilayani Arumeru 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Ngaraseru- Usa River wilayani Arumeru 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  kisalimiana na viongozi wa dini baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ngaraseru- Usa River wilayani Arumeru  kuhutubia mkutano wa hadhara. 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama ngoma ya kikundi cha sana cha Chuo Kikuu cha Makumira cha Arusha baada ya kuwasili kwenye  uwanja wa Ngaraseru - Usa River wilayani Arumeru kuhutubia mkutano wa hadhara

 Waziri Mkuu, Kassim Majliwa akimtwisha ndoo ya maji bibi Agness Silima ikiwa ni ishara ya kuzindua mradi wa maji wa kijiji cha Onderet wilayani Arusha 
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akipiga ngoma ya msanja iliyokuwa ikichezwa na wnanwake wa Arusha baada ya kuwasili kwenye kijiji cha Ondenderet wilayani Arusha Desemba 27, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitazama ngoma ya wanawake wa kimasai baada ya kuzindua mradi wa maji wa kijiji cha Ondenderet wilayani Arusha Desemba 27, 2016. kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizundua mradi wa maji wa kijiji cha Ondenderet wilayani Arusha Desemba 27, 2016.
  Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizundua mradi wa maji wa kijiji cha Ondenderet wilayani Arusha Desemba 27, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wananchi wa eneo la Kwamrombo wilayani Arusha ambao   walijipanga kwa wingi barabarani na kumshawishi kusimama  ili kuzungumza nao. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Arusha  Desemba 27, 2016.

 wanawake wa kimasai wakiimba wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipowasili kwenye uwanja wa mkutano kuhutubia wananchi katika kijiji cha Namanga kilichopo kwenye  mpaka wa Kenya na Tanzania wilayani Longido
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa  akiwapungia wananchi wa kijiji cha Namanga kilichopo kwenye mpaka  wa Kenya na Tanzania kilichopo kwenye  wilayani Longido  wakati alipohutubia mkutano wa hadhara kijijini 
 Waziri  Mkuu, Kassim Majaliwa akihutubia mkutano wa hadhara kwenye kijiji cha Namanga kilichopo kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya mkoani Arusha

 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikabidhiwa kirungu na wazee wa kimasai ikiwa ni ishara ya kumsimika kuwa mmoja wa wazee wa kabila hilo katika mkutano wa hadhara aliouhutubia katika kijjiji cha Namanga kilichopo kwenye mpaka wa Kenya na Tanzania  wilayani Longido
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wazee wa kimasai baada ya kuhutubia mkutano wa hadhara katika kijiji cha Namanga kilichopo kwenye mpaka wa Kenya na Tanzania wilayani Longido Desemba 16, 2016.  Wapili kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Desemba 16, 2016 alikabidhi pikipiki 10 kwa vijana wa bodaboda wa Namanga na  Longido  mkoani Arusha . Pichani, Waziri Mkuu akikabidhi pikipiki hizo baada ya kuhutubia mkuano wa hadhara katika kijiji hicho.

Waziri Mkuu, Kassim Majliwa kizungumza na wananchi wa kijiji cha Ormapinu  wilayani Arusha ambao wlijipanga  kwa wingi barabarani na kumshawishi kusismama ili kuwasikiliza. Alikuwa katika ziara ya mkoa wa Arusha Desemba 27, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

No comments: