Tanzania
na Umoja wa Nchi za Kiarabu (UAE) zimepiga hatua kubwa za ushirikiano hususan
wa kiuchumi ambapo kwa takwimu za Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) hadi
Juni, 2015 Makampuni 67 kutoka UAE yamewekeza hapa nchini katika sekta
mbalimbali kwa mtaji wa thamani ya Dola za Marekani milioni
497.12 na kuajiri Watanzania zaidi ya 9,044.
Hayo
yalibainishwa jana katika sherehe za kuadhimisha Siku ya Kitaifa ya UAE
zilizofanyika jijini Dar Es Salaam ambapo Waziri wa Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Augustine Mahiga alikuwa Mgeni
Rasmi.
Tanzania
na UAE zinatarajiwa kufanya Mkutano wa Kwanza wa Tume ya Pamoja ya
Kudumu ya Ushirikiano (JPC) ambao utakuwa chachu ya kuimarisha mahusiano
baina ya nchi hizi mbili hususan ya kiuchumi.
Akiongea
katika hafla hiyo, Mhe. Waziri alilipongeza taifa hilo kwa kuadhimisha siku
yake ya Kitaifa ikiwa imepiga hatua kubwa ya kimaendeleo ya kichumi, kijamii
na kisiasa. Mhe. Waziri alisema kuwa siku hiyo ni inatoa fursa pia ya
kutathmini mahusiano mazuri yaliyopo baina ya Tanzania na UAE.
Kwa
upande wake, Balozi wa UAE hapa nchini, Mhe. Abdulla
Ibrahim Ghanim Alsuwaidi aliishukuru Serikali ya Tanzania kwa
ushirikiano mkubwa inayotoa kwa Ubalozi huo ambao unamwezesha kutekeleza
majukumu yake kwa wepesi ikiwa ni pamoja na kuimarisha mahusiano ya nchi hizi
mbili. Mhe. Balozi aliahidi kuendeleza ushirikiano huo hususan katika
kutimiza azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya Kuifanya Tanzania kuwa nchi ya
Viwanda.
Umoja
wa Falme za Kiarabu (UAE) unajumusha falme saba ambazo ni Abu Dhabi, Dubai,
Sharjah, Ras Al Khaimah, Fujairah, Ajman na Umm al-Quwain huadhimisha
siku yake ya Kitaifa tarehe 02 Disemba ya kila mwaka tokea mwaka 1971.
|
No comments:
Post a Comment