Thursday, December 29, 2016

Wauguzi Muhimbili Watoa Zawadi kwa Wagonjwa Leo

 Mkurugenzi wa Uuguzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Agnes Mtawa akizungumza na wauguzi baada ya wauguzi hao kutoa zawadi kwa wagonjwa waliolazwa katika hospitali hiyo. Zawadi hizo zimepokelewa na mtoto Neema Selemani kwa niaba ya wagonjwa wengine. Kutoka Kushoto ni Mkuu wa Jengo la watoto, NPC One,  Bi. Anna Mponeja na Katibu wa Tughe Tawi La Muhimbili, Bw. Faustine Fidelis.
 Baadhi ya wauguzi wakiwa katika hafla fupi ya kutoa zawadi kwa wagonjwa mbalimbali.
 Mkurugenzi wa Uuguzi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Bi. Agnes Mtawa akitoa zawadi kwa mtoto Neema Selemani ambaye amepokea kwa niaba ya wagonjwa waliolazwa katika hospitali hiyo.

 Wauguzi wakifuatilia hafla hiyo leo.
 Mkuu wa Jengo la Watoto, NPC One, Bi. Anna Mponeja (katikati) akiwa amevishwa kitenge alivyopewa  zawadi na wauguzi wenzake.
 Meneja kutoka majengo mbalimbali katika hospitali hiyo wakiwa katika hafla hiyo Leo. Kutoka Kulia ni Meneja wa Jengo la Ufuaji, Bi. Lina Kinabo, Meneja wa Jengo la Upasuaji, Bi. Jane Chuwa, Meneja wa Jengo la Huduma za Nje, Bi. Juni Samwel na Meneja wa Jengo la Sewahaji, Bi. Salome Mayenga. 
 Mkuu wa Jengo la Watoto, NPC One, Bi. Anna Mponeja akimkabidhi Mkurugenzi wa Uuguzi katika hospitali hiyo, Bi. Agnes Mtawa zawadi maalamu.
 Bi. Anna Mponeja akimlisha keki mtoto Neema Seleman Leo katika hospitali hiyo.
Ni wakati wa kufungua Champainge..Picha zote na John Stephen, Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH)

No comments: