Monday, December 19, 2016

WATOTO WA KITUO CHA"WATOTO WETU TANZANIA" WAKUMBUKWA NA WAFANYAKAZI WA CBA BENKI

Watoto 108 wanaoisha katika mazingira magumu wanaolelewa katika kituo cha”Watoto Wetu Tanzania”(WWT),kilichopo Kimara Suka jijini Dar es Salaam,pamoja na walezi wao wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa benki ya CBA walipotembelea kituo hicho kutoa msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo vyakula na nguo.
Mwanzilishi na Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto wanaishi katika mazingira magumu wa kituo cha”Watoto Wetu Tanzania”(WWT) kilichopo Kimara Suka jijini Dar es Salaam, Evance Tegete akikabidhiwa msaada wa mfuko wa sabuni na Meneja Masoko wa Benki ya CBA,Salomon Kawiche(kulia) wakati wafanyakazi hao walipotembelea kituo hicho kutoa msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo vyakula na nguo.
Meneja Masoko wa Benki ya CBA,Salomon Kawiche(kulia) akimkabidhi msaada wa mafuta ya kupikia Victor Mussa anayelelewa katika Kituo cha kulea watoto wanaishi katika Mazingira Magumu cha”Watoto Wetu Tanzania”(WWT) cha Kimara Suka jijini Dar es Salaam,wakati wafanyakazi wa benki hiyo walipotembelea kituo hicho kutoa msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo vyakula na nguo.Kushoto ni Mwanzilishi na Mkuu wa Kituo hicho,Evance Tegete.
Meneja Uhusiano wa Banki ya CBA, Anna Shirima (kulia) akisaidiana na watoto wanaolelewa katika kituo cha”watoto wanaoishi katika mazingira magumu cha “Watoto Wetu Tanzania”(WWT) kilichopo Kimara Suka jijini Dar es Salaam,kuweka vyakula pamoja, baada ya kukabidhiwa na wafanyakazi wa benki hiyo msaada huo wa vitu mbalimbali vikiwemo vyakula na nguo.
Mtoto anayelelewa katika kituo cha kulea watoto wanaoisha katika mazingira magumu cha”Watoto Wetu Tanzania”kilichopo Kimara Suka jijini Dar es Salaam, Ivu Muhagama (kushoto)akikabidhiwa msaada wa viatu na Meneja Uhusiano wa Banki ya CBA,Anna Shirima,wakati wafanyakazi wa benki hiyo walipotembelea kituo hicho chenye watoto 108 kutoa msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo vyakula na nguo.
Wafanyakazi wa Benki ya CBA wakimsikiliza kwa makini Mwanzilishi na Mkuu wa Kituo cha Kulelea watoto wanaoisha katika mazingira magumu cha”Watoto Wetu Tanzania”(WWT), Evance Tegete (kushoto)kilichopo Kimara Suka jijini Dar es Salaam, wakati wafanyakazi hao walipofika kituoni hapo kutoa msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo nguo na vyakula kwa ajili ya watoto hao 108 .

No comments: