Tuesday, December 13, 2016

Wafugaji, wakulima wachangamkia fursa shule ya kiingereza Msata

Jamii ya wafugaji na wakulima wa mananasi wilayani Chalinze na Bagamoyo, wamepongezwa kwa kuchangamkia fursa za elimu msingi kwa mchepuo wa Kiingereza kwenye shule ya Mustlead iliyopo kata ya Msata,Wilayani Chalinze,Mkoani Pwani.

Hayo yalisemwa jana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Kasenyenda Investments, Bw.Benjamin Thompson wakati akikabidhi vyeti vya kumaliza shule ya awali kwa watoto wa shule, hiyo iliyopo kijiji cha Masuguru.

Alisema ni jambo linalotia moyo kuona jamii hizo zilivyoamua kuchukua maamuzi magumu ya kusomesha watoto, huku zikiwa a changamoto nyingi za kimaisha.

“Sehemu nyingi nchini, shule hizi huchukuliwa kwamba ni kwa ajili ya matajiri au watu wa daraja fulani, jambo ambalo ni tofauti na hali niliyoikuta hapa, maana wengi wenu ni wakulima na wafugaji wenye maisha ya kawaida,” alisema.

Amempongeza mwekezaji kwa kuamua kuwekeza shule hiyo vijijini,sambamba na mkakati wa serikali wa kuboresha elimu nchini, kitu kinachochochea maendeleo ya kijiji hicho na vingine vinavyoizunguka shule hiyo vikiwemo Kiwangwa, Fukayosi, Msata, Mandela, Miono, Makurunge Mwavi, Kidomole, Mkenge na Lugoba.

Naye Mwenyekiti wa Bodi ya Shule hiyo Bw.Idd Mapiphi alisema yeye ni shahidi wa ubora wa elimu ya shuleni hapo,kwani pamoja na mtoto wake, watoto wanapiga hatua nzuri kielimu kwenye shule hiyo ya Kiingereza haikuwahi kuwepo katika kata zao tangu Tanzania ipate Uhuru.

“Ujio wa shule hii ulitushangaza wengi, kwani tulijua haijengwi kwa ajili yetu.Lakini tuliambiwa kwamba hata sisi tunaruhusiwa kupeleka watoto kwa kulipa ada kidogo kidogo, basi tukasikia faraja sana juu ya hilo,” alisema.

Mwakilishi wa wazazi wa shule hiyo, ambaye pia ni Mwenyekiti wa kijiji cha Bago Bw.Maulid Tamla ameupongeza uongozi wa shule kwa kusimamia utoaji wa elimu bora kwenye mazingira ya kisasa.

Meneja wa shule hiyo Bw. Peter Stewart aliwaasa wakazi wa mikoa ya Dar es Salaam na Pwani kuacha kupeleka watoto wao mbali na maeneo ya nyumbani, kwa ajili ya elimu wakati shule yake ipo na ni ya kutwa na pwani ina viwango vya kimataifa.

“Wakati umefika kwa watanzania kuacha kupeleka watoto wetu nchi za nje au mbali sana na nyumbani kwani kwa kufanya hivyo unajikosesha nafasi ya kuwa karibu na watoto kwa kushindwa kumtembelea mara kwa mara.”

Alisema shule mbali na masomo ya kiada, shule ina mpango wakuazisha masomo ya ziada kwa vitendo kwenye fani ya kilimo cha mbogamboga na matunda ili kuwajengea wanafunzi msingi mzuri wa maisha ya kujitegemea.
NB:Kwa kuomba nafasi ya kuleta mtoto shule hii, piga nambari 0764411111/ 0786202202
Mgeni rasmi kwenye mahafali ya elimu ya awali kwenye shule msingi Mustlead ya Msata,Wilayani Chalinze Mkoani Pwani Bw Benjamin Thompson(wa tano kulia), akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu,wazazi pamoja uongozi wa shule hiyo jana
Mkurugenzi wa Kampuni ya Kasenyenda Investments Bw Benjamin Thompson akikabidhi cheti cha uhitimu wa elimu ya wali kwa Mtoto Ibrahim Kimaki kwenye shule ya msingi Mustlead iliyopo Msata,Wilayani Mkoani Pwani.Mama wa Mtoto huyo Adela Kimaki akishuhudia.

 Sehemu ya shule hiyo kwa muonekano wa nje

No comments: