Wednesday, December 21, 2016

MFUKO WA FIDIA KWA WAFANYAKAZI WAZINDUA HUDUMA YA ULIPAJI WA MAFAO YA FIDIA NA UZINDUZI WA UBIA BAINA YA WCF NA WATOA HUDUMA ZA AFYA


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Ajira na wenye ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama, akikata utepe kuzindua mafao ya Fidia na na ubia baina ya watoa huduma za afya .Uzinduzi huo ulifanywa na Waziri Mhagama kwa niaba ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa jijini Dar es Salaam, Desemba 20, 2016. wanaoshuhudia ni Naibu Mawaziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Mh. Anthony Mavunde, (wapili kulia), Mh. Dkt. Abdallah Possi, (watatu kulia), Bw. Emmanuel Humba, Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), wanne kulia, na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba. (watano kulia). .( PICHA NA MUHIDIN SUFIANI)

NA ANTHONY JOHN, GLOBU YA JAMII
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge kazi ,vijana Ajira na watu wenye ulemavu, Jenista Muhagama, amewataka waajili wote kuwasilisha Michango ya wafanyakazi wao Mfuko Fidia kwa Wafanyakazi WCF kwa wakati.

Akizungumza katika Uzinduzi wa Huduma za utoaji wa Mafao ya fidia kwa wafanyakazi na ubia kati ya Mfuko na watoa Huduma za Afya amesema kuwa
kwa Mwaka huu wafedha Serikali imewasilisha Michango ya wafanyakazi wake wote ambapo alizitaka Sekta binafsi pia kuwasilisha Michango yao kwa wakati.

Sanjari  na Hayo Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko huo Masha Mshomba ameongeza kuwa Mpaka kufikia Novemba 30 Mwaka huu Jumla ya waajili 5945 wamechangia na wamepewa na ya usajili.

Hata Hivyo Mweketi  wa Bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko huo Emmanuel Humba amesema Mfuko Huo utachangia kwa kiwango kikubwa Sera ya Tanzania ya Viwanda  iliyoa anzishwa na Serikali ya awamu ya tano kwani wafanyakazi watakapo  kuwa na Afya njema watafanya kazi kwakujiamini na kuleta Maendeleo.

 Waziri Mhagama akihutubia
 Mwenyekiti wa bodi ya WCF, Bw. Emmanuel Humba akitoa hotuba yake
 Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw.Masha Mshomba, akitoa hotuba yake
 Mgeni rasmi, Naibu Mawaziri, viongozi wa WCF, na waliotunukiwa vyeti wakiwa kwenye picha ya pamoja

Waziri Mhagama, akimkabidhi cheti cha ubia baina ya WCF na watoa huduma za afya,  Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya, Bernard Konga, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Huduma ya Utoaji wa Mafao ya Fidia kwa Wafanyakazi na Ubia kati ya Mfuko na watoa huduma za afya, WCF uliozinduliwa jijini Dar es Salaam, leo.


Waziri Mhagama, akimkabidhi cheti cha ubia baina ya WCF na watoa huduma za afya,  Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Mkifupa (MOI), Dkt. Othman Kiloloma, wakati wa hafla ya uzinduzi wa Huduma ya Utoaji wa Mafao ya Fidia kwa Wafanyakazi na Ubia kati ya Mfuko na watoa huduma za afya, WCF uliozinduliwa jijini Dar es Salaam, leo.

 Mgeni rasmi akimpongeza msanii Mrisho Mpoto kwa ujumbe wake murua kupitia sanaa
Mgeni rasmi akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa WCF na wageni wengine
Waziri akisalimiana na mameneja na maafisa wa WCF, wakati akiwasili
 Wafanyakazi wa WCF wakimsubiri mgeni rasmi
 Waziri akiongozana na  Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, huku akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi wa
Waziri Mhagama, akisalimiana na baadhi ya wafanyakazi waWCF

No comments: