Thursday, December 29, 2016

VYOMBO VYA HABARI HAVIKUTANGAZA WAGOMBEA WANAWAKE KWENYE UCHAGUZI MKUU ULIOPITA- TATHMINI

Afisa mratibu wa umoja wa mataifa kitengo cha wanawake Rashida Shariff akifungua warsha ya siku mmoja iliyokuwa na lengo la kujadili ripoti ya uchaguzi mkuu kwa wagombea wanawake,vijana na makundi maalumu iliyofanyika kwenye Hotel ya Lush Garden jijini Arusha mwishoni mwa wiki iliyopita picha zote na mahmoud ahmad wa globu ya jamii
Mratibu wa semina hiyo Edson Msofe kutoka TAMWA akiwa na Rashida Sharifu kutoka UN WOMEN wakifuatilia jambo kwenye warsha iliyoandaliwa na chama cha waandishi wa habari wanawake hapa nchini(TAMWA)kwa kushirikiana na UN WOMEN na kuwashirikiasha wagombea wanawake,vijana na walemavu

VIONGOZI KUTOKA VYAMA VYA SIASA WAKIFUATILIA WARSHA HIYO

Mweneykiti wa chama cha walemavu ambaye pia alikuwa mgombea kwenye uchaguzi mkuu akiteta jambo na aliyekuwa mgombea wa kiti cha uraisi kupitia chama cha ACT wazalendo Anna Mghwira wakibadilishana mawili matatu kabla ya kuanza kwa warsha hiyo

sehemu ya washiriki wakifuatilia warsha hiyo

WAHARIRI WA REDIO  ZA JIJINI ARUSHA Baraka Sunga na Joseph Laizer AIDEA FM NA SUNRISE WAKIWA NA MWANDISHI WA  CLOUDS TV Beatrise gerald


Makundi yakichangia maoni yao katika warsha hiyo

Wagombea wanawake waliogombea kwenye uchaguzi mkuu uliopita wilayani Meru wakiteta jambo wakati wa warsha hiyo

Kundi la waandishi wa habari kutoka vyombo mbali mbali walioshiriki warsha hiyo wakijadiliana mada kwenye warsha hiyo ya siku mmoja

WAGOMBEA NA VIONGOZI WA VYAMA VYA SIASA WAKIFUTILIA WARSHA HIYO ILIYOANDALIWA NA TAMWA NA UN WOMEN KWA WAGOMBEA WAANDISHI WA HABARI VIJANA NA MAKUNDI MAALUMU

Washiriki wakifuatilia jambo wakti semina ikiendelea

Mwandishi wa habari wa gazeti la Dail News Hazla quire akiwa na mwandishi wa mwananchi Zulfa Mussa na Mwandishi wa Channel 10 Arstide Dotto wakifuatilia kwa karibu warsha hiyo ambapo imedaiwa kuwa wagombea wanawake waliombwa hadi rushwa ya Ngono ili wapate Airtime kutoka kwa wanahabari picha zote na globu ya jamii Arusha.


                        Na Mahmoud Ahmad Arusha
Wadau wa maendeleo,viongozi wa siasa na vyombo vya habari wanalojukumu la kuhakikisha wanahamasisha wanawake, makundi maalum na vijana kuomba nafasi za uongozi kwa wingi ilikuweza kuwa na usawa wa kijinsia kwenye masuala mbalimbali ya kujiletea Mandeleo.
Hayo yamebainishwa kwenye warsha ya siku moja iliyowashirikisha wagombea wanawake,makundi maalum na vijana,wanahabari, pamoja na viongozi wa vyama vya siasa iliyoandaliwa kwa pamoja na TAMWA na UN WOMEN na kufanyika wilayani Arumeru mkoani hapa.
Akizungumza wakati akitoa mada mratibu wa semina hiyo Rashida Shariff alisema kuwa warsha hiyo ni kushirikiana matokeo ya ripoti ya uchambuzi na kujadili changamoto walizopata wagombea wanawake,makundi maalumu na vijana katika kipindi cha uchaguzi  kwa vyombo vya habari hapa nchini kutoripoti ipasavyo habari zao kutokana na vyombo hivyo kuwa ni vya kibiashara zaidi.
Alisema kuwa malengo ya warsha hiyo ni kujadili changamoto za uchaguzi mkuu na nini kifanyike,ambapo wanatambua vyombo vya habari  ni chanzo mojawapo katika kuwatoa wananchi katika giza na kuwapeleka katika mwanga ili kusaidia na kuibua changamoto ya kuweza kufikisha taifa katika usawa wa kumfanya mwanamke,makundi maalumu na vijana kuwa nao wanauwezo sawa  na wengine ambapo wanasiasa wanawake,makundi maalumu na vijana kama watapewa kipaumbele cha kupata nafasi ya habari zao kuripotiwa na vyombo hivyo kila mara.
“Warsha hii ni kufuatilia jinsi vyombo vya habari vilivyoripoti taarifa za wanawake na vijana katika kugombea kwenye uchaguzi mkuu uliopita na kupata uchambuzi wa dhana ya kijinsia katika vyombo vya habari juu ya usawa wa kijinsia katika huduma za jamii na uongozi”alisema Shariff
Kwa upande wake Katibu wa chama cha wananchi (CUF)mkoani hapa Zuberi Mwinyi alisema kuwa lazima kuwe na mabadiliko kwa wanahabari kupewa semina za mara kwa mara ilikusaidia wanawake,makundi maalumu na vijana kwa sababu tasnia ya habari ndio nyenzo ya kumtoa mtu kutoka eneo moja kwenda jingine.
Alisema kuwa tofauti na hapo watanzania watajiona hakuna kinachoendelea kwa kuwa hakuna tathmini ya mabadiliko katika sekta ya kuwasaidia wanawake,makundi maalum na vijana iliweze kufikia malengo ya kuwa na usawa wa kijinsia katika jamii wanaoishi.
Nae Mjumbe wa halmashauri kuu ya Uvccm mkoani hapa Saitoti Zelothe alisema kuwa ifike mahali wanawake,makundi maalum na vijana wakasaidiwa kukuwa kiuchumi na kuweza kwenda sambamba na wagombea wengine kwani suala la gharama za kifedha katika uchaguzi halikwepiki na limekuwa mwiba kwa wagombea wa kundi hilo kukosa mwamko wa kugombea.

No comments: