Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
SERIKALI imesema haitavumilia vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto vikiendelea kufanyika, hali ambayo inasababisha baadhi ya wanawake na watoto kukosa haki zao.
Hayo yamesemma na Waziri wa Afya, Maendeleo Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mh. Ummy Mwalimu wakati akizindua Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya wanawake na Watoto 2017 -2022, amesema tatizo la ukatili dhidi wanawake na watoto ni kubwa nchini na limeathiri maendeleo yao na ya taifa kiujumla.
Waziri wa Afya, Maendeleo Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akikata utepe kuashiria katika uzinduzi Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya wanawake na Watoto 2017 - 2022, leo jijini Dar es Salaam.
Ummy amesema kwa mujibu wa takwimu za jeshi la polisi vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto vilivyoripotiwa 2015 vilifikia 22,876 kati ya hivyo vitendo vya ubakaji vilikuwa 3,444 , shambulio , kujeruhi na matusi vilikuwa 14, 561.
Amesema ukatili dhidi ya watoto unafanywa majumbani na shule hivyo kila shule ya msingi na sekondari kutaundwa timu za ulinzi pamoja na kila kata kuwa na timu ya ulinzi.
Naye Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Philip Mpango ameagiza Wilaya, Mikoa na Miji midogo kutenga bajeti ya mpango huo ili uweze kutekelezeka wenye thamani ya zaidi ya sh. Bilioni Tano.
Waziri wa Afya, Maendeleo Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu pamoja na Mawaziri Mbalimbali waliofika kwenye uzinduzi wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya wanawake na Watoto 2017 - 2022, leo jijini Dar es Salaam.
Katika uzinduzi huo mawaziri nane wametoa msimamo wao katika utekelezaji wa mpango kazi huo.
Mawaziri hao ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage, Waziri wa Maendeleo Kilimo na Uvuvi, Charles Tizeba , Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Utaribu wa Bunge, Sera ,Kazi na Walemavu, Jenesta Mhagama, Waziri wa Katiba na Sheria Dk. Harrison Mwakyembe, Naibu Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia, Mhandisi Stella Manyanya, Naibu Waziri Habari,Michezo,Utamaduni na Sanaa, Annastanzia Wambura, Naibu Waziri na Nishati na Madini, Medrad Kalemani
pamoja na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.
Waziri wa Afya, Maendeleo Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza katika uzinduzi Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya wanawake na Watoto 2017 - 2022 leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wadau waliohudhuria uzinduzi wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya wanawake na Watoto 2017 - 2022, leo jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya, Maendeleo Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya mawaziri mara baada uzinduzi wa Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya wanawake na Watoto 2017 - 2022, leo jijini Dar es Salaam.Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya jamii.
No comments:
Post a Comment