Monday, December 19, 2016

Uzinduzi wa ‘Yamoto Taarab’ Watia Kiwewe Mashabiki Dar Live

DAR ES SALAAM: Bendi mpya ya muziki wa taarab iitwayo Yamoto Taarab jana usiku katika ukumbi wa maraha wa Dar Live ulioko Mbagala Zakhem ulipagawisha umati wa mashabiki ambao pamoja na muziki huo walijimwaya kwa muziki wa vikundi mbalimbali vya mchiriku na muziki wa kizazi kipya.
Kundi la Yamoto likiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi wao, Saidi Fela.
Mwanamuziki wa Yamoto Taarab, Fatuma Mcharuko, akitunzwa pesa na shabiki.
Leila Rashid (kushoto) akiimba huku Mohamed Mauji akiungurumisha gitaa.
Omar Tego akiimba huku mashabiki wakimtunza.
Msanii mlemavu maarufu kwa jina la Chiba akionyesha umahiri wakunengua kwa staili ya Nyani Kagoma. 
Wanamuziki wa kizazi kipya, Chegge Chigunda na Mheshimiwa Temba, wakitoa burudani.
Mheshimiwa Temba akiserebuka na mnenguaji wake.
Madada sita toka Mkubwa na Wanae wakitoa burudani.

(PICHA ZOTE NA ISSA MNALLY)

No comments: