Wafanyakazi wa kampuni ya bia ya TBL wakionyesha kwa waandishi wa habari
chupa mpya ya Chibuku Super ya Ml 500 wakati wa hfla fupi ya uzinduzi
iliyofanyika jijini Mwanza leo.
Wafanyakazi wa kampuni ya bia ya TBL wakionja Chibuku super ya Ml
500 wakati wa hfla fupi ya uzinduzi iliyofanyika jijini Mwanza leo.
Meneja Masoko wa TBL Group Oscar Shelukindo,akizungumza na waandisi wa
kuhusiana na muonekano mpya wa chupa ya Chibuku Super ya Ml 500 wakati
wa hafla fupi iliyofanyika jijini Mwanza leo. kulia ni Meneja Kiwanda
cha Chibuku Super Mwanza Herbert Ilembo.
Mwanza Desemba 1,2016:Kampuni ya TBL Group, leo imezindua Chibuku Super kwenye chupa ya bia ya ml 500, huku ikitoa wito kwa watanzania kutumia vinywaji vinavyozalishwa hapa nchini ili kujenga uchumi wa taifa kwa ujumla.
Akizungumza katika hafla ya uzinduzi huo uliofanyika katika ukumbi wa kiwanda kilichopo eneo la Pasiansi Mwanza , Meneja Masoko wa TBL Group, Bw. Oscar Shelukindo alisema uzinduzi wa bia hiyo ya Chibuku Super” kwenye chupa ya glasi inayorudishwa (Returnable) unatarajiwa kuleta mapinduzi makubwa katika soko la Bia hapa nchini.
“Leo ni siku ya furaha kubwa sana kwetu TBL na kwa watumiaji wote wa Bia yetu hi ya asili , kwani tumeweza kuzindua Bia hii imetengenezwa kwa utaalamu wa hali ya juu na kwa kutumia mitambo ya kisasa kabisa, hivyo kuwahakikishia wanywaji Ubora wa hali ya juu, ina ujazo wa nusu lita na itauzwa kwa bei ya shilingi 700/- tu, kwa chupa na 14,000 kwa kreti,’’ alisema.
Akiizungumzia bia hiyo Shelukindo alisema inatengenezwa kwa kutumia malighafi za hapa nyumbani, ikiwemo nafaka ya mahindi na mtama bora toka kwenye ardhi ya Tanzania na hivyo kutoa kila sababu kwa watanzania kujivunia kinywaji chenye asili ya taifa lao.
“Chibuku Super ina kilevi cha asilimia 4, kinachomfanya mtumiaji aweze kuitumia kwa muda mrefu akiwa na marafiki, lakini pia inampa lishe nzuri kutokana na virutubisho vinavyopatikana katika nafaka zinazotumika kutengeneza bia hii,’’ aliongeza
Akizungumzia juu ya usambazaji wa Bia hiyo, meneja mauzo wa TBL Bw. Fred Kazindogo alisema baada ya uzinduzi huo itaanza kupatikana Desemba 2 mwaka huu kwa wasambazaji wakubwa na katika baa mbalimbali na sehemu nyinginezo zinazouza vileo.
Alisema kwa kuanzia Bia hiyo itaanza kupatikana katika mikoa 15 ikiwemo Mwanza, Kagera, Mara, Shinyanga, Geita, Tabora, Singida, Kigoma, Simiyu, manyara , Kilimanjaro, Arusha, Katavi, Mbeya na Rukwa.
“Na kwa wauzaji wa jumla, tunatarajia watahamasika kuuza bia ya Chibuku Super kwani ina faida nzuri na inadumu kwa miezi 4 kwenye soko, muda ambao ni mrefu sana kulinganisha na products zetu nyingine,’’alisema
No comments:
Post a Comment