Waziri wa nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu Sera na Uratibu, Jenister Mhagama (kushoto) na Waziri wa
Fedha na Mpango, Dr. Phillip Mpango (katikati) wakijadili masuala pamoja na wakurugenzi
wakuu wa mifuko hifadhi ya jamii ya NSSF na PPF, Profesa Godius Kahyarara na
Bw.William Erio pamoja na Mbunge Jimbo
la Morogoro Kusini Mashariki Omari Mgumba (kulia) kuhusiana
na mradi mkubwa wa ujenzi wa kiwanda cha sukari kitakachojengwa katika eneo la
Mkulazi, mkoani Morogoro ikiwa ni uwekezaji wa pamoja wa mifuko
hifadhi ya jamii ya NSSF na PPF wakati viongozi hao walipotembelea
mradi huo mwishoni mwa wiki.
Waziri wa nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu Sera na Uratibu, Jenister Mhagama na Waziri wa Fedha na Mpango,
Dr. Phillip Mpango wakikagua ujenzi wa barabara inayoelekea
sehemu ya mradi ambayo inafanyiwa ukarabati mkubwa na kampuni ya ujenzi ya SUMA
JKT.
Waziri wa nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu Sera na Uratibu, Jenister Mhagama na Waziri wa Fedha na Mpango,
Dr. Phillip Mpango wakikagua ujenzi wa barabara inayoelekea
sehemu ya mradi ambayo inafanyiwa ukarabati mkubwa na kampuni ya ujenzi ya SUMA
JKT.
Waziri wa nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu Sera na Uratibu, Jenister Mhagama (wa tatu kushoto) na Waziri
wa Fedha na Mpango, Dr. Phillip Mpango (katikati) wakifuatilia maelezo kutoka
kwa muwakilishi wa kampuni ya Mkulazi Holding inayotekeleza mradi mkubwa wa ujenzi
wa kiwanda cha sukari kitakachojengwa katika eneo la Mkulazi, mkoani Morogoro
ikiwa ni uwezeshaji wa pamoja wa mifuko hifadhi ya jamii
ya NSSF na PPF wakati viongozi hao walipotembelea mradi huo mwishoni
mwa wiki.
Waziri wa nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu Sera na Uratibu, Jenister Mhagama (wa tatu kushoto) na Waziri
wa Fedha na Mpango, Dr. Phillip Mpango (katikati) wakifuatilia maelezo kutoka
kwa muwakilishi wa kampuni ya Mkulazi Holding inayotekeleza mradi mkubwa wa ujenzi
wa kiwanda cha sukari kitakachojengwa katika eneo la Mkulazi, mkoani Morogoro
ikiwa ni uwezeshaji wa pamoja wa mifuko hifadhi ya jamii
ya NSSF na PPF wakati viongozi hao walipotembelea mradi huo mwishoni
mwa wiki.
aziri wa nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu Sera na Uratibu, Jenister Mhagama (kushoto) na Waziri wa
Fedha na Mpango, Dr. Phillip Mpango (katikati) wakimsikiliza Mbunge Jimbo
la Morogoro Kusini Mashariki Omari Mgumba (kulia) ambae
jimboni kwake ndipo unatekelezwa mradi
mkubwa wa ujenzi wa kiwanda hicho.
Wananchi wa kijiji cha
Kidunda, kata ya Mkulazi, wilaya ya Morogoro Vijijini wakikaribisha ugeni huo
muhimu. Kukamilika kwa mradi huo kunatarajiwa kutoa ajira zaidi ya 100,000 huku
kipaumbele kikiwekwa zaidi kwa wakazi wanaoishi maeneo jirani na mradi.
Wananchi wa kijiji cha
Kidunda, kata ya Mkulazi, wilaya ya Morogoro Vijijini wakikaribisha ugeni huo
muhimu. Kukamilika kwa mradi huo kunatarajiwa kutoa ajira zaidi ya 100,000 huku
kipaumbele kikiwekwa zaidi kwa wakazi wanaoishi maeneo jirani na mradi.
Wananchi wa kijiji cha
Kidunda, kata ya Mkulazi, wilaya ya Morogoro Vijijini wakikaribisha ugeni huo
muhimu. Kukamilika kwa mradi huo kunatarajiwa kutoa ajira zaidi ya 100,000 huku
kipaumbele kikiwekwa zaidi kwa wakazi wanaoishi maeneo jirani na mradi.
Washirika muhimu! Wakurugenzi
wakuu wa mifuko hifadhi ya jamii ya NSSF na PPF, Profesa Godius Kahyarara
(kulia) na Bw.William Erio (kushoto) wakisikiliza hotuba ya Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera na
Uratibu, Jenister Mhagama alipokuwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha
Kidunda, kata ya Mkulazi, wilaya ya Morogoro Vijijini mwishoni mwa wiki.
Waziri wa nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu Sera na Uratibu, Jenister Mhagama akizungumza na
wananchi wa kijiji cha Kidunda, kata ya Mkulazi, wilaya ya Morogoro Vijijini
wakati alipotembelea mradi huo mwishoni mwa wiki ambapo aliwahakikishia wakazo
hao kuhusiana na utekelezaji wa mradi huo huku akiwaahidi kuwa mradi utatoa
kipaumbele zaidi kwa wakazi wa eneo hilo hususani vijana.
Waziri wa nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu Sera na Uratibu, Jenister Mhagama (wa pili kulia) na Waziri
wa Fedha na Mpango, Dr. Phillip Mpango (wa tatu kulia) walipotembelea bwawa la
Kidunda lililopo kijiji cha Kidunda, kata ya Mkulazi, wilaya ya Morogoro
Vijijini. Mawaziri hao walipokea ombi la kuwezesha ujenzi wa daraja
litakalounganisha kijiji hicho na Wilaya ya Kisarawe, Mkoa wa Pwani ili
kurahisisha mawasiliano baina ya mikoa hiyo miwili.
Waziri wa nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu Sera na Uratibu, Jenister Mhagama (kushoto) na Waziri wa
Fedha na Mpango, Dr. Phillip Mpango (kulia) wakijipongeza baada ya kukamilisha
ziara hiyo muhimu. Katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa mfuko hifadhi ya jamii wa NSSF
Profesa Godius Kahyarara.
Waziri wa Fedha na Mpango,
Dr. Phillip Mpango (kushoto) akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mkuu wa mfuko
hifadhi ya jamii wa PPF Bw.William Erio
MIFUKO ya hifadhi ya
jamii ya NSSF na PPF imeanza utekelezaji wa awali wa mradi mkubwa wa
ujenzi wa kiwanda cha sukari kitakachojengwa katika eneo la Mkulazi, mkoani
Morogoro ikiwa ni jitahada ya mifuko hiyo kwa pamoja kuunga mkono muelekeo wa serikali
ya awamu ya tano wa kuwekeza kwenye uchumi wa viwanda.
Kukamilika kwa kiwanda
hicho kinachotajwa kuwa kitakuwa ni kikubwa zaidi Afrika Mashariki, kutaongeza
uzalishaji wa sukari wa hapa nchini ambapo zaidi ya tani laki mbili (200,000)
zitakuwa zikizalishwa kwa mwaka sambamba na kutoa ajira zaidi ya 100,000 kwa
hatua ya awali.
Akizungumza na wananchi
wa kijiji cha Kidunda, kata ya Mkulazi, wilaya ya Morogoro Vijijini wakati
alipotembelea mradi huo mwishoni mwa wiki, Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
Sera na Uratibu, Jenister Mhagama aliekuwa ameambatana na Waziri wa
Fedha na Mpango, Dr. Phillip Mpango, mbali na kuipongeza mifuko hiyo,
aliwahakikishia wakazo hao kuhusiana na utekelezaji wa mradi huo huku
akiwaahidi kuwa mradi utatoa kipaumbele zaidi kwa wakazi wa eneo hilo hususani
vijana.
“Mradi huu una ushawishi
mkubwa kutoka kwa Rais John Magufuli kutokana na adhma yake ya kuibadili
Tanzania kuwa nchi ya viwanda na umekuja kwa wakati muafaka. Nataka huu uwe wa
mfano,’’ alisema Waziri Mhagama ambae pia aliambatana na Mkuu wa mkoa wa
Morogoro Dk Stephen Kebwe, Mbunge Jimbo
la Morogoro Kusini Mashariki Omari Mgumba pamoja na
wawakilishi wa kampuni ya Mkulazi Holding inayosimamia utekelezaji wa mradi huo
pamoja na viongozi wengine wa serikali.
Waziri Mhagama aliwaomba
watekelezaji wa mradi huo kuainisha mapema aina ya rasilimali watu
watakaohitajika kwenye mradi ili waanze kuandaliwa mapema kuepuka suala la
kuagiza wataalamu kutoka nje ya nchi kuja kufanya kazi ambazo zingeweza
kufanywa na wataalamu wa ndani iwapo wangeandaliwa mapema.
Kwa upande wake Waziri
Mpango alisema tayari serikali imeshatenga sh bilioni 17 katika mwaka wa fedha
2016/2017 kwa ajili ya kumalizia fidia na mipaka kwa wakazi wanaoishi kwenye
shamba la miwa kwa ajili ya kiwanda hicho lenye ukubwa wa ekari 63,000.
“Lengo kubwa hapa ni
kuzalisha sukari itakayotuwezesha kukidhi mahitaji yetu ya ndani na kuuza nje
ya nchi pamoja na bidhaa ambatano ikiwemo ethanol. Pia nitoe wito kwa vijana wa
eneo hili kuhakikisha wanakuwa katika vikundi ambavyo vitawawezesha kutekeleza
kwa urahisi miradi mbalimbali ikiwemo kuanzisha mashamba yatakayosaidia
kuongeza malighafi kwa kiwanda hiki,’’ alisema.
Zaidi Dk. Mpango
aliwataka viongozi wa serikali wilayani humo wakiwemo wahandisi
kuhakikisha wanatoka maofisini ili kukagua ujenzi wa miundombinu inayoambatana
na mradi huo ikiwemo barabara inayojengwa na kampuni ya ujenzi ya SUMA JKT
kuelekea eneo la mradi.
“Ile barabara ndio
itatumika kusafirisha bidhaa mbalimbali kutoka na kuelekea kiwandani na iwapo
itatengenezwa chini ya kiwango kutokana na uzembe tu wa kushindwa kumsimamia
mkandarasi hatutaelewana,’’ alisema Dk Mpango huku akiionya kampuni ya SUMA JKT
kutekeleza mradi huo kwa viwango vya ubora ili kulinda imani ya serikali kwa
makampuni ya umma katika utekelezaji wa miradi yake mbalimbali.
Kwa upande wake Dr Kebwe
mbali na kuahidi kuusimamia vema mradi huo hadi kukamilika kwake, alitoa wito
kwa vijana wa eneo hilo kuhakikisha wanafanya kazi badala ya kuwategemea
zaidi wakina mama na wazee kwenye shughuli za uzalishaji.
“Ninazo takwimu
zinazoonyesha kuwa katika kata hii wakina mama na wazee ndio wanaofanya kazi
zaidi kuliko vijana na kwa mujibu wa takwimu hizo wakina mama na wazee
wanafanya kazi kwa asilimia 68 huku vijana mpo…mbadilike!,’’ alionya.
No comments:
Post a Comment