Thursday, December 8, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI


SIMU.TV: Baadhi ya wachimbaji mchanga wilayani Bukoba mkoani Kagera wameitaka serikali kuangalia upya utozaji tozo kwa safari za magari yanayochukua mchanga huo; https://youtu.be/6hCOfEZ-wWM

SIMU.TV: Siku chache baada ya wachimbaji wadogo wa dhahabu katika kijiji cha Nyaligongo wilayani Shinyanga kuruhusiwa na Rais Magufuli kuendelea na uchimbaji, wameibuka na kusifu tamko hilo; https://youtu.be/zqAOsbEULzs

SIMU.TV: Rais Dkt John Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na mke wa mwanzilishi wa taifa la Sudan Kusini Rebecca Mabior ili kutatua mgogoro wa nchi hiyo; https://youtu.be/bqXOD-NOVpA

SIMU.TV: Rais Dkt Magufuli anatarajia kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania ambapo maandalizi ya sherehe hizo tayari yamekamilika; https://youtu.be/pUtBUkRSMiQ

SIMU.TV: Kuelekea maadhimisho ya miaka 55 ya Uhuru, baadhi ya wazee mkoani Iringa wamewataka watanzania kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli; https://youtu.be/89LslhE0jgY

SIMU.TV: Serikali imesema imeridhishwa na zoezi la upanuzi wa barabara ya Alli Hassan Mwinyi kuanzia eneo la Morocco mpaka Mwenge; https://youtu.be/JB1mHYZOsIk

SIMU.TV: Waziri wa viwanda, biashara na uwekezaji Charles Mwijage amezitaka halmashauri nchini kufungua viwanda vidogo vidogo ili kupunguza tatizo la ajira; https://youtu.be/kLilomT8sts

SIMU.TV: Wakati huo huo waziri wa viwanda na biashara wa nchini Rwanda amesema wanategemea bandari ya Dar Es salaam katika kusafirisha mizigo kwenda nchini humo; https://youtu.be/3q5GFAl_B0w

SIMU.TV: Mfumuko wa bei wa taifa kwa mwezi Novemba umeongezeka na kufikia asilimia 4.8 ukilinganiasha na hali ilivyokuwa ya 4.5 kwa mwezi uliopita; https://youtu.be/26blz7lzKK8

SIMU.TV: Mtandao wa wakulima nchini Tanzania umewataka wakulima nchini kujiunga na bima za kilimo ili waweze kuwa kinga dhidi ya mazao yao; https://youtu.be/fzdpI8-PX7s  

SIMU.TV: Mashindano ya masumbwi ya mabingwa wa mabingwa kwa nchi za Afrika mashariki yanatarajia kuanza hapo kesho jijini Dar Es salaam huku mabondia wanawake wakijinasibu kushinda; https://youtu.be/WfT5TG1s5Lo

SIMU.TV: Timu ya taifa ya soka la ufukweni ya Tanzania kesho inashuka dimbani kucheza mchezo wa kirafiki na timu ya taifa ya mchezo ya Uganda; https://youtu.be/dISbdIr_R3c

SIMU.TV: Shirika la utangazaji visiwani Zanzibar limeandaa mashindano ya soka la vijana chini ya miaka 17 ili kurudisha hadhi ya michezo visiwani humo; https://youtu.be/XSXYHMo1EAA

SIMU.TV: Mashindano ya kombe la dunia kwa siku zijazo yanaweza kuwa na mabadiliko kwa kuongezeka kwa timu baada ya Rais wa sasa wa FIFA kuonekana kuvutiwa sana na mpango huo; https://youtu.be/ZlqyHY_jBRs

No comments: