Monday, December 26, 2016

Safari ya Mwisho ya Mpiganaji katika tasnia ya Habari, Marehemu Mpoki Bukuku

Na Humphrey Shao ,Globu ya Jamii
Waziri wa habari, utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Nnauye amesema  amejifunza mengi kupitia kazi za mwandishi na mpiga picha wa kampuni ya TheGurdianLtd marehemu Mpoki Bukuku kutokana na mchango wake  mkubwa katika tasnia ya habari.
"Bukuku ameacha pengo kubwa hivyo hatosahaulika... wanahabari hatuna cha kufanya ila tunamshukuru Mungu na kupitia kazi zake tujifunze yale yote aliyoyafanya," alisema.
Akisoma historia ya Bukuku, kaka wa marehemu, Alfred Mwakaposa alisema marehemu alizaliwa 15/3/1972 katika Hospitali ya Mount Meru mkoani Arusha,  akiwa mtoto wa tano kwenye familia ya Bukuku.
Alisema alianza elimu ya msingi katika Shule ya Forodhani, Mlimwa Dodoma na baadae kuhamia Kisarawe, elimu ya sekondari alisoma Canon Andrea mkoani Dodoma na kidato cha tano na sita katika Shule ya Makumira Arusha.
"Baadaye marehemu alijiunga na elimu ya chuo cha uandishi wa habari TSJ ngazi ya cheti na Diploma... Amewahi kufanya kazi katika gazeti la Majira, Mwananchi na kuhamia Guardian mpaka mauti yalipomfika," alisema.
Akizungumza kwa niaba ya wasanii wa filamu, Muigizaji maarufu Steve Nyerere alisema tasnia ya filamu imepata pigo kubwa kumpoteza Bukuku hivyo wanaamini anapoenda ni sehemu nzuri.
"Nimemjua Mpoki wakati tupo Singida, tunaamini anapoenda Mpoki ni sehemu nzuri, tuko pamoja na familia yake, " alisema. 
Jeneza lenye mwili wa mpiga picha maarufu Marehemu Mpoki Bukuku likiwa katika eneo la uwanja wa Shule ya Wazazi, Tabata Kimanga jijini Dar mchana huu tayari kwa kutoa heshima za mwisho 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Nape Moses Nnauye akizungumza jambo wakati wa kuagwa kwa mwili wa mpiga picha maarufu  Mpoki Bukuku  katika eneo la uwanja wa Shule ya Wazazi, Tabata Kimanga jijini Dar mchana huu.
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe akizungumza jambo wakati wa kuagwa kwa mwili wa mpiga picha maarufu  Mpoki Bukuku.
Mbunge wa jimbo la Ubungo, Saed Kubenea akitoa salamu za pole kwa familia ya Marehemu Mpoki Bukuku wakati wa kuagwa kwa mwili huo.
Mpigapicha Mkuu wa gazeti la Jambo Lelo pamoja na Muwakilishi wa Bloggers, Richard Mwaikenda akitoa salamu za rambirambi katika Msiba wa Mpoki Bukuku, viwanja vya Shule ya Wazazi, Tabata Kimanga jijini Dar.

Baadhi ya waombolezaji wa wakiwa kwenye shughuli ya kuagwa kwa mwili wa marehemu Mpoki Bukuku katika uwanja wa Shule ya Wazazi, Tabata Kimanga jijini Dar mchana huu.No comments: