Wednesday, December 21, 2016

NSSF YATOA MSAADA WA VIFAA TIBA HOSPITALI YA AMANA


Meneja Kiongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Xavier Lukuvi (kushoto), akimkabidhi sehemu ya msaada wa vifaa tiba zikiwemo dawa na mashuka muuguzi kiongozi wa wodi ya wazazi katika hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam, Scolastica Bayongo katika hafla iliyofanyika hospitalini hapo.
Wafanyakazi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), wakitandika kitanda katika wodi ya wazazi katika hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam, baada ya kukabidhi msaada wa mashuka na madawa katika hospitali hiyo.


Muuguzi Kiongozi wa wodi ya wazazi katika hospitali ya Amana, Scolastica Bayongo (kushoto), akisaidiana na Ofisa Uhusiano Mwandamizi wa NSSF, Amina Mmbaga (katikati), na Ofisa Mkuu Mwandamizi Uhusiano na Masoko wa NSSF, Theopista Muheta.
Meneja Kiongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Xavier Lukuvi (kushoto), akimkabidhi sehemu ya msaada wa madawa na mashuka daktari katika wodi ya wazazi, Dk. Ally Mzaha katika hafla iliyofanyika hospitalini hapo.
Kuwafariji wazazi.
Ofisa Uhusiuano na Masoko wa NSSF, Kiamba Rajab akiwagawia zawadi kwa akina mama katika wodi ya wazazi.
Ofisa Uhusiano na Masoko wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Kiamba Rajab akitoa fulana kwa wazazi waliolazwa katika wodi ya akinamama hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam, NSSF ilitoa msaada wa Dawa pamoja na Mashuka katika wodi hiyo.
Meneja Kiongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Xavier Lukuvi (kushoto), akimkabidhi sehemu ya msaada wa madawa na mashuka daktari katika wodi ya wazazi, Dk. Ally Mzaha katika hafla iliyofanyika hospitalini hapo.
Meneja Kiongozi wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), Xavier Lukuvi akizungumza na waandishi wa habari.



NA GLORY CHACKY

MFUKO wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) umetoa msaada wa mashuka 80 na dawa mbalimbali katika Hospitali ya Rufaa ya Wilaya ya Ilala, Amana kwaajili ya wazazi na watoto wachanga.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Meneja Kiongozi wa NSSF Wilaya ya Ilala Xavier Lukuvi alisema lengo la msaada huo ni kusaidia kuboresha huduma kwa kundi hilo ambalo linahitaji uangalizi maalumu.

Alisema mashuka hayo na dawa, vyote vina thamani ya Sh. milioni 3.5 ni sehemu ya kurudisha fadhila kwa jamii wanaoishi katika Wilaya hiyo ambapo hospitali ya Amana ni miongoni mwa hospitali zinazotoa huduma za matibabu kupitia fao la NSSF (SHIB).

"Hii ni kuimarisha ujirani kwa kuwakumbuka wateja wetu ambao tumekuwa tukifanya nao kazi kwa muda mrefu, na tunatambua changamoto iliyopo katika huduma za afya hasa kwa watoto na wanawake" alisema Lukuvi.

Kwa upande wake Mganga katika wodi ya Wazazi Ally Mzaha alisema msaada huo umekuja muda muafaka kwani kwasasa kuna tatizo kubwa la mashuka na dawa kutokana na idadi ya wagonjwa wanaowapokea.

"Jambo hili limekuja muda mwafaka ambao idadi ya wagonjwa katika wodi yetu ni kubwa kuliko uwezo wake, hivi tulivyopata leo vitasaidia kupunguza tatizo hili kwa kiasi fulani.

No comments: