Tuesday, December 27, 2016

Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW) kuwanufaisha wanawake wengi nchini Tanzania

Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani "WOMAN ON WHEEL" (WOW) umelenga kuwapa fursa wanawake kujiajiri na kuajiriwa katika sekta ya usafirishaji kwa kuendesha vyombo vya moto vya abiria na mizigo.
Mradi wa WOW kwa sasa unasajili wanawake kwa ajili ya kuwapatia fursa ya kufundishwa udereva bure katika viwango mbalimbali na baadae kuwatafutia ajira na wengine kuwawezesha ili waweze kujiajiri.
Mradi wa WOW umelenga katika kipindi cha mwezi Disemba hadi Februari uwe umesajili wanawake 600 nchi nzima ili waweze kupatiwa mafunzo.
Lengo kubwa la mradi ni kuondoa mila potofu za mfumo dume wa uwepo wa kazi za kiume na kike.
Mradi wa WOW utawezesha wanawake kushiriki kikamilifu kuchangia pato la taifa kwa kujiwezesha kulipa kodi mbalmbali za serikali kupitia sekta ya usafirishaji.
1
Martin Gabone-Mkurugenzi Mkuu Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW) akizungumza na washiriki wa semina hiyo ya siku moja hawapo pichani, iliyolenga kuwapa fursa wanawake kujiajiri na kuajiriwa katika sekta ya usafirishaji kwa kuendesha vyombo vya moto vya abiria na mizigo kupitia mradi huo.
2
Martin Gabone-Mkurugenzi Mkuu Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW) akizungumza na washiriki wa semina hiyo ya siku moja , iliyolenga kuwapa fursa wanawake kujiajiri na kuajiriwa katika sekta ya usafirishaji kwa kuendesha vyombo vya moto vya abiria na mizigo kupitia mradi huo.
3
Baadhi ya wanawake washiriki wa semina hiyo ya siku moja wakifurahia maelezo na umuhimu wa Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW).
4
Baadhi ya wanawake washiriki wa semina hiyo ya siku moja wakifuuatilia maelezo ya umuhimu wa Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW).
5
Victor Francis-Meneja Mafunzo wa Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW) akielezea jambo wakati alipotoa mafunzo kwa wanawake washiriki wa semina hiyo.
6
Victor Francis-Meneja Mafunzo wa Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW) akifafanua jambo huku akisikilizwa kwa makini na baadhi ya washiriki.
7
Baadhi ya washiriki wakifuatilia maelezo kutoka kwa Victor Francis-Meneja Mafunzo wa Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW)
8
Victor Francis-Meneja Mafunzo wa Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW) akitoa maelekezo kwa baadhi ya washiriki wa semina hiyo.
9
Victor Francis-Meneja Mafunzo wa Mradi wa Wanawake Kwenye Usukani (WOW) akigawa baadhi ya vipeperushi vyenye maelezo muhimu kuhusu mradi huo.

1 comment:

Thobias Omega said...

Nice idea, nimependa huu Mradi.....pls naomba contacts za viongozi wa mradi nahitaji kuwasiliana nao pls
0742125315
0653509917