Sunday, December 25, 2016

MKUU WA WILAYA YA ILALA AWAAGIZA POLISI KUACHA KUWANYANYASA WAENDESHA BODABODA



Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

MKUU wa Wilaya Ilala, Sophia Mjema ameagiza polisi kuacha mara moja kuwanyanyasa waendesha bodaboda na kutaka polisi kutumia mashine ya EFD pale wanapotoa faini kwa bodaboda hao.

Kutumia mashine za EFD kutawafanya waendesha bodaboda kulipa ndani ya siku saba kama wanavyofanya kwa wenye bodaboda.

Hata hivyo amesema maagizo ya mkuu wa Mkoa ya askari mgambo na ulinzi shirikishi wafanye kazi na watendaji wa kata na kuhoji kuwa mgambo na ulinzi shirikishi wanapenda kazi ya kukamata bodaboda.

Mkuu wa Wilaya ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa bonanza la bodaboda jana lililofanyika Pugu, Jijini Dar es Salaam, Sophia amesema kunyanyasika kwa bodaboda kunatokana na baadhi yao kutotambua umuhimu wa kazi zao.Alifafanua kuwa “Ulinzi shirikishi na mgambo ni marufuku kuwasumbua bodäboda, kwani wanayo haki ya kufanya kazi na kuishi kwa amani kama ilivyo”.

Sophia amesema licha ya kuwepo kero za bodaboda kukamatwa inatokana na baadhi yao kutopewa elimu ya usalama barabarani hivyo lazima wapewe elimu hata wakikosea watajua.Amesema wakati umefika wa kazi za bodaboda kuheshimika kudharau kazi hiyo inafanya wafanye kazi bila uhakika.

Hata hivyo amesema kutokana na kupata malalamiko atafanya mkutano kati ya bodaboda na jeshi la polisi kwa ajili ya kutoa elimu ya pamoja na kutatua sintofahamu zinazojitokeza kwa bodaboda.
.Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akiwa katika pikipiki kabla ya uzinduzi wa bonanza la Bodaboda Pugu jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akizungumza na waendesha bodaboda katika uzinduzi wa bonanza Pugu, jijini Dar es Salaam.Picha zote na Emmanuel Massaka,Globu ya Jamii.
Mrakibu Msaidizi wa Jeshi Polisi (ASP),Charle’s Kanyunyu akizungumza katika uzinduzi wa bonanza jana Pugu, jijini Dar es Salaam.
Katibu wa Bodaboda wa Kituo cha Mombasa, Athuman Omary, akitoa kero wanazokutana nazo katika madereva wa bodaboda katika uzinduzi wa bonanza jana Pugu, jijini Dar es Salaam.
Sehemu mdereva wa Bodaboda wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya Ilala, Sophia Mjema katika uzinduzi wa bonanza la Bodaboda Pugu jijini Dar es Salaam.

No comments: