Sunday, December 18, 2016

MHANDISI NGONYANI AMUAGIZA MKANDARASI KUMALIZA UJENZI MAPEMA

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani (Wa tatu kulia) akijadiliana jambo na Mkandarasi wa kampuni ya Rv associates India& AES Tanzania anayejenga Daraja la Kilombero. Daraja hilo lipo katika barabara kuu ya Ifakara –Mahenge Mkoani Morogoro.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani amemuagiza Mkandarasi wa kampuni ya Rv associates India & AES Tanzania  anayejenga daraja la Kilombero lenye urefu wa mita 384 kukamilisha ujenzi huo mapema ifikapo januari mwakani  ili daraja hilo lianze kutumiwa na wananchi wa Mkoa wa Morogoro.

Mhandisi Ngonyani ametoa agizo mara baada ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa daraja hilo lenye urefu wa mita 384 linalounganisha  barabara kuu ya Ifakara –Mahenge mkoni Morogoro.

“Wananchi wa Ifakara wanahamu ya kuona daraja hili linakamilika na kuanza kutumika mapema, hivyo ongezeni kasi ya ujenzi wa daraja hili ili likamilike haraka na kwa ubora uliokusudiwa ili liweze kudumu na kutumika kwa muda mrefu”. amesisitiza Mhandisi Ngonyani.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani (Wa kwanza kushoto) akipata maelezo Ujenzi wa Daraja la Kilombero kutoka kwa Mkandarasi wa kampuni ya Rv associates India& AES Tanzania. Daraja hilo lipo katika barabara kuu ya Ifakara –Mahenge Mkoani Morogoro.

Ameongeza kuwa kukamilka kwa daraja hilo kutawafanya wananchi kuachana na usafiri wa kutumia kivuko cha Mv. Kilombero ambacho wakati wa mvua kubwa hushindwa kutoa huduma za usafiri kwa wananchi hao na hivyo kukwamisha shughuli zao za kimaendeleo.

Katika hatua nyingine Mhandisi Ngonyani amekagua barabara ya kuu ya kitaifa (Trunk roads) ya kutoka Mikumi-Mahenge, Kilosa kwa mpepo-Londo ambopo amesema kuwa Serikali itaanza ujenzi wa barabara ya Kidatu –Ifakara(KM 67) kwa kiwango cha lami ifikapo machi mwakani wakati barabara ya Lupilo hadi Lumecha upembuzi yakinifu unaendelea.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa halmashauri ya mji Ifakara Bw. Mashaka Mbilinyi ameelezea umuhimu wa barabara hiyo kuwa itakuwa kichocheo cha mendeleo ya kiuchumi kwa majimbo manne ya Mlimba, Malinyi, Ulanga na Kilombero.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani (Wa pili kulia), akiendelea na ukaguzi wa sehemu ya juu ya daraja la Kilombero.

“Barabara hii itakapokamilika itawawezesha wananchi kupata huduma katika sehemu mbalimbali za majimbo yetu na pia kusafirisha kusafirisha mizigo ya nafaka kwenda katika masoko mbalimbali na hivyo kukuza kipato cha mwananchi na taifa kwa ujumla”. amesema Bw. Mbilinyi.

Naye Mbunge wa Jimmbo la Mlimba Mhe. Suzani Kiwanga na Mbunge wa Kilombero Mhe. Peter Lijuakali kwa pamoja wameishukuru Serikali na kusema kuwa ujenzi wa barabara hiyo itakuwa mkombozi kwa wananchi wa kanda ya Kusini kwa vile itaunganisha Kilombero, Malinyi na Ulanga na Mkoa wa Ruvuma.

Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani yupo Mkoani Morogoro kwa ziara ya kukagua Miundombinu ya barabara, Madaraja na Reli.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani (Wa kwanza kushoto) akipata maelezo ya ramani ya Ujenzi wa Daraja la Kilombero kutoka kwa Mkandarasi wa kampuni ya Rv associates India& AES Tanzania. Daraja hilo lipo katika barabara kuu ya Ifakara –Mahenge Mkoani Morogoro.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani (aliyenyoosha kidole) akitoa maelekezo kwa Mkandarasi wa kampuni ya Rv associates India&AES Tanzania anayejenga Daraja la Kilombero. Daraja hilo lipo katika barabara kuu ya Ifakara –Mahenge Mkoani Morogoro.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani (Mbele) akitoa akisisitiza jambo kwa Mkandarasi wa kampuni ya Rv associates India& AES Tanzania anayejenga Daraja la Kilombero. Daraja hilo lipo katika barabara kuu ya Ifakara –Mahenge Mkoani Morogoro.
Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani (Wa tatu kushoto) akifafanua jambo kwa Mkandarasi wa kampuni ya Rv associates India&AES Tanzania anayejenga Daraja la Kilombero.Daraja hilo lipo katika barabara kuu ya Ifakara –Mahenge Mkoani Morogoro.
Muonekano wa Daraja la Kilombero lenye urefu wa Mita 384 ambapo ujenzi wake unaendelea, Daraja hilo lipo katika barabara kuu ya Ifakara –Mahenge Mkoani Morogoro. Picha na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

No comments: