Saturday, December 17, 2016

.MAHAFALI YA NNE YA CHUO KIKUU CHA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA (MUST) YANOGA

Kutoka kushoto ni Naibu Katibu Mkuu  Waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mhe. Simon Msanjila, Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia (MUST)  Profesa Mark Mwandosya na mwenyeketi wa baraza la chuo kikuu cha sayansi na teknolojia Profesa Penina Mlama kwa pamoja wakiwa katika maandamano kuelekea katika ukumbi wa Nyerere kabla ya hafla kuanza.Naibu Katibu Mkuu wa Elimu Sayansi na Teknolojia Mh.Simon Msanjila akihutubia katika hafla hiyo ya mahafali ya nne ya Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia (Mbeya University of Science and Technology - MUST) kilichopo mkoani mbeya, Mh.Msanjila amekipongeza chuo hicho kwa kuongeza baadhi ya mafunzo ikiwemo mafunzo ya ufindi na mafunzo ya sayansi ya kiafya kwa kushirikiana na hospitali ya Rufaa mkoani mbeya.Pia mh.Simon Msanjila ametoa wito kwa kila mtu mwenye uwezo wa kujifunsa mafunzo ya sayansi na teknolojia yatolewayo katika chuo kikuu cha sayansi na teknolojia kilichopo mkoani mbeya na kuwataka wahitimu kuzikimbilia fursa mbalimbali  haswa katika harakati za kutafuta ajira. Sehemu  ya wahitimu wa stashahada ya kawaida na stashahada ya kwanza katika fani mbalimbali za sayansi na teknolojia wakitunukiwa. Jumla ya wahitiumu wote waliomaliza kozi mbalimbali ni 804 ambapo idadi kubwa ni jinsia ya kime.Wahitimu sambamba na wageni waalikwa na wafanyakazi wa chuo hicho cha sayansi na teknolojia walio hudhuria hafla hiyo ya mahafali ya nne ya MUST yaliyofanyika katika ukumbi wa Nyerere uliopo chuoni hapo mkoani Mbeya.PICHA NA MR.PENGO WA MMG MBEYA.

No comments: