Saturday, December 3, 2016

MAHAFALI YA CHUO KIKUU MUHIMBILI YAFANA, SABA WATUNUKIWA SHAHADA ZA UZAMIVU


Na Zainab Nyamka, 
Globu ya Jamii

MAHAFALI ya 10 Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) yafana kwa wahitimu 944 kutunukiwa shahada mbalimbali za masomo ya Afya huku Mkuu wa Chuo Rais Mstaafu, Alhaji D Ali Hassan Mwinyi akiwatunukiwa wanafunzi saba shahadan ya uzamivu.
Mahafali hayo yaliyofanyika leo Jijini Dar es salaam, Makamu Mkuu wa Chuo MUHAS, Ephata Kaaya amesema kuwa azma ya Chuo chao ni kuwa na wanafunzi wa kike na wakiume kwa idadi sawa kwani katika mwaka huu wa mahafali wanafunzi 372 sawa na aslimia 39.4 ni wanawake kwahiyo bado wanaendela na mpango wa kuwawezesha wanafunzi wa kike kujikunga na programu mbalimbali zinazotolewa hapa chuoni.
Kaaya amesema kuwa , katika kuendeleza kutoa nafasi kwa wanafunzi MUHAS wamefanikiwa kupata imefanikiwa kukamilisha ukarabati wa kliniki mpya ya wagonjwa wa afya ya kinywa na meno watakaokuwa wanajilipia wenyewe na vifaa tiba vimeshapayikana kutoka shirika lisilo la kiserikali la The Miracle Corners Of the World (MCW)la Nchini Marekani na vinategemewa kuwaili nchini na kufungwa kwenye kliniki hiyo mwezi Januari.
Katika ,mahafali hayo, wahitimu saba waliweza kutunukiwa shahada za uzamivu kwa kufanya tafiti mbalimbali za magonjwa na dawa ambao ni Siana Nkya,Ramadhan Nondo, Dickson Mkoka, Gladys Mahiti, Grace Shayo, Coline Mahende na Richard Mwaiselo.
Mkuu wa Chuo pia aliweza kuwatunukiwa wahitimu wawili wa shahada ya uzamili wa Sayansi Maalumu ambao ni Mohamed Mnacho na John Ngendahayo huku wahitimu nane wakipatiwa shahada ya juu katika masuala mbalimbali pia 183 shahada ya uzamili na wahitimu 376 walitunukiwa stashahada,

















Makamu Mkuu wa Chuo Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS) Profesa Ephata Kaaya akitoa hotuba kwa wahitimu wa Chuo hicho katika mahafali ya 10 yaliyofanyika leo Jijini Dar es salaam, Kulia ni Mkuu wa Chuo hicho cha MUHAS, Rais Mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi na Mwenyekiti wa MUHAS  Mariam Joy Mwafisi.






 Mkuu wa Chuo 
 Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (



MUHAS), Rais Mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi na akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Chuo cha Afya na Syansi Shirikishi kwenye mahafali ya 10 yaliyofanyika chuoni hapo leo Jijini Dar es salaam.

















































 Mkuu wa Chuo Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS), Rais Mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi akimtunuku Shahada ya uzamivu (PhD) Grace Shayo katika mahafali  ya 10 yaliyofanyika leo Jijini Dar es salaam.



















































Mkuu wa Chuo Cha Afya na Sayansi Shirikishi  Muhimbili (MUHAS), Rais Mstaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi akiwa anaingia katika Uwanja wa mahafali ya chuo hicho akiambatana na viongozi mbalimbali wa MUHAS yaliyofanyika leo Jijini Dar es salaam.


Wahitimu wakiwa wanaingia Uwanja wa Mahafali ya 
Chuo Kikuu Cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).

Wahitimu wa Chuo Cha Afya na Sayansi Shirikishi  
 Muhimbili wakisubiri kutunukiwa shahada mbalimbali.
Wahitimu wa Chuo Cha Afya na Sayansi Shirikishi  
 Muhimbili wakisubiri kutunukiwa shahada mbalimbali. 

Wahitimu wa Chuo Cha Afya na Sayansi Shirikishi  
 Muhimbili wakisubiri kutunukiwa shahada mbalimbali. 






Wahitimu wa Chuo Cha Afya na Sayansi Shirikishi  M
uhimbili wakisubiri kutunukiwa shahada mbalimbali. 
Picha zote na Zainab Nyamka.


No comments: