Tuesday, December 20, 2016

M-PAPER INAVYOWEZA KURAHISISHA HUDUMA MBALIMBALI

Kutokana na maendeleo ya Sayansi na Teknolojia, kwa sasa maisha yamerahisishwa sana. Huna haja ya kutumia nguvu kubwa sana kutafuta bidhaa. Unaweza kukaa ndani tu na ukafanya manunuzi yako kwa kutumia simu yako ya mkononi tu na bidhaa ikakufikia popote ulipo bila hata ya kutoa jasho. Huo ndio urahisi ambao huduma ya M-PAPER inakuletea. 


  M-PAPER ni nini?


M-PAPER ni huduma ambayo inakufanya wewe mfuatiliaji wa habari kwa njia ya magazeti na majarida, kusoma magazeti na majarida uyapendayo kwa kutumia simu yako ya mkononi ambapo utaweza kusoma ukurasa wa kwanza hadi wa mwisho kwa nusu bei ya gazeti halisi. Kwa mfano kama gazeti halisi unalonunua mtaani linauzwa Sh 1000/= basi ukilinunua na kulisoma kupitia M-PAPER litakuwa na gharama ya Sh 500/= tu.

Ni magazeti/majarida yapi yanapatikana kwenye huduma hii ya M-PAPER?

Kupitia App ya M-PAPER utaweza kusoma magazeti mbali mbali kama vile Tabibu, Uhuru, Rai, Tanzania Daima, HabariLeo, The Citizen, Majira, JamboLeo, Daily News, Mtanzania, Raia mwema, Mzalendo, Mwanahalisi na pia yakiwemo magazeti yako pendwa ya Michezo na Burudani kama vile Dimba, Bingwa, Mwana Soka na SpotiLeo.


Unawezaje kuipata huduma ya M-PAPER?


Huduma hii inapatikana kwa njia kuu MBILI ambazo ni mtandaoni kupitia link ya www.mpaper.co.tz au kwa kudownload App iitwayo M-PAPER inayopatikana Google Store kwa wale watumiaji wa simu za Android na App Store kwa wale watumiaji wa simu zinazotumia mfumo wa iOS.

Nawezaje kujiunga na huduma hii ya M-PAPER?

Zifuatazo ni hatua za kujiunga na huduma ya M-PAPER kupita ile njia ya ku-download app..Soma maelezo kisha husishanisha na picha inayoonekana chini kwa mifano zaidi. (Kwa simu za Android tu)

1.      Ingia kwenye Google Play au App Store kwenye simu yako ya mkononi kisha andika M-PAPER kisha bonyeza INSTALL

2.      Baada ya ku-install app kwenye simu yako, Chagua Lugha kati ya KIINGEREZA au KISWAHILI

3.      Baada ya hapo ingiza naomba yako ya simu kwa wale watumiaji wa mtandao wa Vodacom

4.      Ukishaweka namba ya simu, utatumiwa namba ya uthibitisho kwa njia ya SMS kwenye namba yako ambapo utaweka namba hiyo uliyotumiwa kwenye sehemu unayotakiwa kujaza

5.      Baada ya hapo sasa utaweza kuyaona magazeti yote na majarida yanayopatikana.


 Nawezaje kununua gazeti au jarida baada ya kujiunga?


Utaweza kununua gazeti kupitia M-PAPER baada ya kuongeza salio kwenye akaunti yako kwa kutumia akaunti yako ya M-Pesa, muda wa kawaida wa maongezi (Airtime) AU kupitia kadi zako za malipo za benki (Credit Cards) kama inavyoonekana kwenye picha namba moja hapo chini.

Kuongeza salio kupitia kwenye akaunti yako ya M-Pesa fuata utaratibu kama inavyoonekana kwenye picha namba tatu hapo chini ambazo ni:

1.      Piga *150*00#

2.      Chagua 4 Lipa kwa M-Pesa

3.      Chagua 3 kwenye orodha

4.      Chagua 5 Vodacom

5.      Chagua 4 M-Paper

6.      Weka namba yako ya Kumbukumbu ambayo utaiona ukibonyeza akaunti yangu Mfano:( 117524)

7.      Weka kiwango

8.      Weka PIN Kulipa

9.      Utapokea ujumbe wa udhibitisho wa malipo.


 Kuongeza salio kupitia Salio la kawaida kwenye simu yako, utatakiwa kubongeza kitufe cha Muda wa Maongezi kwenye picha namba moja hapo chini, kisha utaweka kiasi unachotaka kuongeza kama inavyooneka kwenye picha namba mbili, na vivyo hivyo kwa kutumia credit cards kama inavyoonekana kwenye picha namba nne hapo chini ambapo utachagua huduma unayotaka kutumia.


Unaweza kusoma magazeti yote ya siku/wiki/mwezi husika bila kikomo kwa kununua vifurushi vya siku, wiki au mwezi kama inavyooneka kwenye picha namba tano hapo chini ambapo kifurushi cha wiki kitagharimu Sh 499/=, cha mwezi Sh 2,999/= na cha mwezi Sh 11,999/=



NB:

Mchakato wote huu wa kujiunga na M-PAPER ni kwa simu za Android tu, tutazungumzia mchakato kwa wale watumiaji wa iPhone siku nyingine.

Kama wewe sio mtumiaji wa mtandao wa Vodacom, unaweza kujiunga kupitia Facebook au Email na ukafanya malipo kupitia credit cards au ukatumiwa salio kutoka M-Pesa na rafiki yako mwenye namba ya Vodacom kuja kwenye namba yako.

No comments: