Wednesday, December 28, 2016

JAFO AFANYA ZIARA WILAYANI MANYONI MKOA WA SINGIDA

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo akiangalia
kitanda ambacho kinatumiwa na akina mama wajawazito wakati wa
kujifungua katika Hospitali ya wilaya ya Itigi mkoani singida wakati
alipofanya ziara ya kushtukiza. Kulia kwake ni Dkt. Mary Rume Kaimu
Mganga Mkuu wa Wilaya Itigi na anayefuatia ni Mkuu wa wilaya Manyoni
Geoffrey Mwambe.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo
akimsikiliza Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya Itigi Pius Luhende
wakati alipokuwa akitoa maelezo ya namna walivyojipanga kushughulikia
kero ya wodi ya wazazi katika Hospitali ya wilaya ya Itigi mkoani
singida.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo akipata
maelezo toka kwa Agnesi Katumbo juu ya kusitishwa kwa kutolewa kwa
risiti za kielectroniki ambayo ni kinyume na utaratibu wa Serikali na
kutoa wiki moja kurudisha huduma hiyo ambayo ni chanzo cha kupotea kwa
fedha za Serikali.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Selemani Jafo akipata
maelezo toka Mkuu wa wilaya Manyoni Geoffrey Mwambe wakati wa ziara
yake aliyoifanya wilayani humo Manyoni na Halmashauri ya Itigi,
alieleza juu ya changamoto za wahamiaji, uharibifu wa mazingira na
tatizo la utoro wa wanafunzi ambalo linasababishwa na wazazi zaidi
katika wilaya hiyo, walio kaa kulia kwake ni Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Manyoni Edward C. Fussi na anayefuata ni Mwenyekiti wa Halmashauri
ya Manyoni Moses Matonya.
Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo
akisisitiza jambo kwa Wakuu wa Idara na baadhi ya watumishi wa
Halmashauri ya Manyoni (hawapo pichani) juu ya uwajibikaji kwa vitendo
na sio kwa mazoea ili kuleta ufanisi sehemu za kazi walio kaa kushoto
kwake ni Mkuu wa wilaya Manyoni Geoffrey Mwambe, Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Manyoni Moses Matonya na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manyoni Edward Fussi

Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo
akimpima uzito mmoja wa watoto katika hospitali ya wilaya ya Manyoni
alipotembelea hospitali hiyo wilayani manyoni leo hii.

……………..

NAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(Tamisemi), Selemani Jafo, amefanya ziara katika halmashauri mpya ya
Itigi na Manyoni huku akibaini uwepo wa changamoto mbalimbali hususan
upungufu wa dawa katika Kituo cha Afya Itigi na Hospitali ya wilaya ya
Manyoni mkoani Singida.
Akizungumza katika ziara hiyo, Jafo amesema mara baada ya kutembelea
Halmashauri hizo amebaini changamoto za dawa katika kituo cha afya
Itigi pamoja na vifaa katika chumba cha mama huku akisema zipo
changamoto ambazo zinazotakiwa kutatuliwa ndani ya halmashauri hiyo.

Jafo akizungumza kuhusu suala la upatikanaji wa dawa, amesema tatizo
hilo linaonekana ni kikwazo kutokana na watendaji kushindwa kutumia
fedha za dharura wanazopewa na serikali kununulia dawa na vifaa tiba.

“Naziagiza Halmashauri hizi kuhakikisha zinaweka kipaumbele uboreshaji
wa vituo vya afya kwa kununua dawa nyingi na vifaa vingine tofauti na
kusubiri zinazotoka Bohari ya Madawa (MSD),”amesema Naibu Waziri huyo

Amewaagiza watendaji wa idara mbalimbali kuhakikisha wanashirikiana na
mkurugenzi wa Itigi ili kutimiza wajibu wao na kuifanya halmashauri
hiyo kuwa bora na kuwaonya kuacha kufanya kazi kwa mazoea.

“Kila mtumishi ahakikishe anajali muda wa kazi na kuacha tabia ya
kutoenda kwa ratiba ya kazi, watumishi wa Tamisemi wanatakiwa
kujiamini katika kazi zao na kuacha uoga ama kufanya kazi hadi pale
wanapofuatiliwa hasa kwenye miradi mbalimbali,”amesema

Kadhalika, Naibu Waziri huyo amewataka wahasibu kuacha tabia ya
kuabudiwa kutokana na kuamua kuidhinisha fedha hadi pale
watakapojisikia na kusababisha miradi mingi kukwama na mingine kufa.

Kwa upande wake, Mganga Mkuu wa hospitali ya wilaya ya Manyoni, Dk.
Francis Mwanisa, amesema hospitali hiyo inakabiliwa na upungufu wa
dawa licha ya kupokea wagonjwa kutoka sehemu mbalimbali nje ya wilaya
hiyo.

No comments: