Na Stella Kalinga
Mkuu wa Mkoa wa
Simiyu Mhe.Anthony Mtaka ameongoza harambee ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ya
Gambosi iliyopo Kata ya Gambosi wilayani Bariadi Mkoani humo.
Harambee hiyo
imefanyika kufuatia azma ya Askofu wa Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA)
Tanzania, Ndg.Mark Malekana kutaka kuunga mkono juhudi za wananchi wa kata
aliyozaliwa ya Gambosi katika ujenzi wa shule hiyo, kwa kuwa watoto wa kata
hiyo wamekuwa wakisoma katika shule ya sekondari Miswaki kata ya jirani ya
Mwasubuya.
Akitoa taarifa ya
ujenzi wa Shule ya Sekondari Gambosi, Kaimu Afisa Mtendaji wa Kata ya Gambosi,
Longino Nasari amesema Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi kwa kushirikiana na
wananchi wameanza kwa kujenga vyumba vitatu vya maabara, jengo la utawala na
matundu 08 ya vyoo.
Askofu Malekana
amewataka wananchi wa Gambosi kushirikiana na Serikali kujenga shule na
miundombinu mingine ya Huduma za Jamii bila kujali tofauti zao za kiitikadi na
dini ili kuitengeneza Gambosi mpya ya tofauti na jinsi inavyodhaniwa na watu
kuwa ni mahali penye mambo ya kishirikina.
Aidha, Askofu
Malekana ametoa wito kwa wananchi wa Gambosi hususani vijana kufanya kazi kwa
bidii ili kuleta maendeleo katika eneo hilo na kubadili fikra na mtazamo wa
watu wengi juu ya eneo hilo.
“Maendeleo hayaji
kwa muujiza wala hayaji kwa bahati mbaya, acheni hadithi za kusema kama Mungu
kakupangia kufa maskini utakufa maskini, au kama ulipangiwa kuwa na tajiri
utakuwa hivyo, hapana Mungu hakupanga hivyo. Muachane kabisa na fikra hizo potofu
fanyeni kazi kwa bidii, mjenge Gambosi Mpya”
Pamoja na
kuhimiza maendeleo Askofu Malekana amewataka wananchi wa Gambosi kudumisha
amani na kuwatengenezea mazingira rafiki watumishi wanaopangwa kufanya kazi katika
eneo hilo ikiwa ni pamoja na kujenga
nyumba za kupangisha ili waone fahari kufanya kazi Gambosi.
Kwa upande wake
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka amewataka wananchi kuona umuhimu wa
elimu na kuwapeleka shule watoto wote wanaopaswa kwenda shule mapema mwezi
Januari, 2017 shule zitakapofunguliwa.
Wakati huo huo
Mtaka amewataka wananchi kuvitumia vituo vya kutolea huduma za Afya pale
wanapougua badala ya kwenda kwa waganga wa jadi ili kupunguza vifo visivyo vya
lazima vinaivyoibua chuki na visasi
vitokanavyo na ramli chonganishi, ikiwa ni pamoja na ukataji wa mapanga kwa
vikongwe kwa imani za kishirikina.
“Tumieni
vituo vyetu vya huduma za Afya vilivyopo
ili mfanyiwe uchunguzi na kupewa tiba kwa gharama nafuu; wazee na watoto
chini ya miaka mitano wanatibiwa bure. Pamoja na unafuu huo unasikia mtu anampeleka
mtoto kwa mganga anachanjwa chale akifikishwa hospitali hana damu hana maji
anakufa, akifa mnaanza kutafuta mchawi, hiyo tabia iachwe kabisa” amesema Mtaka
Katika Harambee
hiyo ya ujenzi wa Shule ya Sekondari Gambosi mifuko 604 ya saruji, nondo 100,
bati 20, misumari kilogramu 7, Madawati 80, Unga wa Ngano mfuko mmoja na mafuta
ya kula katoni 1 kwa ajili ya chakula cha mafundi, vitabu 18 na fedha taslimu vilipatikana,
vyote vikiwa na thamani ya shilingi 21,761,050, ikiwa ni michango ya Askofu wa
Kanisa la SDA Tanzania na wadau wake, Viongozi wa Serikali ya Mkoa na Wilaya,
Wafanyabiashara wa Bariadi na wananchi wa Gambosi.
Mkuu wa Mkoa
amehimiza fedha hizo zitumike kwa makusudi yaliyokusudiwa na ujenzi uendelee
ili kufikia mwaka 2018 shule hiyo ifunguliwe.
Askofu wa Kanisa
la Waadventista Wasabato (SDA), Ndg.Mark Malekana akizungumza na wananchi wa Gambosi(hawapo pichani) wakati wa
Harambee ya Ujenzi wa Shule ya Sekondari Gambosi iliyofanyika jana
katika kijiji cha Gambosi wilayani Bariadi.
Askofu
wa Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA), Ndg.Mark Malekana (kushoto) Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (kulia) wakisaini vitabu vya wageni wakati
wa Harambee ya Ujenzi wa Shule ya
Sekondari Gambosi, iliyofanyika jana katika kijiji cha Gambosi wilayani
Bariadi.
Mkuu
wa wilaya ya Bariadi, Mhe.Festo Kiswaga akizungumza na wananchi wa Gambosi (hawapo
pichani) wakati wa Harambee ya Ujenzi wa
Shule ya Sekondari Gambosi iliyofanyika jana katika kijiji cha Gambosi wilayani
Bariadi.
Kutoka
kulia Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Askofu wa Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA)
wakiwa na viongozi wengine wakati walipotembelea eneo la ujenzi wa Shule ya
Sekondari Gambosi kabla ya kufanya harambee ya ujenzi wa shule hiyo kijijini
Gambosi (Bariadi).
Baadhi
ya wananchi wa Kijiji cha Gambosi wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,
Mhe.Anthony Mtaka (hayupo pichani) wakati wa
Harambee ya Ujenzi wa Shule ya Sekondari Gambosi iliyofanyika jana
kijijini hapo wilayani Bariadi.
Diwani
wa Kata ya Gambosi, Mhe.Bahame Kaliwa akizungumza na wananchi wa Gambosi
(hawapo pichani) wakati wa Harambee ya Ujenzi wa Shule ya Sekondari
Gambosi iliyofanyika jana katika kijiji cha Gambosi wilayani Bariadi.
Paroko
wa Parokia ya Ngulyati wilayani Bariadi akizungumza na wananchi wa Gambosi
(hawapo pichani) wakati wa Harambee ya
Ujenzi wa Shule ya Sekondari Gambosi iliyofanyika jana katika kijiji cha
Gambosi wilayani Bariadi.
Mbunge
wa Jimbo la Itilima ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara Mkoa
wa Simiyu, Mhe.Njalu Silanga akizungumza na wananchi wa Gambosi (hawapo
pichani) kabla ya kuchangia katika
Harambee ya Ujenzi wa Shule ya Sekondari Gambosi iliyofanyika jana
katika kijiji cha Gambosi wilayani Bariadi.
Makamu
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bariadi, Mhe.Duka Mashaurimapya akipeana
mkono na Askofu wa Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA), Ndg.Mark Malekana
baada ya kuwasilisha mchango wa Halmashauri hiyo wakati wa Harambee ya Ujenzi wa Shule ya Sekondari
Gambosi iliyofanyika jana katika kijiji cha Gambosi.
Mwenyekiti
wa Wafanyabiashara Mkoa wa Simiyu na Mbunge wa Itilima ,akipeana mkono na
Diwani wa Kata ya Gambosi Mhe. Bahame Kaliwa, baada ya kuwasilisha mchango wake
wakati wa Harambee ya Ujenzi wa Shule ya
Sekondari Gambosi iliyofanyika jana katika kijiji cha Gambosi.
Askofu
wa Kanisa la Waadventista Wasabato (SDA), Ndg.Mark Malekana akimuonesha Mkuu wa
Mkoa wa Simiyu,Mhe.Anthony Mtaka risiti
aliyopewa baada ya kununua mifuko 100 ya saruji
kwa ajili ya kuchangia Ujenzi wa
Shule ya Sekondari Gambosi.
Baadhi
ya wananchi wa Kijiji cha Gambosi wakienda kuchangia wakati wa Harambee ya Ujenzi
wa Shule ya Sekondari Gambosi iliyofanyika jana katika kijijini hapo.
Mkuu
wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka (kulia) akizungumza na wananchi wa Gambosi
(hawapo pichani) wakati wa Harambee ya Ujenzi
wa Shule ya Sekondari Gambosi iliyofanyika jana katika kijiji cha Gambosi
wilayani Bariadi.
No comments:
Post a Comment