Meya wa jiji la Mbeya David Mwashilindi akisaini Mkataba kwa ajili ya uboreshaji wa Miundombinu ya barabara katika jiji la Mbeya. |
Na JamiiMojaBlog
HALMASHAURI ya Jiji
la Mbeya, leo imeingia mkataba na makandarasi mbalimbali wa ujenzi wa miundombinu
ya barabara pamoja na madaraja katika Kata 14.
Mkataba huo,
umesainiwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Mbeya, David Mwashilindi huku
ukishuhudiwa na baadhi ya madiwani wa Kata husika pamoja na mwanasheria wa
halmashauri hiyo Davis Mbembela.
Awali
akizungumzia tukio hilo kabla ya kusaini, Meya Mwashilindi amesema, mkatba huo,
unalenga kuboresha miundombinu katika
baadhi ya kata katika halmashauri hiyo
ambapo kazi hiyo inataraji kuanza mapema mwezi huu.
Aidha, amesema kuwa mkataba huo unagharimu kiasi cha shilingi
milioni 300 na kwamba kazi kubwa itakayofanyika ni uboreshaji wa barabara na
matengenezo ya madaraja katika kata 14 kati ya 36 zilizomo ndani ya Jiji la
Mbeya.
“Kampuni zilizoingia
mkataba leo ni tano na zote ni makandarasi wa ndani na kubwa zaidi ni wazawa,”amesema.
Pia, Mwashilindi amewataka makandarasi waliochukua
kazi hizo kuhakikisha wanafanya kazi kwa kiwango kinachotakiwa na kwa muda
muafaka huku akiwatoa hofu juu ya fedha, kwani bajeti ya matengenezo hayo
tayari imeidhinishwa..
Hata hivyo,
katika kuhakikisha zoezi hilo linafanikiwa kwa asilimia 100, Mwashilindi
amewataka watendaji pamoja na madiwani kuhakikisha wanatembelea na kukagua miradi
hiyo, wakati ikiendelea kufanyika na kuachana na tabia ya kusubili mradi
ukamilike na kukabidhiwa na ndipo kuanza kubaini kasoro.
“Serikali imekuwa
ikitumia fedha nyingi na asilimia kubwa inatokana na kodi za wananchi hivyo
ninawaombeni madiwani na watumishi hasa wa idara husika kuhakikisha mnatembelea
na kuukagua mradi huu wakati wote wa mchakato, sitapenda kusikia changamoto
mara baada ya mradi kukamilika,”amesema.
Mwisho.
Baadhi ya Wakandarasi wa makampuni mbalimbali ya jiji la Mbeya wakisaini mikataba kwa ajili ya uboreshaji wa miundombinu ya barabara katka baadhi ya kata jijini Mbeya. |
No comments:
Post a Comment