Wednesday, December 7, 2016

DC WA BUHIGWE KANALI GAGUTI AANZA ZIARA YA SIKU KUMI YA KUKAGUA WALIONUFAIKA NA MRADI WA TASAF BILA SIFA

Na Rhoda Ezekiel Buhigwe,

MKUU wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Marko Gaguti amesema wameanza ziara ya siku 10 ya kutembelea na kukagua nyumba kwa nyumba  ili kuwabaini watu wanaonufaika na mpango wa kuwasaidia kaya masikini TASAF  awamu ya tatu,  ambao hawana sifa na kuwaondoa katika Mpango.

Katika ziara hiyo iliyoanza jana katika Kijiji cha Munanila,Dc Gaguti alisema katika Wilaya ya Buhigwe kuna jumla ya kaya 307 zilizo andikishwa kama kaya masikini, lakini hazina vigezo vya kunufaika na mradi huu kutokana na hali zao za kiuchumi na mazingira  wanayo ishi hayaonyeshi kuwa ni masikini hivyo watatakiwa kuondolewa katika mpango huo.

Alisema Ziara hiyo itafanyika kwa siku kumi itahusisha viongozi wote wa ngazi ya Kijiji,kata na Wilaya ili kuwabaini wale wote ambao hawastahili  waondolewe na wanufaika wabaki kuwa wale wanao stahili tuu kupatiwa msaada huo wa kaya lengwa.

Gaguti alisema kuna baadhi ya wanufaika wamekimbia baada ya kupewa taarifa ya uhakiki wa wanufaika wa mradi huo  kwa kuhofia wanaweza kutolewa,kwa wale ambao hawakuwepo kwenye kaya zao ili kuhakikiwa watakuwa wamejiondoa,kwa sasa tumetoa maelekezo kwa viongozi wa vijiji kushirikiana na serikali ili kukamilisha suala hilo kwa nakini bila kumpendelea wala kumuonea mtu yeyote.

"Leo tumeanza zoezi la kuwabaini wanufaika wasio na sifa zoezi,zoezi hili litakuwa ni la siku kumi katika ziara ya leo,na tumefanikiwa kuwabaini baadhi ya wanufaika ambao hawana sifa,hivyo watatakiwa kuondolewa kwenye mradi na kwa waliokwepa kufanyiwa tathimini ya kunufaika na mradi watakuwa wamejiondoa wenyewe, tunahitaji kubaki na watu ambao wana sifa ya kupatiwa fedha za TASAF ili lengo la serikali la kuzisaidia kaya masikini litimie",alisema Gaguti.

Kwa upande wake Mratibu wa TASAF Wilaya ya Buhigwe Chubwa Deogratius alisema mkakati wa kuwaingiza wahusika ulishirikisha jamii husika pamoja na wenyeviti wa vijiji ambapo Wananchi wenyewe walikuwa wakidangsnya taarifa yupi anastahili kuingizwa kwenye mpango na yupi hastahili .

Alisema baada ya kupokea barua kutoka Wizarali sisi kama wasimamizi wa mpango huu tumeamua kupita nyumba kwa nyumba kwa walengwa ilikuweza kujilizisha yupi anastahili kuendelea kuingizwa kwenye mpango na yupi hastahili ilikuweza kukamilisha adhima ya serikali ya kuzisaidia kaya masikini.

Katika ziara ya siku ya leo kuna jumla ya kaya tatu ambazo hazina sifa. Anjelina Josia na Veronica James ni baadhi ya wanufaika walio kuwa  kwenye mpango na hawana vigezo vya kuwemo kwenye mpango huo wakati kuna baadhi wenye vigezo vya kuwa kaya masikini wameshindwa kuingizwa kwenye mpango hali ambayo inatia wasiwasi  na ziara hiyo kuendelea na uchunguzi.
 
 MKUU wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Marko Gaguti akizungumza na mmoja wa Wamufaika na mradi wa Kaya Masikini (TASAF),wakati wa ziara yake ya siku 10 ya kutembelea nyumba kwa nyumba  ili kuwabaini watu wanaonufaika na mpango wa kuwasaidia kaya masikini TASAF  awamu ya tatu,  ambao hawana sifa waondolewa katika Mpango.
 MKUU wa Wilaya ya Buhigwe Kanali Marko Gaguti akiwa sambamba naMratibu wa TASAF Wilaya ya Buhigwe Chubwa Deogratius wakiendelea na ukaguzi wa Wamufaika na mradi wa Kaya Masikini (TASAF),wakati wa ziara yake ya siku 10 ya kutembelea nyumba kwa nyumba  ili kuwabaini wale watu wanaonufaika na mpango wa kuwasaidia kaya masikini TASAF  awamu ya tatu,bila kuwa na sifa  katika Mpango.

No comments: