Tuesday, December 27, 2016

ASKARI JESHI NA WANAHABARI WALIVYOSHEREHEKEA MIAKA 55 YA UHURU KATIKA KILELE CHA UHURU ,MLIMA KILIMANJARO

Safari ya kuekea kilele cha Uhuru inaanza majira ya saa 5:00 usiku kwa kuianza safari kutoka Kibo Hut.
Safari ilikuwa ni usiku kucha 
Jua likachomoka wakati safari ikiendelea.
Kadri kulivyokucha ndivyo washiriki walivyoendelea kupata nguvu ya kuendelea na safari ya kufika Uhuru Peak.
Matumaini yakaanza kuonekana baada ya alama ya Gilmans Point kuanza kuonekana.
Mdogo mdogo ndo ilikua kauli ya kuongeza morali kwa wapandaji.
Gilmans Point hatimaye washiriki wakafika lakini hii ni hatua ya kwanza bado hatua mbili ili kufika Uhuru Peak.
Miongoni mwa waliofika Gilmans Point ni Naibu Kamanda wa kikosi cha nchi kavu cha jeshi la Ulinzi Brigedia Jenerali Jairo Mwaseba.
Safari ya kuelekea Uhuru Peak ikaendelea.
Hatimaye wapandaji wakapita kituo cha pili ambachi ni Stella na mongoni mwa waliofika hapa ni aliyekuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) Balozi Charles Sanga.
Safari ilivyoendelea kuelekea Uhuru Peak safu ya vilima vikiwa vyenye barafu ndio vilitawala eneo hilo.
Hatimaye safari ya siku sita ya Wanahabari na askari wa jeshi la Ulinzi ya kupanda Mlim Kilimanjaro kwa ajili ya kumbukumbu ya miaka 55 ya Uhuru wa Tanganyika ikafika tamati.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii 
Kanda ya Kaskazini aliyekuwepo katika safari hiyo.

No comments: