Mradi wa uboreshaji wa huduma ya majisafi katika Kijiji cha Kasapo,
Kata ya Mkuyuni, Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro.
Waziri wa Rasilimali za Maji na Umwagiliaji wa Misri, Prof. Dkt.
Mohammed Abdel Aty na Waziri wa Maji na Umwagiliaji nchini, Inj. Gerson
Lwenge, pamoja na Balozi wa Misri nchini, Yasser Ahmed Al Eldin
Elshawaf wakimsikiliza Mkurugenzi Msaidizi wa Rasilimali za Maji, Grace
Nsanya mara baada ya kuzindua mradi wa maji wa visima 30 kwa ajili ya
uboreshaji wa huduma ya majisafi kwa wilaya za Same, Mwanga, Kiteto,
Bariadi na Itilima.
Waziri wa Rasilimali za Maji na Umwagiliaji wa Misri, Prof. Dkt.
Mohammed Abdel Aty na Waziri wa Maji na Umwagiliaji nchini Inj. Gerson
Lwenge, wakifungua maji yaliyotokana na moja ya visima 8 vilichochimbwa
mkoani Kilimanjaro katika Kijiji cha Kasapo, Kata ya Mkuyuni, Wilayani
Same.
Waziri wa Rasilimali za Maji na Umwagiliaji wa Misri, Prof. Dkt.
Mohammed Abdel Aty na Waziri wa Maji na Umwagiliaji nchini, Inj. Gerson
Lwenge wakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Mecky Sadick na Mkuu
wa Wilaya ya Same, Rosemary Senyamule.
Waziri wa Rasilimali za Maji na Umwagiliaji wa Misri, Prof. Dkt.
Mohammed Abdel Aty akijaza ndoo ya maji kwa ajili ya kumtwisha mkazi
wa Kijiji cha na Waziri wa Maji na Umwagiliaji nchini, Mhandisi Gerson
Lwenge akiangalia, kuashiria uzinduzi na makabidhiano ya mradi wa maji
wa visima 30 kwa ajili ya uboreshaji wa huduma ya majisafi uliotekelezwa
kwa ushirikiano wa Serikali ya Tanzania na Misri katika wilaya kame za
Same, Mwanga, Kiteto, Bariadi na Itilima wa mradi huo wa maji.
Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Inj. Gerson Lwenge akiwa pamoja na
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji na Umwagiliaji (katikati), Inj.
Emmanuel Kalobelo na Mkurugenzi wa Rasilimali za Maji, Hamza Sadiki
katika hafla ya uzinduzi na makabidhiano ya mradi wa maji wa visima 30
kwa ajili ya uboreshaji wa huduma ya majisafi kwa wilaya za Same,
Mwanga, Kiteto, Bariadi na Itilima.
No comments:
Post a Comment