Waziri wa Mambo ya Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe |
Serikali imesema utaratibu ulioanza kujitokeza nchini wa baadhi ya asasi za kidini na wananchi kuyalipia faini makundi ya wafungwa magerezani, una hatari ya kupotosha dhamira na dhana nzima ya adhabu katika mfumo uliopo wa Haki jinai.
Waziri wa
Mambo ya Katiba na Sheria, Dk. Harrison Mwakyembe amesema hayo jijini Dar es
Salaam na kusema dhana na dhamira ya
adhabu kwa makosa ya jinai ni kumfanya aliyetenda kosa ajutie kosa lake na
wengine wenye mwelekeo kama wa kwake katika jamii, wajifunze na wajirekebishe
ili nao yasije yakawakuta.
Akijibu
maswali ya waandishi wa habari ofisini kwake kuhusu malalamiko ya Mwenyekiti wa Bodi ya
Parole, Agustino Mrema kuwa waliolipiwa faini bado mpaka leo hawajaachiwa,
Waziri huyo alimpongeza Kamishna Mkuu wa Magereza, John Minja, kwa kutotetereka
katika kusimamia sheria.
Amesema
kulipiwa faini kwa makundi na watu wasio na nasaba moja kwa moja na wafungwa,
kunaondoa kabisa lengo la adhabu la
kumfanya mkosaji ajutie kosa lake na wengine katika jamii waliokuwa na mwelekeo
huo kujirudi.
Ameongeza
kuwa pamoja na nia njema ambayo walipa faini hao wanaweza kuwa nayo, usamaria
wema huo umweza kuchochea uvunjaji zaidi wa sheria kwa imani kuwa kuna mtu
baadaye atakaye watoa kwa pesa bila wao au ndugu zao wa karibu kutoa jasho
lolote.
Hivi karibuni
Kanisa la Assemblies of God (Mlima wa Moto) Mikocheni B Dar es Salaam
liliwalipia faini wafungwa kadhaa katika magereza ya Keko, Segerea na Ukonga
Dar es Salaam na gereza la Isanga, Dodoma.
Naye Mwenyekiti
wa Bodi ya Parole, Mhe. Augustine Mrema, amesikika akiulaumu uongozi wa
Magereza nchini kwa kuendelea kuwashikilia wafungwa waliolipiwa faini na hivyo
kuongeza msongamano magerezani.
Idara ya
Magereza nayo inajitetea kuwa kuwa hata baada ya kulipiwa faini, lazima
ijiridhishe na matakwa ya sheria ya haki jinai.
No comments:
Post a Comment