Waziri wa Nchi Ofisi
ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira Mh. January Makamba amewataka
Wananchi wa Zanzibar kuulinda na
kuuheshimu Muungano pamoja na mapinduzi tukufu ya Zanzibar. Ameyasema hayo
alipokua ziarani Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Aliongeza kuwa anaipongeza Serikali ya Mkoa kwa juhudi
wanazozifanya kuhakikisha wanasimamia
usalama kwa raia wote . Akiwasilisha
taarifa kwa Mh Waziri, Katibu tawala wa Mkoa wa Kasazini Pemba Mohamed
Ali alitaja changamoto zinazowakabili ni uchakavu wa jengo la Ofisi ya Mkuu wa
Mkoa hivyo kuomba Waziri awsaidie.
Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na
Mazingira Mh. January Makamba yupo katika ziara mkoani Kaskazini Pemba pamoja
na Unguja.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiongea mara baada ya kupokea taarifa ya Mkoa wa Kaskazini Pemba alipokua ziarani Mkoani humo.
Katibu Tawala wa Mkoa wa Kaskazini Pemba Yusuf Mohamed Ali akisoma taarifa ya Mkoa wakati akiiwasilisha kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira Mh. January Makamba alipotembelea mkoa huo huko Pemba
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira Mh. January Makamba (aliyenyoosha mkono) akiwa pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Wete- Pemba Bwana Rashid Hadid Rashid wakati alipokua ziarani mkoani Kasakzini Pemba.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akikagua mazingira ya jengo ala Ikulu ndogo ya Ofisi ya Mh Makamu wa Rais lililopo Wete mkoa wa Kaskazini Pemba.
Waziri wa Nchi Ofisi
ya Makamu wa Rais - Muungano na Mazingira Mh. January Makamba akiangalia
kingo za uzio wa jengo la makazi ya Makamu wa Rais huko Wete- Pemba.
No comments:
Post a Comment