Monday, November 28, 2016

WAZAZI HALMASHAURI YA KAKONKO WAFANIKIWA KUTOA CHAKULA S/ MSINGI 59

Judith Mhina - Maelezo

Wazazi Halmashauri ya Kakonko, wafanikiwa kutoa chakula katika shule 59 zilizopo katika Halmashauri hiyo kuamzoa mwaka  2015.

Mkoa wa Kigoma una jumla ya Halmashauri 8 na kati ya hizo ni Kakonko peke yake ndio imefanikiwa kutoa huduma ya uji shuleni. Nikiongea na Waratibu kata kata 5 za Kakonko Bw Jobson Johnston, Scolastica Andrew, Paschal Mlelema, Eliud Kayigwe na Samson Sike kwa wakati mmoja wamesema hatukujua kama Halmashauri nyingine hawana huduma hiyo katika shule zao walidhani ni mpango wa Mkoa

Hata hivyo, walisema:” Changamoto walizoziainisha waratibu Kata wa Halmashauri nyingine hazina mashiko hivyo ni vema wakajithatiti kuhamasisha  wazazi nina hakika wakielewa umuhimu wa chakula shuleni , watakubali kuchangia na hatimaye watoto watapata Uji na kutoa huduma hiyo.

Watoto wa Shule ya Msingi ButaLe Maalum wakipata Chakula cha Mchana shuleni

Waliongeza kwa kusema utafiti wa Shirika la Kimataifa la Watoto UNICEF uliofanyika 2001-2003,  ulionyesha watoto waliowengi wa shule za msingi Mkoa wa Kigoma wamedumaa kwa kubeba mizigo mikubwa kuliko uwezo wao na kukosa chakula bora, wakati Mkoa unakila aina ya chakula, na kuongeza mafuta ya mawese matunda mbogamboga za majani yote yanayopatikana Tanzania yapo Kigoma, , hivyo  hakuna sababu ya msingi ya watoto kudumaa.

Mratibu Kata kiongozi wa Kakonko kwenye Warsha ya Mpango wa Kuinua Kiwango cha Elimu, Bw Jobson Johnston alisema kila mzazi anachangia kilo 5 ya mahindi, hivyo shule kupata mahindi zaidi ya mahitaji ya mwaka , ambapo huuza kiasi kwa ajili ya  kupata fedha ya kununulia maziwa, sukari na mafuta ya mawese.

Uji unaotolewa mashuleni umekuwa na virutubisho bora kabisa kumfanya mwanafunzi apate usikivu wamasomo darasani, nakuweza kufanya vizuri.Kila mwanafunzi huja shule na kikombe chake kwa ajili ya huduma ya kupata uji.

Kakonko in jumla ya kata 13 nazo ni Kiziguzigu, vijiji 3 Gwarama, vijiji 6 Kasuga, vijiji 3 Mugunzu, vijiji 4 Muhange, vijiji 4 Kitanga, vijiji 3 Kasanda, vijiji 7 Nyabibuye, vijiji 2 Gwanumpu, vijiji 4 Kakonko, vijiji 4 Kanyonza, vijiji 1 Nyamtukuzavijiji 3 na Rugenge vijiji 4 ambapo kwa ujumla kuna shule 59 za Msingi za Serikali.

Halmashauri ya Kakonko ni kati ya Halmashauri mpya zilizoanzishwa mwaka 2014, ina jumla ya shule za Msingi 59, ambazo kwa sasa zote zimeingia kwenye mpango wa kupata chakula shuleni., Aina ya chakula kinachotolewa ni  uji na Baadhi zinztoa Ugali na maharage aidha, chakula kinapata virutubisho kwa kuwekwa mafuta ya mawese na zile shule zenye kufuga ngombe wanaweka maziwa  kwenye uji hii imesaidia kwa  kiasi kikubwa kupandisha mahudhurio kwa watoto   kupenda kwenda shule.

Mkoa wa Kigoma ni kati ya mikoa yenye uzalishaji mkubwa wa chakula hapa nchini, wenye mazingira mazuri ya kupata mvua bila vikwazo. Ardhi yake ni nzuri yenye rutuba sehemu nyingi wanalima kilimo hai ,yaani bila kutumia mbolea za chumvu cnumvi, lakini kupata mavuno mengi. Hakika Mkoa huu hauna sababu kwa nini usitoe chakula katika shule za Msingi zote Mkoa mzima.

No comments: