Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya Ulinzi na Usalama ya Mtaa wa Mbagala-Kiburugwa, Bw.Kassim Mohammed Mnyoge, akizungumzia maagizo hayo |
NA
K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
WAKAZI wa Mtaa
wa Mbagala- Kiburugwa, wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, wamefanya kikao Jumapili
Novemba 20, 2016, cha kujadili maagizo ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Kamishna
Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, (SACP), Gilles Muroto kuhusu masuala ya Ulinzi
na Usalama ngazi ya Mtaa.
Akizungumza
kwenye kikao hicho, Kaimu Afisa Mtendaji wa Kata Bw.Saleh Kaitani, alisema,
kikao hicho kitajadili mambo mawili, mosi ni maagizo ya SACP Muroto na pili ni
masuala ya mpango wa kusaidia kaya masikini wa TASAF.
Kusuhusu suala
la ulinzi na usalama, Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya Ulinzi na Usalama ya Mtaa
huo, Bw.Kassim Mohammed Mnyoge alisema, SACP Muroto katika kikao chake na
watendaji kilichofanyika Oktoba 28, 2016 kwenye shule ya msingi Kigungi, alitoa
maagizo kadhaa kuhusu hatua za kuchukua katika kuhakikisha wananchi
wanashirikishwa katika suala la ulinzi na usala.
“Kila mjumbe wa
mtaa kwa kushirikiana na Mratibu, waorodheshe katika daftari wakazi wa mtaa
husika ili kujua idadi yao na shughuli wanazofanya.” Alisema Bw. Kassim wakati
akiwasilisha taarifa kwa wananchi.
Mtaa wa
Kiburugwa una wakazi wanaofikia 18,000 kwa mujibu wa Bw. Kassim.
Akifafanua zaidi
kuhusu suala hilo la Ulinzi na Usalama, Bw. Kassim alisema, SACP Muroto
ameagiza wananchi mjadili jinsi ya kushiriki katuika suala la ulinzi na usalama
kwenye mitaa.
Kila mwenye
nyumba, anapotembelewa na mgeni ni lazima akatoe taarifa kwa mjumbe wa nyumba kumi
au kwa mratibu wa eneo husika, lakini pia kila mwananchi lazima ashiriki kwenye
suala la ulizni na akikaidi Mjumbe wa mtaa apelike taarifa kwa mwenyekiti wa
serikali ya mtaa ili taarifa hiyo imfikia RPC kwa hatua za kisheria ambazo
adhabu zake ni faini ya shilingi elfu 50,000 au kifungo cha miezi sita jela au
vyote kwa pamoja.
Maagizo mengine
yaliyojadiliwa ni pamoja wazazi kuwadhibiti watoto wao, na endapo mtoto mwenye
umri chini ya miaka 18 atajihusisha na vitendo vya
kihalifu kama kujiunga na makundi ya “panya road”, basi mzazi wa mtoto huyo
atakamatwa kwa vile ni jukumu lake kuhakikisha mtoto huyo anakuwa katika
maadili mema.
Wakichangia
kwenye mjadala huo, wananchi wengi wamekubaliana na maagizo hayo ya kushiriki
kwenye ulinzi lakini wakaonyesha wasiwasi namna ya utekelezaji wake.
“Ninapenda
nijulishwe, ulinzi huu ambao wananchi tunatakiwa kushiriki ni wa namna gani, maana
hali ya sasa sio kama ile ya zamani ya enzi za Mrema, mambo ya sungusungu
kutembea na panga nataka kujua tunalindaje na usalama wetu ukoje endapo
nitadhurika.” Aliuliza mwananchi mmoja Bw.Hamisi Omary Libinongi.
Mwananchi
mwingine, alisema, ni vema wananchi wanapolinda wakaongozana na askari wenye
silaha, kwani wahalifu wa sasa, wanabeba silaha nzito nzito na kwamba itakuwa
hatari kwa mwananchi kufanya doria kwa kutumia panga pekee.
Akijibu hoja
kuhusu jinsi ya ushiriki wa wananchi katika ulinzi, Mwneyekiti wa Serikali ya
Mtaa huo, Bw.Said Mwinshehe Ng’agi, alisema, wananchi hawapaswi kuwa na
wasiwasi katika suala hilo la ulinzi, kwani kila kundi la wananchi wanaolinda
kwenye eneo fulani, wataongozana na askari wawili wenye silaha.
Naye Kaimu Afisa
Mtendaji wa Kata hiyo ya Kiburugwa, Bw.Salehe Kaitani, amesema maagizo hayo ni
ya serikali na wananchi hawana buni kushirikiana ili kuyatekeleza. “Wananchi
tunapaswa kutekeleza maagizo haya ya Jeshi la polisi, najua zipo changamoto za
baadhi ya askari kutokuwa waaminifu, lakini kama mjuavyo askari wa namna hii
ambao hawana wito, wamekuwa wakichukuliwa hatua na nyinyi wananchi toeni
taarifa kwa viongozi kama mnakutana na askari wanaodai rushwa.” Alisema Bw.
Laitani.
Mwananchi akiuliza swali kuhusu utaratibu wa kiulinzi kwa kushirikiana na wajumbe wa mtaa.
Mwananchi akiuliza nini umuhimu wa vijana wa ulinzi shirikishi kwenye mitaa
Mzee Hamisi Omary Libinongi, akkuliza namna wananchi watakavyotekeleza ulinzi huo bila ya kupatwa na madhara
Kaimu Afisa Mtendaji wa Kata ya Kiburugwa, Bw.Salehe Kaitani, akifafanua baadhi ya maswali yaliyoulizwa na wananchi
Mjumbe wa nyumba kumi, Bw. Jumanne Mohammed Ngayeka almaarufu kama "Nongwa" aliuliza swali
Kaimu Afisa Mtendaji wa Kata ya Kiburugwa, Bw.Salehe Kaitani,akihutubia wananchi
Wananchi wakifuatilia kwa makini kwenye mkutano huo
Mwenyekiti mstaafu wa serikali ya mtaa wa Mbagala-Kiburugwa, Mzee Adiswele, maarufu kama "Pepe Kale" akizungumzia uzoefu wake katika swala la ulinzi shirikishi
Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mbagala-Kiburugwa,
wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati
ya Ulinzi na Usalama ya Mtaa huo, Bw.Said Mwinshehe Mng'agi, (kulia) akizungumza na wananchi
Baadhi ya wananchi waliohudhuria
Baadhi ya wananchi waliohudhuria
No comments:
Post a Comment