Tuesday, November 22, 2016

WAKALA ZA SERIKALI ZATAKIWA KUBADILISHANA UZOEFU KIUTENDAJI ILI KUBORESHA HUDUMA


 Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi wa Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mick Kiliba akiongoza mjadala katika kikao cha Mrejesho wa Ufuatiliaji na Utekelezaji wa Mifumo na Viwango vya Utendaji kazi kwa Wakala za Serikali kilichofanyika katika ukumbi wa Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) leo.
 Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Mifumo na Viwango vya Utendaji Kazi kutoka Ofisi ya Rais - Utumishi, Bi. Veila Shoo akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa Mifumo na Viwango vya Utendaji Kazi kwa Wajumbe kutoka katika Wakala mbalimbali za Serikali katika ukumbi wa Wakala za Serikali katika kikao kilichofanyika ukumbi wa Wakala kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) leo. Katikati ni Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi wa Ofisi ya Rais-Utumishi, Bw. Mick Kiliba na kushoto ni Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA), Bw. Dominic Rwekaza.
 Baadhi ya washiriki kutoka Wakala Mbalimbali za Serikali wakifuatilia mada katika kikao chaMrejesho wa Ufuatiliaji na Utekelezaji wa Mifumo na Viwango vya Utendaji kazi kwa Wakala za Serikali kilichofanyika katika ukumbi wa Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) leo.
Kaimu Mtendaji Mkuu wa chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) Dkt. Henry Mambo akichangia mada kuhusu taarifa ya utekelezaji wa Mifumo na Viwango vya Utendaji Kazi kwa Wakala mbalimbali za Serikali katika ukumbi wa Wakala za Serikali katika kikao kilichofanyika ukumbi wa Wakala kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) leo.


Serikali imezitaka wakala zake kuwa na utaratibu wa kubadilishana uzoefu juu ya Mifumo na Viwango ya Utendaji Kazi  ili kuboresha utoaji huduma kwa umma.

Hayo yalisemwa leo na Mkurugenzi wa Idara ya Uchambuzi na Ushauri wa Kazi wa Ofisi ya Rais-Utumishi, Bwana Mick Kiliba alipokuwa akifungua kikao kazi cha Mrejesho wa Ufuatiliaji na Utekelezaji wa Mifumo na Viwango vya Utendaji kazi vya Wakala za Serikali kwa niaba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais-Utumishi, kilichofanyika katika ukumbi wa Wakala ya Mafunzo kwa Njia ya Mtandao (TaGLA) leo.

Bwana Kiliba alisema kuwa, Serikali imekuwa ikifanya maboresho katika nyanja mbalimbali ikiwemo sekta ya Umma na kwamba moja ya mkakati wa kuboresha Utumishi wa Umma ni pamoja na kuimarisha Mifumo na Viwango vya Utendaji Kazi.

“Mifumo na Viwango vya Utendaji Kazi ndio msingi na nyenzo muhimu ya uwajibikaji na uboreshaji wa utoaji wa huduma katika Taasisi za Umma zikiwemo Wakala za Serikali,” Bwana Kiliba alisisitiza.

Alibainisha kuwa, matumizi ya Mifumo na Viwango vya utendaji kazi katika Wakala za Serikali ni jambo muhimu katika kufikia matarajio na malengo ya kuanzishwa kwake.

Aidha, alifafanua kuwa, zoezi la kufuatilia utekelezaji wa Mifumo na Viwango vya utendaji kazi lilifanyika mwezi Mei, 2016 na lilijikita katika kubaini hali halisi ya utekelezaji wa Mifumo na Viwango vya utendaji kazi katika Wakala za Serikali 18. 

No comments: