Wednesday, November 2, 2016

WADAU WA UJENZI WAKAGUA UWANJA WA KIMATAIFA WA MWL. JULIUS NYERERE (TB III)

Mwenyekiti wa Ujumbe maalum wa wadau wa Ujenzi, Bi. Elizabeth Tagora (wa kwanza kulia), akijadiliana jambo na Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Nchini (TANROADS), Eng. Patrick Mfugale (wa kwanza kushoto), wakati ujumbe huo ulipokagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo la tatu la Abiria (Terminal III) katika Uwanja wa Ndege wa kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere (JNIA). 
Mkurugenzi wa Mradi wa ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria (TB III), Eng. Mohamedi Milanga akifafanua jambo kwa ujumbe maalum wa wadau wa ujenzi walipokagua hatua za ujenzi wa jengo hilo. 
Mkurugenzi wa Mradi wa ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria (TB III), Eng. Mohamedi Milanga akionesha wajumbe maalum wa wadau wa ujenzi eneo la kupumzikia abiria katika Jengo la Tatu la Abiria (TB III) waliokagua hatua za ujenzi wa jengo hilo. 
Muendelezo wa jengo la tatu la abiria sehemu ya pili katika hatua za ujenzi. Jengo hilo litakapokamilika litakuwa na uwezo wa kuhudumia abiria 2,800 kwa wakati mmoja. 
Muonekano wa eneo zitakapokuwepo huduma za kibenki na Idara ya Uhamiaji katika Jengo la tatu la Abiria (TB III). 
Muonekano wa sehemu ya mbele ya wa Jengo la Tatu la Abiria (TB III) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere (JNIA). Jengo hilo linatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwaka ujao. 
Muonekano wa juu wa Jengo la Tatu la Abiria (TB III) katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwl. Julius Nyerere (JNIA).

No comments: