Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome akitoa
neno la ukaribisho kwa ujumbe kutoka nchi za Nordic ulipotembelea wizara
wake jana 14/11/2016 jijini Dar Es Salaam.(Picha na Zainul Mzige
wa Modewjiblog)
Serikali
ya Tanzania imeshukuru msaada mkubwa unaotolewa na Mashirika ya Umoja
wa Mataifa katika kuhakikisha kwamba taifa linakuwa na mfumo imara wa
utoaji haki kwa kuzingatia demokrasia na uwajibikaji.
Serikali
imesema kumekuwepo na mabadiliko makubwa katika mfumo ya utoaji haki
nchini kutokana na misaada iliyotolewa na nchi hizo kupitia Mashirika ya
Umoja wa Mataifa ambao unasaidia mpango huo wa UNDAP.
Hayo
yameelezwa wakati ujumbe mzito wa kutoka nchi za Nordic ulipotembelea
Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria. Nchi hizo za Nordic pamoja kutoa
mchango wake mkubwa katika bajeti za serikali ya Tanzania pia hutoa
mchango mkubwa kwa mashirika ya Umoja wa Mataifa yanayofanya shughuli
zake nchini.
Mataifa
hayo ni ya Sweden, Norway, Denmark, Finland na Iceland ambayo kwa
pamoja yanaitwa mataifa ya Nordic ni wadau muhimu wa Umoja wa Mataifa na
pia kwa serikali ya Tanzania.
Ujumbe
kutoka nchi hizo upo nchini kwa ajili ya kuimarisha mahusiano kati yao
na Mashrika ya Umoja wa Mataifa yanayofanyakazi kama taasisi moja na
nchi hizo (Delivering as one) kwa lengo la kuimarisha na kusukuma mbele
malengo ya maendeleo endelevu (SDGs).
Katika
ziara hiyo iliyoanzia Novemba 14 wajumbe hao waliweza kuangalia
utekelezaji mbalimbali wa miradi ya Umoja wa Mataifa na hasa hatua za
mwanzo za miradi ya UNDAP ll.
Ujumbe
huo wenye watu 13 kutoka Wizara za Mambo ya Nje za mataifa hayo
wanatarajia kuzuru pia Kigoma na Dodoma wakimaliza Dar es Salaam.
Wakiwa
Dar es Salaam, jana na leo watakutana na wawakilishi wa taasisi
mbalimbali zisizo za kiserikali na AZAKI na pia wanatarajia kutembelea
ofisi za Bunge.Taarifa iliyotolewa katika mkutano huo imesema ingawa
msaada wa Umoja wa Mataifa umekuwa siku zote ukililenga eneo maalumu
linaloshughulikiwa na mashirika tofauti ya Umoja wa Mataifa, imekuwa
nguvu kupima athari zake katika maeneo mbalimbali yaliyokusudiwa.
Mkurugenzi
Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Awa
Dabo akielezea dhumuni la ziara ya ujumbe kutoka nchi za Nordic
ulioambatana na wataalam kutoka Umoja wa Mataifa ulipotembelea wizara
hiyo jana 14/11/2016 jijini Dar Es Salaam.
Hata
hivyo imeelezwa kuwa kupitia programu mbalimbali na miradi katika
demokrasia na uwajibikaji kuwezesha utawala bora, kumefanya kuwepo na
nafuu fulani.
Serikali
ya Tanzania ilielezea matumaini yake kwamba UNDAP ll, Mashirika ya
Umoja wa Mataifa yakifanya kazi kama taasisi moja yatasaidia wizara
katika kufanikisha kwa namna sahihi mfumo wa haki kwa wananchi.
Programu
hizo ni pamoja na UNDAP 1 iliyosaidia wizara kutengeneza na kutekeleza
mpango wa haki za binadamu (MHRAP 2013-2017). Mpango huo ulibainisha
maeneo mbalimbali yaliyotakiwa kufanyiwa kazi na wadau mbalimbali.
UNDAP
I ilisaidia wizara kupitia Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa serikali
kujenga uwezo kwa wafanyakazi wake katika masuala ya majadiliano katika
mikataba na namna ya kuiandika hasa katika sekta ya uziduaji.
Mkurugenzi
Idara ya Katiba na Ufuatiliaji Haki Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria
Bw. Patience Ntwina (aliyesimama) akitoa taarifa ya utekelezaji wa
miradi mbalimbali inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa kwa ujumbe kutoka
nchi za Nordic ulioambatana na wataalam kutoka Umoja wa Mataifa
ulipotembelea wizara hiyo jana 14/11/2016 jijini Dar Es Salaam.
Wanasheria kadha wa serikali na majaji walinufaika na elimu hiyo.
Aidha
chini ya UNDAP I, Umoja wa Mataifa ulitoa msaada wa kiufundi kwa wizara
kwa lengo la kuwezesha kufanya utafiti kuhusu hali ya mfumo wa haki wa
mtoto nchini Tanzania na kuweza mkakati endelevu wa haki za mtoto
kuanzia wmaka 2013-2017.
Wizara pia inasaidiwa kufuatilia mkakati huo kupitia majukwaa ya haki za watoto yanayofanyika kila mwaka.
Wizara
ya Mambo ya Katiba na Sheria kwa mujibu wa sera ndiyo iliyokabidhiwa
majukumu ya kutengeneza kanuni na viwango, kuratibu na kufuatilia utii
usio na shuruti katika mfumo wa sheria na hivyo kupata matokeo
yaliyokusudiwa ya sheria husika.
Wizara
hii inajishughulisha na masuala ya Katiba, utawala na utoaji wa haki;
uandishi wa sheria; uendeshaji wa mashtaka; Mikataba na sheria za
kimataifa: msaada wa kisheria na haki za binadamu;usajili uboreshaji wa
sheria, kabidhi wasihi, udhamini na mufilisi na kadhalika
Naibu
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Bw. Gerson Mdemu akizungumzia ufadhili wa
Umoja wa Mataifa kwa ofisi yake wakati wa mkutano na ujumbe kutoka nchi
za Nordic ulioambatana na wataalam kutoka Umoja wa Mataifa uliofanyika
katika Wizara ya Mambo ya Sheria na Katiba jana 14/11/2016 jijini Dar Es
Salaam.
Mamlaka ya Wizara katika mambo mengi ni mtambuka na hivyo kuifanya kuwa na ugumu fulani katika utendaji wake.
Aidha
akifafanua zaidi amesema kutokana na misaada ya mashirika ya Umoja wa
Mataifa, Watanzania wameweza kuwa na mfumo bora zaidi wa haki kwa watoto
wanaoingia matatani na sheria.
Aidha
watoto zaidi ya 1,500 wamepatiwa msaada wa kisheria katika mji wa Mbeya
na Dar es Salaam na yote hayo yamewezeshwa na UNDAP l.
Wizara
pia iliangalia matatizo ya ukatili wa kijinsia na watoto katika Dar es
Salaam, Dodoma na Kilimanjaro na matokeo yake kusambazwa kwa wadau
mbalimbali kwa kuyafanyia kazi.
Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Afisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa
Umma na Utawala Bora Zanzibar Bw. Kubingwa Mashaka Simba akitoa taarifa
ya utekelezwaji wa miradi inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa kwa ujumbe
wa wataalam wa Umoja huo waliotembelea Wizara ya Mambo ya Katiba na
Sheria Tanzania Bara jana 14/11/2016 jijini Dar Es Salaam.
Aidha
kwa kusaidiwa na Umoja wa Mataifa ambayo iliratibu mkutano wa kwanza wa
wadau kuzungumzia sheria ya ndoa ya mwaka 1971 katika hali ya kuongeza
haki zaidi ka wanawake na watoto.
Pia
alisema katika UNDAPll mashirika hayo ya Umoja wa Mataifa yanasaidia
pia kuangalia mfumo wa haki wa sasa hasa kwa makundi yenye uhitaji
yaliyosahaulika na kukuza ulinzi na usalama kwa mama na mtoto.
Ujumbe
huo pamoja na kuwa mzito pia utafanya safari ya kuangalia miradi ya
Bunge iliyopewa chapuo na fedha za Umoja wa Mataifa pia watatembelea
eneo la dawati la Jinsia Chang'ombe na kutembelea taasisi ya PASADA.
Maeneo mengine ni ghala la Chakula Kizota, miradi ya TASAF na pia kiwanda cha kusindika mafuta kilichopo Dodoma.
Kiongozi
wa ujumbe kutoka nchi za Nordic ulioambatana na wataalam kutoka
Mashirika ya Umoja wa Mataifa, Anders Ronquist kutoka Shirika la
Kimataifa la Maendeleo la Sweden (SIDA) akizungumza jambo kwa niaba ya
ujumbe huo ulipotembelea wizara hiyo jana 14/11/2016 jijini Dar Es
Salaam.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la
Maendeleo (UNDP), Alvaro Rodriguez akitoa neno la shukrani kwa Katibu
Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome
(kushoto) wakati wa ziara ya ujumbe kutoka nchi za Nordic ulioambatana
na wataalam kutoka Mashirika ya Umoja wa Mataifa ulipotembelea wizara
hiyo.
Sehemu
ya ujumbe kutoka nchi za Nordic ulioambatana na wataalam kutoka
Mashirika ya Umoja wa Mataifa ulipotembelea Wizara ya Mambo ya Katiba na
Sheria jana 14/11/2016 jijini Dar Es Salaam.
Balozi
wa Sweden nchini Mhe. Katarina Rangnitt akizungumza jambo wakati
akiagana na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Prof.
Sifuni Mchome (kushoto). Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja
wa Mataifa na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo (UNDP), Alvaro
Rodriguez akiteta jambo na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na
Sheria, Amon Mpanju mara baada ya kumalizika kwa mkutano na ujumbe wa
Nordic uliotembelea wizara hiyo jana.
Deepika
Nath wa UN Women akimwonyesha kitu Edgar Kiliba (kushoto) wa Ofisi ya
Mkuu wa Umoja wa Mataifa kitengo cha mawasiliano mara ya kumalizika kwa
mkutano wa ujumbe kutoka nchi za Nordic ulioambatana na wataalam kutoka
Mashirika ya Umoja wa Mataifa ulipotembelea Wizara ya Mabo ya Katiba na
Sheria jana 14/11/2016 jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment