Friday, November 18, 2016

UFUNDI WA VETA WAHITAJIKA KATIKA UCHUMI WA VIWANDA –SABUNI

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa VETA , Geoffrey Sabuni akizungumza katika mahafali ya 46 katika Chuo cha VETA, Chang’ombe  leo jijini Dar es Salaam.
 Mkuu wa Chuo cha VETA, Chang’ombe, Douglas Kipokola  akitoa maelezo katika mahafali ya 46 ya chuo hicho leo jijni Dar es Salaam.
 Wahitimu wakiimba shairi kwa mgeni rasmi (hayupo pichani) katika Mahafali ya 46 ya Chuo cha VETA, Chang’ombe leo jijini Dar es Salaam.
 Sehemu ya wahitimu wakati wa Mahafali ya 46 ya Chuo cha VETA, Chang’ombe leo jijini Dar es Salaam.
 Sehemu ya wazazi  katika Mahafali ya 46 ya Chuo cha VETA, Chang’ombe leo jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuu VETA , Geoffrey Sabuni akitoa cheti kwa mmoja wa wahitimu katika Mahafali ya 46 ya Chuo cha VETA, Chang’ombe leo jijini Dar es Salaam


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.

NCHI inakwenda katika uchumi wa viwanda ambavyo vinahitaji wataalam  mbalimbali  katika kuweza kufikia  uchumi huo kwa kuhitaji wataalam wanaozalishwa nchini wakiwemo wahitimu wa mafunzo stadi yanayotolewa  na vyuo vya VETA.

Hayo ameyasema leo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mafunzo na Ufundi Stadi (VETA), Geoffrey Sabuni wakati wa mahafali ya 46 katika Chuo cha VETA,  Changombe Dar es Salaam, amesema VETA inazalisha wataalam ambao wamebobea kwa ujuzi.

Amesema wahitimu wa VETA hawatafuti ajira kutokana na kuwa ujuzi wanaoupata  unawawezesha  kujiajiri au kuajiriwa kwa kutafutwa na wamekuwa wakifanya vizuri katika maeneo walioajiriwa na kujiajiri.

Sabuni amesema wanaosoma VETA  wapo waliohitimu kidato nne hadi  waliopata shahada ya kwanza hivyo jamii iondoe dhana  ya kwamba wanaosoma VETA ni wale walioshindwa kufanya vizuri katika shule za sekondari na msingi.

Aidha amewataka wahitimu wanaozalishwa na vyuo hivyo kuwa na  weledi  katika kufanya kazi na kuondokana kuwaibia waajiri hali ambayo itafanya baadhi yao kupoteza sifa ya kujiajiri au kuajiliwa.

Nae Mkuu wa Chuo cha  VETA Changombe, Douglas Kipokola amesema kuwa wahitimu mwaka huu  wako 423 katika fani mbalimbali na kwamba wapo tayari katika soko la ajira kutokana na mafunzo walioyapata.

Amesema kuna changamoto za  walimu ambapo wameshaanza kulifanyia kazi kutokana na mitaala inahitaji mafunzo yenye tija  kwa uwiano wa mwalimu mmoja  kwa wanafunzi wasiozidi 20.

No comments: