Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania TTCL, Bw. Waziri
W. Kindamba (kushoto) akiwaelezea wananchi mitaani juu ya ofa mpya ya
huduma ya Simu za Mezani katika eneo la Posta Mpya leo jijini Dar es
Salaam, pembezoni mwa mtaa wa Azikiwe
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania TTCL, Bw. Waziri
W. Kindamba (wa kwanza kushoto) pamoja na baadhi ya wakuu wa Idara na
Vitengo na Wafanyakazi wa TTCL wakizunguka baadhi ya mitaani wakielezea
hudumba mbalimbali za kampuni hiyo kwa wakazi wa Jiji la Dar Es Salaam
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania TTCL, Bw. Waziri
W. Kindamba (kushoto) akiwaelezea wananchi mitaani juu ya ofa mpya ya
huduma ya Simu za Mezani katika eneo la Posta Mpya leo jijini Dar es
Salaam, pembezoni mwa mtaa wa Azikiwe.
KAMPUNI ya Simu Tanzania TTCL, leo imeanza Kampeni ya kuwafuata wateja
wake mitaani ili kuzungumza nao, kuwapa taarifa za huduma zinazotolewa
na kuwaunganisha wateja hao katika huduma mbali mbali za TTCL. Kampeni
hiyo imeongozwa na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL Bw Waziri W.
Kindamba na kusaidiwa na Wakuu wa Idara na Vitengo pamoja na Wafanyakazi
wa TTCL waliosambaa katika maeneo mbali mbali ya Jiji la Dar Es Salaam.
"Huu utakuwa ni utamaduni wetu, tutawafuata Wateja popote walipo,
tutawapa taarifa za huduma zetu bora na nafuu, tutawasikiliza na
kufanyia kazi maoni yao.
Tunataka
kuwahakikishia Wananchi kuwa, hii ni TTCL Mpya, Shirika lao la
kizalendo limerejea katika nafasi ya mhimili mkuu wa Mawasiliano nchini
Tanzania. Watumie huduma zetu, waone tofauti, wapate ubora na viwango
vya juu kabisa", amesema Bw Kindamba.
Kwa upande wake Afisa Mkuu wa Masoko na Mauzo wa TTCL Bw Peter Ngota
amesema, TTCL inawaletea wateja wake Ofa MPYA kabambe kwa ajili ya Simu
ya Mezani inayotoa uhakika wa mawasiliano kati ya Wanafamilia. Kwa Mteja
atakayeongeza salio la shilingi 23,000/- atapata ofa ya Simu Bure
pamoja na ofa kupiga simu TTCL kwenda TTCL bure.
Afisa Mkuu Masoko na Mauzo wa TTCL, Bw Peter Ngota akigawa vipeperushi
vyenye ofa mpya ya huduma ya Simu za Mezani katika eneo la Palm Beach,
barabara ya Ally Hassan Mwinyi
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania TTCL, Bw. Waziri
W. Kindamba (wa pili kushoto) pamoja na baadhi ya wakuu wa Idara na
Vitengo na Wafanyakazi wa TTCL wakizunguka baadhi ya mitaani wakielezea
hudumba mbalimbali za kampuni hiyo kwa wakazi wa Jiji la Dar Es Salaam
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania TTCL, Bw. Waziri
W. Kindamba akigawa vipeperushi kwa mmoja wa wananchi vinavyoelezea ofa
mpya ya huduma ya Simu za Mezani katika eneo la Posta Mpya leo jijini
Dar es Salaam, pembezoni mwa mtaa wa Azikiwe.
Afisa wa Huduma kwa Wateja TTCL, Josephine Nsunaluga, akigawa
vipeperushi vyenye ofa mpya ya huduma ya Simu za Mezani katika eneo la
Kijitonyama, barabara ya Ally Hassan Mwinyi.
Afisa wa Huduma kwa Wateja TTCL, Blandina Mnyaga akigawa vipeperushi
vyenye ofa mpya ya huduma ya Simu za Mezani katika eneo la Moroco,
barabara ya Ally Hassan Mwinyi.
Meneja Msaidizi (Support) TTCL Dar es salaam - Kaskazini Bw Michael
Nchimbi akigawa vipeperushi vyenye ofa mpya ya huduma ya Simu za Mezani
katika eneo la Morocco, barabara ya Ally Hassan Mwinyi.
Afisa wa TTCL, Bw Aloyce Julius akigawa vipeperushi vyenye ofa mpya ya
huduma ya Simu za Mezani katika eneo la Palm Beach, barabara ya Ally
Hassan Mwinyi.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania TTCL, Bw. Waziri
W. Kindamba (katikati) pamoja na baadhi ya wakuu wa Idara na Vitengo na
Wafanyakazi wa TTCL wakizunguka baadhi ya mitaani wakielezea hudumba
mbalimbali za kampuni hiyo kwa wakazi wa Jiji la Dar Es Salaam.
Hapa baadhi ya wafanyakazi pamoja na Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa
Kampuni ya Simu Tanzania TTCL, Bw. Kindamba na baadhi ya wakuu wa Idara
na Vitengo wakionesha alama ya T mara baada ya kampeni yao.
No comments:
Post a Comment