Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Wazir
W. Kindamba (kulia) akimkabidhi kibao cha kuashiria huduma bure ya
intaneti ya teknolojia ya Wi-Fi kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo
ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa Mohamed Janabi (kushoto) leo jijini
Dar es Salaam katika hafla ya Kampuni ya TTCL kukabidhi huduma hiyo.
Huduma hiyo ina itakayotolewa kwa mwaka mmoja inagharimu shilingi
milioni 120.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa
Mohamed Janabi akizungumza katika hafla ya Kampuni ya TTCL kukabidhi
huduma ya bure ya intaneti ya teknolojia ya Wi-Fi kwa Taasisi ya Moyo ya
Jakaya Kikwete. Huduma hiyo itakayotolewa kwa mwaka mmoja inagharimu
shilingi milioni 120.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Wazir
W. Kindamba (kulia) akizungumza katika hafla ya kampuni ya TTCL
kukabidhi huduma bure ya intaneti ya teknolojia ya Wi-Fi kwa Taasisi ya
Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa
Mohamed Janabi akifuatilia.
KAMPUNI ya Simu Tanzania (TTCL) leo imefunga huduma za mawasiliano ya
intaneti bure katika Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)
itakayowawezesha madaktari, wafanyakazi wengine, wagonjwa pamoja na
wananchi wanaofika katika kituo hicho kupata huduma ya mawasiliano ya
intaneti bure yenye kasi ya hali ya juu.
Akikabidhi
huduma hiyo, Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania
(TTCL), Bw. Wazir W. Kindamba alisema kampuni hiyo imetumia jumla ya
shilingi milioni 120 kufunga huduma bure ya intaneti katika kituo hicho
na itatolewa kwa muda wa mwaka mmoja ikiwa ni kuiwezesha taasisi hiyo
kuendesha shughuli zake kwa ufanisi.
Akifafanua
zaidi Bw. Kindamba alisema huduma hiyo ambayo itagharimu shilingi
milioni 10 kwa kila mwezi ambazo zitakuwa zikilipwa na TTCL ikiwa ni
mchango wake kwa jamii na hasa kwa matibabu yanayofanyika katika kituo
hicho itakuwa ikitolewa kwa teknolojia ya Wi-Fi bure kwa kipindi cha
mwaka mmoja kuanzia Novemba 10, 2016 hadi Novemba 10, 2017.
"Kwa
kuzingatia umuhimu wa sekta ya afya na kazi kubwa inayofanywa na
Taasisi hii, TTCL tumetoa intaneti yenye kasi hadi kufikia spidi ya
100Mbps, spidi hii itasaidia kuongeza uwajibikaji katika kutoa huduma
kwa wananchi, kuimarisha mawasiliano miongoni watumishi wa JKCI na nje
ya Taasisi, kupashana habari za kitabibu na kubadilishana taarifa za
kitabibu miongoni mwa wataalamu kutoka hospitali za ndani na hospital za
nje ya mipaka ya Tanzania," alisema Kindamba.
Alisema
mbali na huduma hiyo TTCL imekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha
mawasiliano ya uhakika yanatumika katika sekta ya afya ili kuboresha
utoaji wa huduma kwa wananchi na tayari imefanikiwa kuunganisha
hospitali za rufaa za Mkoa wa Dar es salaam kupitia Mkongo wa TTCL ambao
umeunganishwa kwenye Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano.
Aidha
alizitaja hospitali nyingine zinazonufaika na huduma ya mawasiliano
hayo ni pamoja na Hospitali ya Rufaa ya Muhimbili, Hospital ya Amana,
Hospitali ya Mwananyamala, Hospitali ya Temeke, Hospitali ya Bagamoyo,
Hospitali ya Rufaa ya KCMC iliyopo Mkoa wa Kilimanjaro na Hospitali ya
Rufaa ya Bugando iliyopo mkoani Mwanza.
Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), Profesa
Mohamed Janabi akizungumza katika hafla ya Kampuni ya TTCL kukabidhi
huduma ya bure ya intaneti ya teknolojia ya Wi-Fi kwa Taasisi ya Moyo ya
Jakaya Kikwete. Huduma hiyo itakayotolewa kwa mwaka mmoja inagharimu
shilingi milioni 120.
Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL), Bw. Wazir
W. Kindamba akizungumza katika hafla ya kampuni ya TTCL kukabidhi
huduma bure ya intaneti ya teknolojia ya Wi-Fi kwa Taasisi ya Moyo ya
Jakaya Kikwete (JKCI) leo jijini Dar es Salaam. Huduma hiyo ina
itakayotolewa kwa mwaka mmoja inagharimu shilingi milioni 120.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete
(JKCI), Profesa Mohamed Janabi akitoa shukrani zake mara baada ya
kukabidhiwa huduma hiyo alisema TTCL inapaswa kutambua imetoa mchango
mkubwa wa kuokoa maisha ya wagonjwa mbalimbali wanaopatiwa huduma katika
taasisi hiyo.
Alisema
kwa maendeleo ya sasa huduma za kitabibu zinatolewa kwa njia ya
intaneti kwa wataalamu wa kituo kimoja kufanya mawasiliano na kituo
kingine jambo ambalo limekuwa msaada mkubwa katika kutoa huduma hizo kwa
wagonjwa na hata kukabiliana na changamoto ya baadhi ya wataalamu wa
afya na vifaa vya matibabu.
Alisema
kwa JKCI huduma za intaneti sio kwa ajili ya starehe bali ni muhimu
zaidi kusaidia madaktari katika kutekeleza majukumu yao, jambo ambalo
kwa sasa watakuwa wakilipata muda wote wawapo eneo la kazi.
Profesa Janabi aliongeza kuwa kiasi cha shilingi milioni 120 ambazo
kituo cha JKCI ilipaswa kukilipa kwa gharama ya huduma hiyo sasa
watakielekeza kwa wagonjwa zaidi ya 20 watakaofanyiwa upasuaji kwa fedha
hizo ikiwa ni kutambua mchango wa TTCL katika kusaidia huduma za afya
kwa jamii.
"Ndugu
Mkurugenzi kwa msaada wenu huu tambueni kuwa mmeokoa maisha ya wagonjwa
takribani ishirini ambao hawana uwezo kulipia gharama za matibabu na
sasa JKCI itawafanyia huduma za upasuaji kwa gharama mlizozitoa kwetu
kutokana na mchango wenu kwa jamii...tutajitahidi kuwapa taarifa juu ya
wagonjwa hao na idadi yake. Picha ya pamoja mara baada ya zoezi la makabiadhiano.
No comments:
Post a Comment