Tuesday, November 8, 2016

TIMU TATU ZA TAIFA ZA MPIRA WA MIGUU KUONDOKA NCHINI


TIMU ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania ‘Twiga Stars’ inakwea pipa jioni ya leo kuelekea Yaoundé, Cameroon kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa huku Vijana wa timu ya Taifa ya Serengeti Boys wakitarajiwa kuondoka kesho Novemba 9, 2016 kwenda Korea Kusini, kupitia Dubai, Falme za Kiarabu.

Twiga Stars imeondoka na nyota 17 na viongozi sita, kikosi hicho kinaundwa na wachezaji wa timu ya taifa ya Wanawake ya Tanzania Bara yaani Kilimanjaro Queens na ina rekodi nzuri ya kuwa kinara wa viwango vya ubora kwa nchi za Afrika Mashariki na kati lakini zaidi ni mabinga wapya wa ukanda huo – ubingwa uliopatikana Septemba, mwaka huu huko Uganda.

Rekodi hizo zimesukuma Shirikisho la Mpira wa Miguu la Cameroon (FECAFOOT) – nyumbani kwa Rais wa CAF, Issa Hayatou kuikubali Twiga Stars na hivyo kuomba kucheza nayo mwishoni mwa wiki hii. Tayari Twiga Stars imeanza maandalizi ya kutosha chini ya Makocha Sebastian Nkoma na Wasaidizi wake Edna Lema na El Uterry Mohrery.

Kikosi cha Twiga Stars wamo makipa, Fatma Omari na Najiat Abbas; mabeki ni Wema Richard, Sophia Mwasikili, Anastasia Katunzi, Maimuna Hamisi, Fatuma Issa, Happiness Mwaipaja na Mary Masatu wakati viungo ni Donisia Minja, Stumai Abdallah, Amina Ally, Anna Mwaisura na Fadila Kigarawa ilhali washambuliaji ni Fatuma Swalehe, Asha Rashid na Mwanahamisi Omari.

SERENGETI BOYS
Vijana wa Serengeti Boys wamaoondoka kuelekea nchini Korea Kusini kwa ajili ya mashindano yaliyoaandaliwa na nchi hiyo.
Vijana wanaosafiri kesho ni kipa Ramadhani Kabwili, Kelvin Kayego na Samwel Brazio; mabeki ni Shomari Ally, Israel Mwenda, Nickson Kibabage, Dickson Job, Ally Msengi na Enrick Vitalis wakati viungo ni Ally Ng’anzi, Shaban Ada, Asad Juma, Issa Makamba huku washambuliaji wakiwa ni Muhsin Makame, Ramadhani Gadaffi, Rashid Chombo, Cyprin Mtesigwa na Mohammed Abdallah

TAIFA STARS KUONDOKA IJUMAA
Kwa upande wa Taifa Stars, kikosi cha Kocha Mkuu wa Timu ya Mpira wa Miguu ya Tanzania, Charles Boniface Mkwasa kinatarajiwa kuondoka Ijumaa Novemba 11, mwaka huu kikiwa na nyota 20 kati ya 24 waliotangazwa wiki iliyopita. Stars inakwenda Harare, Zimbabwe kucheza na wenyeji kwenye mchezo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika Novemba 13, mwaka huu.
Mchezo huo wa kirafiki wa kimataifa utakaofanyika jijini Harare, umeratibiwa kwa mujibu wa kalenda ya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) ambalo huwa na kalenda ya wiki ya mechi za kimataifa kwa wanachama wake – Tanzania ni miongoni mwao. Shirikisho la Mpira wa Miguu la Zimbamwe liliomba TFF mchezo huo, nasi mara moja tukakubali.

Hii ni faida kwa Tanzania kama itashinda mchezo huo kwa maana kuna alama za nyongeza kama inatokea unaifunga timu mwenyeji.

Matokeo ya mchezo huo, ni sehemu malumu kupima viwango vya ubora na uwezo wa timu za taifa. Kwa sasa Tanzania inashika nafasi ya 144 kati ya nchi 205 wanachama wa FIFA zilizopimwa ubora. Zimbambwe yenyewe inashika nafasi ya 110.
Argentina inaongoza ikifuatiwa na Ubelgiji anakocheza Mbwana Samatta – nyota wa kimataifa wa Tanzania. Samatta anacheza klabu ya K.R.C Genk inayoshiriki Ligi Kuu ya Ubelgiji. Timu nyingine bora kimataifa ni Chile, Colombia na Ujerumani.
Katika Bara la Afrika, Ivory Coast ambayo ni ya 31 kwa ubora duniani ndiyo inayoongoza ikifuatiwa na Senegal (32), Algeria (35), Tunisia (38) na Ghana (45).

No comments: