Monday, November 21, 2016

SIMUTV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI


SIMU.TV: Waziri wa Elimu Prof Joyce Ndalichako, amesema serikali haitosita kuvifungia vyuo vya elimu ya juu ambavyo kimsingi havina sifa wala ubora; https://youtu.be/yT_d5lRd_mQ  

SIMU.TV: Rais Dr John Magufuli amefanya mazungumzo na kiongozi wa kijeshi kutoka nchini China na kuahidi kuongeza ushirikiano baina ya China na Tanzania; https://youtu.be/FS7-6JHMVDw  

SIMU.TV: Vikosi vya ulinzi na usalama kwa nchi za jumuiya ya Afrika mashariki zimejipanga kushirikiana pamoja ili kuhakikisha usalama unaimarika katika jumuiya hiyo; https://youtu.be/eUNf9WLfK3A  

SIMU.TV: Vyombo vya ulinzi na usalama katika mikoa ya Kagera na Kigoma wameombwa kuimarisha hali ya ulinzi ili kuhakikisha silaha haramu haziingizwi nchini; https://youtu.be/SaNOA8hrZcY  

SIMU.TV: Waziri mkuu Kassim Majaliwa ametoa muda wa miezi miwili kwa wakuu wa mapori ya hifadhi za misitu kuweka vibao vya mipaka ili kuepusha migogoro na wananchi; https://youtu.be/uTEB3Hsb33U  

SIMU.TV: Mivutano baina ya viongozi na wananchi juu ya fidia mkoani Mbeya kumechangia kwa kiasi kubwa kuchelewa kwa ujenzi wa barabara na miundombino mingine; https://youtu.be/XQwa5WaKio4  

SIMU.TV: Wavuvi katika soko la kimataifa la samaki la Feri jijini Dar Es salaam wameomba utaratibu wa kuuza samaki kwa mnada ubadilishwe na mfumo wa kilo utumike; https://youtu.be/K24_ArRVFy8

SIMU.TV: Barazala la taifa la uwezeshaji wananchi Kiuchumi NEEC limezitaka kampuni za simu nchini kukamilisha taratibu za kujiunga katika soko la hisa Dar Es salaam;’ https://youtu.be/QuXBtR3gNns  

SIMU.TV: Shirika la hifadhi za taifa TANAPA kwa kushirikiana na mashirika ya ndege wamezindua ratiba za ndege za moja kwa moja mpaka kwenye hifadhi ili kukuza utalii; https://youtu.be/hH7RhXT9TA8

SIMU.TV: Klabu ya soka ya Yanga leo imemtabulisha rasmi kocha mkuu wake raia kutoka Zambia George Lwandamina ambae atachukua mikoba iliyoachwa na Hans Pluijm; https://youtu.be/T0EWMgX-Hus

SIMU.TV: Kozi ya makocha wapya wa soka la wanawake itasaidia kwa kiasi kikubwa kukuza kiwango cha soka la wanawake nchini; https://youtu.be/4ca5AiA7Pt4

SIMU.TV: Timu ya tenisi ya walemavu ya Tanzania imeshindwa kutamba na timu ya walemavu kutoka Kenya kutokana na ukosefu wa vifaa bora vya kuchezea; https://youtu.be/efrufti-wl4

SIMU.TV: Waziri wa elimu, sayansi ,teknolojia na mafunzo ya ufundi Prof. Joyce Ndalichako ameitaka tume ya vyuo vikuu nchini kuvifungia vyuo vyote vitakavyobainika kutokuwa na sifa za kutoa elimu ya juu. https://youtu.be/9uQBjkulgU4

SIMU.TV: Mfuko wa taifa wa bima ya afya NHIF kwa kushirikiana na serikali ya Ujerumani umezindua mradi wa Tumaini la mama wenye lengo ka kugharamia matibabu kwa mama na mtoto. https://youtu.be/Yo21XTkJJ3o

SIMU.TV: Baadhi ya wananchi wanaotumia usafiri wa mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam wamelalamikia kusitishwa kwa daladala za kawaida kuingia katikati ya jiji. https://youtu.be/xYHkyMHGEeI

SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda ametembelea daraja la Nyerere lililopo katika wilaya mpya ya Kigamboni ili kusikiliza kero za wananchi. https://youtu.be/4B3ojmYwiSo

SIMU.TV: Serikali mkoani Lindi imeunga mkono hatua ya wakulima kugoma kuuza korosho zao kutokana na wanunuzi kushusha bei ya zao hilo. https://youtu.be/1LFIBcxqCC0

SIMU.TV: Hali ya utalii katika mbuga za wanyama hapa nchini imeanza kuimarika baada ya shirika la hifadhi za taifa TANAPA kuchukua hatua mathubuti katika kuimarisha sekta ya utalii. https://youtu.be/hW60vOOS37g

SIMU.TV: Baraza la taifa la uwezeshaji wananchi kiuchumi limeyataka makampuni ya simu hapa nchini kutimiza sheria ya kutoa asilimia 25 ya hisa kwa wananchi. https://youtu.be/1EfsjoDbyhU

SIMU.TV: Baadhi ya wananchi wa manispaa ya Songea wameiomba serikali kuipa kipaumbele mikoa ya pembezoni ili iweze kupata miradi ya maendeleo sawa na mikoa mingine. https://youtu.be/AoLKwC5lKVc

SIMU.TV: Wadau wa mchezo wa riadha mkoani Kilimanjaro wameiomba serikali kuhamasisha mchezo huo kuanzia shule za msingi ili kuibua na kukuza vipaji vya mchezo huo. https://youtu.be/G1CQTHlhND4

SIMU.TV: Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF limeshauriwa kuangalia na kuboresha kanuni zinazoendesha ligi daraja la pili nchini ili kuondoa ubabaishaji katika ligi hiyo. https://youtu.be/gMq7Wum9_Do

SIMU.TV: Mkongwe wa muziki wa dansi  nchini anatarajiwa kufanya onesho siku ya jumamosi kwa ajili ya kuadhimisha miaka 30 tangua aingie katika tasnia hiyo. https://youtu.be/cFNd-a4Y7Vs

SIMU.TV: Valence Nandisenga kutoaka nchini Rwanda ameibuka mshindi wa mbio za baiskeli za tour of Rwanda zilizofanyika nchini Rwanda. https://youtu.be/R2H5Vo-mEto

No comments: