Monday, November 7, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI


SIMU.TV: Spika mstaafu wa bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania Samweli Sitta  amefariki dunia jijini Munich nchini Ujerumania alipokuwa akipatiwa matibabu. https://youtu.be/oOy9Fe51pxA

SIMU.TV: Kufuatia kutokea kwa kifo cha Spika mstaafu wa bunge la tisa Samweli Sitta bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania limeairisha kikako chake leo ili kuomboleza msiba huo. https://youtu.be/MMamVNgG5n0

SIMU.TV: Jeshi la polisi jijini Dar es Salaam limefanikiwa kumkamata mwanamke mmoja kwa kujaribu kusafirisha madini ya Tanzanite yenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mia moja bila kuwa na vibali. https://youtu.be/gWGQ9dAsCvY

SIMU.TV: Wananchi wa kata ya Ikondo katika wilaya ya Muleba wamesusia kuchangia shughuli za shughuli za maendeleo kutokana na kutuhumu watendaji kufanya ubadhirifu wa fedha wanazochanga. https://youtu.be/kMCVm0SOcsQ

SIMU.TV: Taasisi ya ujasiriamali na uwekekezaji  imetakiwa kupanua programu yake ya kijana jiajiri ili kuweza kuwafikia vijana wengi nchini. https://youtu.be/WeGGLGi7gh4

SIMU.TV: Wakazi wa Ilala mchikichini jijini Dar es Salaam wamelalamikia kucheleweshwa kwa zoezi la kufanyika kwa tathimini ya makazi yao ili kupisha mradi mkubwa wa umeme. https://youtu.be/taUB-CrHNH8

SIMU.TV: Shirika la nyumba la taifa NHC limezindua sera ya mpangaji mnunuzi ambayo itawawezesha wananchi wa hali ya nchini kumiliki nyumba. https://youtu.be/VhFoACV9pBg

SIMU.TV: Wafanyabiashara mkoani Mbeya wametakiwa kuchangamkia fursa za kibiashara zinazojitokeza ili kuweza kutambuliwa kirahisi na serikali pamoja na taasisi za kifedha na kupata mikopo kirahisi. https://youtu.be/Z-KQzDTH83w

SIMU.TV: Ujumbe wa wafanyabiashara 18 kutoka katika kampuni za nchini Uturuki zinazo zalisha vipuri vya magari wamewasili nchini ili kuangalia fursa za uwekezaji. https://youtu.be/U-qCmKNtGTg

SIMU.TV: Klabu ya Majimaji kwa mara nyingine imeweza kuibuka na ushindi katika mchezo wake dhidi ya Mwadui fc ya mkoani Shinyanga. https://youtu.be/BMJiy0e_h9Y  

SIMU.TV: Aliyekuwa makamu mwenyekiti wa bodi ya ligi kuu ya Tanzania bara Said Mohamed amefariki dunia katika hospitali ya Agakhan jijini Dar es Salaam alipokuwa akipatiwa matibabu. https://youtu.be/qz34ZW-Xw2g

SIMU.TV: Kampuni ya urushaji wa matangazo kwa njia ya digitali ya Multchoice imezindua channel mpya iitwayo Maisha Magic Bongo itakayokuwa ikitangaza filamu za kitanzania. https://youtu.be/gUZAx6PRjzM

SIMU.TV: Mchezaji wa kimataifa wa Ureno Christiano Ronaldo amesema bado ana miaka kumi ya kucheza soka licha ya kufikisha miaka 31. https://youtu.be/L4ebnvC2qYg

SIMU.TV: Watu 18 wamefariki dunia baada ya kutokea kwa ajali iliyohusisha gari aina ya Noah na Lori la mizigo katika kijiji cha Msalala mkoani Shinyanga; https://youtu.be/ms-vz5TybYY

SIMU.TV: Bunge la Jamhuri ya muungano wa Tanzania limehairisha shughuli zake hii leo ili kupisha wabunge kuomboleza kwa msiba wa mheshimiwa Samuel Sitta; https://youtu.be/UM0X-YbQK0Y

SIMU.TV: Kufuatia nchi yetu kupatwa na msiba mkubwa wa aliyewahi kuwa Spika wa bunge Samuel Sitta, TBC wamekuandalia makala fupi kuelezea historia yake; https://youtu.be/9Jcwly-uScc

SIMU.TV: Raia wa Marekani hapo kesho watapiga kura ya kumchagua rais mwingine atakayewaongoza kwa muda wa miaka minne ijayo, wanaoshinda kwa ukaribu ni Hillary Clinton na Donald Trump; https://youtu.be/HMHwlkqGR_w

SIMU.TV: Polisi mkoani Tanga yawaondoa wachimbaji haramu wa madini zaidi ya 3000 waliovamia mgodi wa Magamba; https://youtu.be/OGh556WHNkc

SIMU.TV: Shirika la nyumba la Taifa NHC limezindua sera mpya ambayo itamuwezesha mwananchi wa kipato cha chini kununua nyumba za shirika hilo; https://youtu.be/84K9ac2mOgU

SIMU.TV: Shirika la viwango nchini TBS limetenga jumla ya shilingi milioni 200 kwa ajili ya kupima bidhaa zinazozalishwa na wajasiriamali nchini; https://youtu.be/bjUSYUZPpFU

SIMU.TV: Mkoa wa Mbeya umewaagiza wafanyabiashara mkoani humo kusajili biashara zao ili waweze kutambulika na serikali; https://youtu.be/twJlY0uzQ1s

SIMU.TV: Kampuni ya kukatisha tiketi kwa mtandao ya Start my Safari wamesema teknolojia hiyo imerahisisha na kupunguza usumbufu wa ukataji wa tiketi; https://youtu.be/24UxuDYV4VY  

SIMU.TV: Michezo ya kukamilisha kwa mzunguko wa kwanza wa ligi kuu Tanzania bara itafanyika katika ya wiki hii ili kupisha kwa mchezo wa kirafiki kati ya Stars na Zimbabwe; 

SIMU.TV: Timu ya Uhamiaji imeendelea kutesa katika mashindano ya Netiboli ya Muungano baada ya kuwafunga Jeshi Stars leo hii; https://youtu.be/qKL1DvYhj9I

SIMU.TV: Kikosi cha wachezaji 18 cha timu ya taifa ya wanawake kinatarajia kuondoka wiki hii kuelekea nchini Cameroon kucheza mchezo wa kirafiki; https://youtu.be/9m9iSEL5l4s

SIMU.TV: Aliyekuwa mwenyekiti wa klabu ya Azam Fc Said Mohamed Said amefariki dunia hii leo alipokuwa anakimbizwa hospitali baada ya kuugua ghafla; https://youtu.be/CRx3kFQ0Cg0No comments: