Tuesday, November 29, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI


SIMU.TV: Wakala wa uagizaji wa mafuta kwa pamoja leo umetangaza zabuni ya uagizaji wa mafuta kwa mwaka 2017 huku makampuni ya ndani yakiwekwa kushindana yenyewe. https://youtu.be/4D8vNrBvAaA

SIMU.TV: Kituo cha uwekezaji hapa nchini TIC kimekanusha taarifa za kufungwa kwa kiwanda cha saruji cha Dangote kwa sababu ya gharama za uendeshaji na kusema kuwa kiwanda kimefungwa kutokana na matatizo ya kiufundi. https://youtu.be/WDh45XVrMv8

SIMU.TV: Wenyeiti wa serikali za mitaa 13 wilaya ya Kinondoni wametiwa mbaraoni baada ya wananchi kuwalalamikia kwa mkuu wa mkoa kuuza viwanja kwa mtu zaidi ya mtu mmoja. https://youtu.be/q-2Vr_ney-w

SIMU.TV: Tanzania imepokea msaada kutoka kwa taasisi ya Trade Mark East Afrika kwa lengo la kuisaidia kuinua miundombinu ya  taasisi ya sekta binafsi nchini. https://youtu.be/nEH-OughHbE

SIMU.TV: Balozi wa Ireland hapa nchini ameishauri serikali kuwapa nafasi ya kurudi darasani watoto wa kike wanaokatisha masomo kutokana na mimba za utotoni. https://youtu.be/RqVc69uQZ6Q

SIMU.TV: Baadhi ya wafanyabiashara wa mazao ya kilimo wameonekana kuitikia wito wa kuchangamkia fursa ya kufanya biashara na nchi ya Saudi Arabia. https://youtu.be/Ry5iH-VmS94

SIMU.TV: Benki ya CRDB imesema inaendelea na mkakati wake wa kufungua matawi sehemu mbalimbali nchini na kuzindua huduma mbalimbali ili kuwafikia watanzania wengi. https://youtu.be/mlUTXvrGUi4

SIMU.TV: Katibu mkuu wa chama cha riadha Wilhelim Gudabuda amesisitiza kuwa anampango wa kuinua mchezo wa riadha na kuifanya Tanzania kupata wachezaji bora zaidi. https://youtu.be/mZfblIi1ybM

SIMU.TV: Kocha mkuu wa timu ya soka la  Ufukweni John Mwansasu ametangaza kikosi kitakachoingia kambini kujiandaa na mchezo wao dhidi ya Uganda utakaochezwa Desemba tisa. https://youtu.be/ZdDHPTo-jN0

SIMU.TV: Kamati ya katiba na sheria ya shirikisho la soka TFF imeiagiza klabu ya Simba kumlipa mchezaji Hassan Kessy mshahara wa miezi mitatu ya mwisho katika kumaliza mkataba wake. https://youtu.be/hCTjgQXMbkg

SIMU.TV: Shirikisho la soka TFF limekanusha taarifa zilizoenea kuwa limeandaa mashindano yatakayo shirikisha vilabu mbalimbali zikiwemo Simba na Yanga. https://youtu.be/sZvsasyAruQ

SIMU.TV: Ulimwengu wa soka leo umeshuhudia simanzi nzito baada ya wachezaji wa timu ya Chepecoense kutoka nchini Brazil kupata ajali ya mbaya ya ndege nchini Colombia. https://youtu.be/LY3vegxw85g

No comments: