Thursday, November 3, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISHENI


SIMU.TV: Watu watatu wamekufa na wengine watatu kujeruhiwa baada ya kifusi kuwafunika katika machimbo ya dhahabu wilayani Iramba mkoani Singida; https://youtu.be/N-s_n9zA6lg

SIMU.TV: Rais Dr John Magufuli, amekutana na muwakilishi wa benki ya dunia kwa ukanda wa nchi za kusini na kuzungumzia utekelezi wa miradi ya maendeleo nchini Tanzania; https://youtu.be/aygJEDpRCTo

SIMU.TV: Waziri mkuu Kassim Majaliwa, amesema serikali itaendelea kupeleka fedha katika halmashauri zote nchini ili kuwaletea wananchi maendeleo; https://youtu.be/gev96GWM1eg

SIMU.TV: Jeshi la polisi mkoani Arusha linamshikilia mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema ambae amesafirishwa kutoka Dodoma kwa tuhuma za uchochezi; https://youtu.be/GM0WrdKl9z8

SIMU.TV: Rais Dr John Magufuli kesho atafanya mahojiano ya kwanza na waandishi wa habari tangu akalie kiti cha Urais nchini Tanzania; https://youtu.be/p_GRR1Flhqc

SIMU.TV: Waziri wa mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika mashariki amefungua kikao cha baraza la mawaziri asasi na kisiasa ulinzi na usalama kwa wabunge wa kusini mwa Afrika; https://youtu.be/DZAfXzueEfw

SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa Dar Es salaam Paul Makonda amewaasa wazazi nchini kuhimiza watoto wao kusoma masomo ya sayansi; https://youtu.be/JfJDoiqCDBM

SIMU.TV: Katika kipindi cha mwaka mmoja wa Rais Magufuli madarakani, kituo cha uwekezaji TIC kimesajili miradi yenye thamani ya Dola Bilioni kumi; https://youtu.be/9bUCwU0ZITs

SIMU.TV: Kituo cha utafiti wa zao la Korosho cha Naliendele mkoani Mtwara kimewashauri wakulima wa zao hili kutumia mbinu ya ubebeshaji ili kuongeza uzalishaji; https://youtu.be/qlpZNIeGJOM

SIMU.TV: Baadhi ya wafanyabiashara wanaoshiriki maonesho ya Syria wamelazimika kuuza biashara zao kwa bei ya chini kutokana na hali ya wateja wao; https://youtu.be/c5k_6Hx7IuY

SIMU.TV: Waamuzi waliochaguliwa kuchezesha michuano ya Netiboli kombe la muungano wametakiwa kufuata sheria na kuchezesha kwa haki; https://youtu.be/kU9l8Dn-mAk

SIMU.TV: Kocha mkuu wa Serengeti boys Bakari Shime, amesema mashindano ya kimataifa wanayokwenda kushiriki nchini Korea Kusini itasaidia kukuza kiwango chao; https://youtu.be/nnnf6F-5U8o

SIMU.TV: Mashabiki wa Timu ya Yanga wametakiwa kutokata tamaa na matokeo ya jana na watakiwa kuendelea kuisapoti timu yao kwani mapambano bado yanaendelea; https://youtu.be/BI-a46wFPR0

SIMU.TV: Wadau mbalimbali wa michezo nchini wameuzungumzia mwaka mmoja wa Rais Magufuli akiwa madarakani katika nyanja ya michezo; https://youtu.be/FfDDKoedCFA

SIMU.TV: Wasomi wa vyuo vikuu katika jiji la Dar es Salaam wamesema uongozi wa rais Magufuli umetikisa mifumo iliyoota mizizi kama rushwa na uwajibikaji mbovu katika sekta ya umma. https://youtu.be/MwhsHa7KNoA

SIMU.TV: Kikosi cha kukusanya mapato katika halmashauri ya wilaya ya Liwale kimefanikiwa kukamata pikipiki moja na mbao zaidi ya 800 zinazosadikiwa kuvunwa kinyume na sheria. https://youtu.be/SrSZg4h011Y

SIMU.TV: Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amepokea msaada wa madawati  kutoka kwa shule za Al muntazir ikiwa ni juhudi za kumaliza tatizo la madawati nchini. https://youtu.be/4wygSfNVEuE

SIMU.TV: Wabunge wa Tanzania katika bunge la Afrika Mashariki wametakiwa kuanza kuangalia fursa za masoko kwa bidhaa za Tanzania wakati tukielekea kwenye uchumi wa viwanda. https://youtu.be/gYay_jGm314

SIMU.TV: Baadhi ya watoto waliorejeshwa shule wakitokea kwenye ajira hatarishi za migodini wameiomba serikali kuwachukulia hatua wanaowaajiri watoto. https://youtu.be/bPg4v7wAp2E

SIMU.TV: Baadhi ya wanafunzi katika chuo kishiriki cha elimu cha DUCE wameiomba serikali kuharakisha utoaji wa mikopo kutokana na kukosa fedha za kujikimu. https://youtu.be/hPGmf6Ve3D8

SIMU.TV: Wasichana 50 waliokatisha masomo kwasababu ya kuolewa wakiwa katika umri mdogo katika wilaya za Butiama na Musoma wamepokea msaada wa milioni tano kwa ajili ya kufanyia shughuli za kujiendeleza kiuchumi. https://youtu.be/4L1odWfUg6Q

SIMU.TV: Wakulima wa tumbaku mkoani Tabora wameshauriwa kulima mazao mbadala ya biashara ili kukabiliana na athari za uharibifu wa mazingira. https://youtu.be/8YSXetx5Dfo

SIMU.TV: Klabu ya Mtibwa Sugar imefanikiwa kuibuka na ushindi ilipokuwa ugenini kucheza na Mwadui fc na kuifunga mabao matatu kwa mawili. https://youtu.be/R7RHcJfYdA8

SIMU.TV: Kocha mkuu msaidizi wa timu ya Sister Fc ya mkoani Kigoma Almas Madau amefariki dunia na kuacha pengo kubwa kwa timu hiyo inayoshiriki ligi kuu ya wanawake nchini. https://youtu.be/JKiI3dPb-gA

SIMU.TV: Wasanii wa maigizo na filamu katika halmashauri ya manispaa ya Iringa wamelalamiki ongezeko la wezi wa kazi zao na kuwafanya wasinufaike na kazi hizo. https://youtu.be/8MwwMXUW-D4No comments: