Saturday, November 19, 2016

SIMU TV: HABARI KUTOKA TELEVISEHENI

SIMU.TV: Waziri wa nchi ofisi ya rais TAMISEMI George Simbachawene amesema bado kuna mkanganyiko katika dhana ya uzalendo katika kizazi cha sasa. https://youtu.be/sah-WjSUFV8

SIMU.TV: Hatimaye mahakama kuu kanda ya Mwanza imetoa hukumu ya kesi ya uchaguzi wa jimbo la Bunda mjini na kumpa ushindi mbunge Ester Bulaya. https://youtu.be/SGrWsEApkM0

SIMU.TV: Wafanyabiashara katika soko kuu la manispaa ya Songea wameendelea na mgomo kwa siku ya pili leo wakipinga kuongezewa kodi ya pango bila makubaliano. https://youtu.be/aW5de9L6y-E

SIMU.TV: Kamisheni ya utalii visiwani Zanzibar imesema idadi ya watalii wanaotembelea visiwa hivyo inatarajiwa kuongezeka zaidi kutokana na mashirika makubwa ya usafiri wa anga kuanzisha safari za visiwani humo. https://youtu.be/vwEwhSIg8vs

SIMU.TV: Tanzania imeungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha siku ya viwango duniani na kuweka malengo ya kuzalisha bidhaa zenye ubora zaidi. https://youtu.be/gknNiuP77y4

SIMU.TV: Naibu waziri ofisi ya makamu wa rais mazingira na muungano ameziagiza taasisi za serikali zikiwemo gereza la keko na kiwanda cha kutengeneza madawa cha keko kuancha tabia ya kitiririsha maji taka. https://youtu.be/ko9HvNONtjk

SIMU.TV: Wafanyabiashara wadogo katika eneo la Mwenge jijini Dar es Salaam wameahidi kuwa walipa kodi wazuri baada ya manispaa ya Kinondoni kuruhusu magari ya abiria kushusha na kupakia abiria katika eneo hilo. https://youtu.be/GOM8M0yPqeI

SIMU.TV: Waziri wa viwanda biashara na uwekezaji amezindua kamati ya uboreshaji wa mazingia ya biashara nchini na kutoa wito kwa wafanyabishara nchini kutumia furasa zinazopatikana. https://youtu.be/uLEcoGdeb2U

SIMU.TV: Watumishi wa umma na sekta binafsi wanatarajiwa kunufaika kufuatia kuzinduliwa kwa huduma ya Wezesha kutoka benki ya Afrika itakayo wawezesha kupata mikopo kwa urahisi. https://youtu.be/ZxieJupgibs

SIMU.TV: Michuano ya kombe la shirikisho Tanzania bara inayoshirikisha timu 86 kutoka mikoa mbalimbali nchini yanatarajiwa kufunguliwa kesho huko mkoani Tanga. https://youtu.be/2bBXjiyH2KA

SIMU.TV: Bondia wa kimataifa wa Tanzania Fransis Miyeyusho yupo nchini jamhuri ya Czech akitarajiwa kufanya pambano dhidi ya Sebastian Baiting wa nchini humo. https://youtu.be/4CTAi4Kzgw8

SIMU.TV: Mashabiki wa soka ulimwenguni mwishoni mwa wiki hii watashuhudia michezo mbalimbali ya timu hasimu katika ligi tofauti ambapo Real Madrid watakutana na Atletico Madrid, Machester United wakiwalika Arsenal wakati Bayern Munich wakikabiliana na Borusia Dortmund. https://youtu.be/0pEF4aeeqvA

SIMU.TV: Makamu wa Rais Samia Suluhu, amezitaka halmashauri nchini kuacha kulalamikia serikali kuhusu fedha na badala yake waongeze bidii katika kukusanya mapato; https://youtu.be/D-WO9TUFqAU

SIMU.TV: Serikali imevifungia na kuvitoza faini viwanda viwili vya kutengeneza kokoto baada ya kushindwa kuwajengea mazingira mazuri ya kazi wafanyakazi wake; https://youtu.be/l9F9SINTh9k

SIMU.TV: Waziri wa Tamisemi George Simbachawene, amewataka watumishi wote nchini kufanya kazi kwa maslahi ya taifa ili kuhakikisha maendeleo yanapatikana; https://youtu.be/cZtlk6gswsc

SIMU.TV: Waziri mkuu Kassim Majaliwa, amewataka wataalamu wa ujenzi katika eneo la Magomeni Kota kukamilisha ujenzi huo unakamilika kwa wakati; https://youtu.be/YzPaXS9COMY

SIMU.TV: Waziri wa Elimu Prof Joyce Ndalichako, amesema serikali itaendelea kuzalisha walimu wenye uwezo ili kuhakikisha sekta ya Elimu inakuwa imara; https://youtu.be/pEayXj2mJq0

SIMU.TV: Mratibu anayeshughulikia masuala ya makazi kwa wakimbizi kutoka umoja wa mataifa Alvaro Rodriguez amesema wakimbizi wanastahili kupatiwa huduma zote muhimu za kijamii; https://youtu.be/GkID8JWSXHw

SIMU.TV: Wafanyabiashara nchini wamekaribishwa kufanya uwekezaji katika wilaya ya Kigamboni kwani wilaya hiyo ina eneo la kutosha kwa wafanyabiashara; https://youtu.be/FP1VbXh5XXI

SIMU.TV: Vijiji mbalimbali nchini Tanzania wanatarajia kunufaika na uwekezaji mkubwa wa kusambaza vifaa vya umeme wa nguvu za jua; https://youtu.be/yrPqQ3JCsN0

SIMU.TV: Wizara ya viwanda na uwekezaji imewataka wahusika wa usindikaji wa bidhaa nchini kuwatumia watu wa TBS na TFDA ili kuhakiki ubora wa bidhaa zao; https://youtu.be/X43s8QELnQI

SIMU.TV: Kampuni tanzu ya Katapila ya Shandong kutoka China imedhamiria kuwaondolea adha ya ujenzi watanzania baada ya kusogeza mitambo ya ujenzi nchini; https://youtu.be/SvTmQIihiPU

SIMU.TV: Mashindano ya Gofu ya mkuu wa majeshi yameanza kutimua vumbi lake katika viwanja vya Gofu vilivyopo katika kambi ya jeshi Lugalo; https://youtu.be/5jrArnrbQ64

SIMU.TV: Farid Mussa Klabu ya soka ya Azam imewaomba wadau wa soka nchini kuwa na subira kuhusiana na suala la Farid Mussa kwenda kucheza soka la kulipwa huko Hispania; https://youtu.be/6L5I_WOGz6k

SIMU.TV: Shirikisho la mpira nchini limemteua Yahya Mohamed kuwa mwenyekiti wa kamati ya masaa 24; https://youtu.be/J0bA1lkOsY0


No comments: