Thursday, November 17, 2016

SERIKALI YABARIKI UZINDUZI WA TELEVISHENI YA KIDIGITALI KUTOKA STARTIMES

Serikali kupitia Wizara ya Ujezi Uchukuzi na Mawasilano imebariki uzinduzi wa televisheni mpya ya kidigitali kutoka kampuni ya Startimes Tanzania. 
 Akizungumza katika uzinduzi huo kwa niaba ya Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhe. Prof Makame Mbarawa, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Bibi. Maria Sasabo amesema Serikali imefarijika sana na ubunifu kutoka kwa kampuni ya StarTime Tanzania kwa kuanzisha televisheni ya kidigitali isiyotumia kinga’muzi kupata matangazo ya channeli mbalimbali. 
 “Hii ni fursa kwa watanzania kujipatia televesheni hizi ambazo ziko katika teknolojia ya hali juu sana ambazo zitasaidia Tanzania kuingia katika ulimwengu mpya wa mapinduzi ya sekta ya Habari na Mawasiliano” alisema Bibi. Maria. 
 Kwa upande wake Mkurugenzi wa StarTimes Tanzania Bw. Leo Liao amesema kuwa StarTimes imelazimika kutoa televisheni hizo za kisasa ili kuendana na ukuaji wa teknolojia ambapo wateja wataweza vipindi vinavyoenda na wakati katika ubora wa hali ya juu. 
 “Tutahakikisha tunawapa wateja wetu vipindi vyenye ubora na muonekano mzuri ambao wataufurahia ulimwengu wa Digitali unaoendelea kubadilika kila kukicha duniani” alisistiza Bw. Liao. 
 Ameongeza kuwa televisheni hizo zimetengenezwa katika ubora unaotakiwa na ni rafiki kwa mazingira na zimezingatia matumizi madogo ya umeme na zinapatikana kwa bei nafuu ukilinganisha na televisheni kutoka makampuni mengine. 
 Televisheni hizo za kidigitali zinaonesha zaidi ya channeli 100 za kitaifa na kimataifa kuanzia habari, muziki, michezo, sinema, thamthilia,katuni, filamu na vipindi vya Dini.
 Mshehereshaji Luvanda akiwakaribisha wageni wakati wa hafla ya uzinduzi wa televisheni za kidigitali kutoka kampuni ya StarTimes Tanzania uliofanyika Novemba 16,2016 Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa StarTimes Tanzania Bw. Leo Liao akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa televisheni za kidigitali kutoka kampuni yake uliofanyika Novemba 16,2016 Jijini Dar es Salaam.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Bibi. Maria Sasabo akizungumza na wadau sekta ya Habari na Mawasiliano wakati wa hafla ya uzinduzi wa televisheni ya kidigitali kutoka kampuni ya Startimes Tanzania uliofanyika Novemba 16, 2016 Jijini Dar es Salaam.
 Meneja Masoko na Mahusiano wa StarTimes Tanzania Bw. Juma Sharobaro akizungumza wakati wa kuchezesha bahati nasibu ya kumpata mshindi wa moja ya televisheni za kidigitali katika hafla ya uzinduzi wa televisheni hizo uliofanyika Novemba 16, 2016 Jijini Dar es Salaam.
 Mkurugenzi Mkuu wa StarTimes Tanzania Bw. Leo Liao(kushoto) akikabidhi zawadi ya moja ya televisheni za kidigitali yenye upana wa inchi 40 kwa mshindi wa televisheni hiyo Bw.John Paul  wakati wa hafla ya uzinduzi wa televisheni hizo uliofanyika Novemba 16,2016 Jijini Dar es Salaam.

 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Bibi. Maria  Sasabo(kushoto) akipokea zawadi ya moja ya televisheni za kidigitali kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa StarTimes Tanzania Bw. Leo Liao(kulia) wakati wa hafla ya uzinduzi wa televisheni hizo uliofanyika Novemba 16,2016 Jijini Dar es Salaam.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Bibi. Maria  Sasabo(kushoto) akipokea zawadi ya moja ya televisheni za kidigitali kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa StarTimes Tanzania Bw. Leo Liao(kulia) wakati wa hafla ya uzinduzi wa televisheni hizo uliofanyika Novemba 16,2016 Jijini Dar es Salaam.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Bibi. Maria  Sasabo(kushoto) akikabidhi zawadi ya moja ya televisheni za kidigitali yenye upana wa inchi 32 kwa mshindi wa televisheni hiyo Bw.Ambokile Mapasa  wakati wa hafla ya uzinduzi wa televisheni hizo uliofanyika Novemba 16,2016 Jijini Dar es Salaam.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Bibi. Maria  Sasabo( wa pili kushoto) akipata maelekezo kutoka kwa mmoja wa watendaji wa kampuni ya Startimes Tanzania jinsi ya televisheni za kidijitali zinavyofanya kazi wakati wa hafla ya uzinduzi wa televisheni hizo uliofanyika Novemba 16,2016 Jijini Dar es Salaam.
 Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Bibi. Maria  Sasabo( wa pili kushoto) akipata maelekezo kutoka kwa mmoja wa watendaji wa kampuni ya Startimes Tanzania jinsi ya televisheni za kidijitali zinavyofanya kazi wakati wa hafla ya uzinduzi wa televisheni hizo uliofanyika Novemba 16,2016 Jijini Dar es Salaam.
  Mkurugenzi Mkuu wa StarTimes Tanzania Bw. Leo Liao (kulia) akimueleza jambo Naibu Katibu Mkuu wa Wizara Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Bibi. Maria  Sasabo(kulia) wakati wa hafla ya uzinduzi wa televisheni za kidigitali kutoka kampuni ya StarTimes Tanzania uliofanyika Novemba 16,2016 Jijini Dar es Salaam.
Wasanii kutoka Dar es Salaam wakitoa burudani wakati wa hafla ya uzinduzi wa televisheni za kidigitali kutoka kampuni ya StarTimes Tanzania uliofanyika Novemba 16,2016 Jijini Dar es Salaam.

No comments: