Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akitia saini muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia ya mwaka 2016, katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,ambapo Viongozi mbali mbali wa Serikali na vyama vya Siasa walihudhuria hafkla hiyo,[Picha na Ikulu.] 15/11/2016.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akionesha hati muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia ya mwaka 2016,baada ya kusaini hati hiyo katika hafla iliyofanyika leo ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,ambapo Viongozi mbali mbali wa Serikali na vyama vya Siasa walihudhuria hafkla hiyo,[Picha na Ikulu.] 15/11/2016.
Viongozi Wakuu wa Vikosi vya Ulinzi na Usalama Zanzibar wakiwa katika hafla ya utiaji saini muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia ya mwaka 2016,uliotiwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja
Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi na Viongozi mbali mbali wakiwa katika hafla ya utiaji saini muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia ya mwaka 2016,uliotiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo
Baadhi ya Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi na Viongozi mbali mbali wakiwa katika hafla ya utiaji saini muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia ya mwaka 2016,uliotiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo
Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar Mhe,Zubeir Ali Maulid (kulia) na Waziri wa Nishati na Madini Mhe,Profesa Sospiter Muhongo,wakiwa katika hafla ya Utiaji wa saini muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia ya mwaka 2016,uliotiwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,katika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo
Viongozi kutoka kushoto Kadhi Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar Sheihk Khamis Haji,Waziri wa Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo Mhe,Radhid Ali Juma,Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai na Naibu waziri wa Ardhi,Maji,Nishati na Mazingira Mhe,Juma Makungu Juma wakiwa katika Utiaji wa saini muswada wa sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi asilia ya mwaka 2016,uliotiwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein Ikulu Mjini Unguja
Na Dk. Juma Mohammed, MAELEZO Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein amesaini Mswada wa sheria ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia na kusisitiza kwamba Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania haikuvunjwa.
Akizungumza Ikulu Mjini Zanzibar jana wakati akitia saini Mswada wa sheria ya utafutaji, uchimbaji wa mafuta na gesi asilia wa mwaka 2016, Rais Dk. Shein alisema kwamba taratibu zote zimefuatwa wakati wa mchakato wa kutunga kwa sheria hiyo na kuwaomba wananchi kuwapuuza wanaoeneza uzushi.
Rais Dk. Shein alisema haja ya kuwepo kwa sheria hiyo inatokana na masharti ya kifungu cha nne Sheria ya Mafuta na Gesi Asilia 2015 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo inataja kwamba shughuli za uendeshaji wa Mafuta na Gesi Asilia utafanywa Zanzibar kwa kusimamia na kuendeshwa na taasisi kwa mujibu wa Sheria za Zanzibar.
“Kumekuwa na maneno mengi kwamba nisisaini sheria hii, Hakuna katiba wala sheria iliyovunjwa na tunawaomba wananchi kuendelea kuwa watulivu, kuheshimu sheria na kudumisha amani na mshikamano” Alisisitiza Rais Dk. Shein.
Rais Dk. Shein amewataka wananchi wasikubali kuyumbishwa na wala wasibabaishwe na watu wasioitakia mema Zanzibar. Alisema kwamba sheria hiyo sasa itafungua milango kwa Makampuni mbalimbali kujitokeza kuanza kazi ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asili Visiwani Zanzibar.
Alisema kwamba kuna kazi kubwa ya kufanya katika utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia hivyo amewaomba wananchi kuwa wavumilivu na kutoa ushirikiano katika shughuli hiyo ambapo pia amewataka wataalamu katika fani ya mafuta kufanyakazi kwa bidii na maarifa zaidi.
Rais Dk. Shein alisema hadi sasa kuna Makampuni mawili yamejitokeza kuomba kuwekeza katika kazi ya utafutaji na uchimbaji wa mafuta na gesi asilia Zanzibar akiyataja makampuni hayo kuwa ni Ras Gas ya Ras Al –Khaimah na shell.
Rais Dk Shein alisema baada ya mazungumzo ya Serikali mbili katika usimamizi wa rasilmali za Mafuta na Gesi Asilia, iliamuliwa kuwa kila upande katika Jamhuri ya Muungano upewe uwezo wa kusimamia rasilmali hizo na kuanza kwa kufutwa kwa Sheria ya Jamhuri ya Muungano ya Sheria ya Mafuta ya mwaka 1980 na kuanzishwa kwa Sheria mpya ya Mafuta ya mwaka 2015 ambayo ilijengeka katika misingi ya usimamizi wa rasilmali za mafuta na gesi kwa Tanzania Bara.
Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar nayo ilitakiwa kuanzisha sheria yake yenyewe ambayo itasimamia Shughuli kama hizo kwa Zanzibar. Katika kutumia nafasi hiyo, SMZ ilianza kuchukuwa hatua za kuelimisha wadau mbalimbali ndani ya Serikali kwa nia ya kujijenga uwezo ili kuanza kujenga mazingira yakayo weza kuifanya Zanzibar kusimamia masuala ya mafuta na gesi asilia.
Rais Dk Shein alisema katika kipindi cha mwaka 2015 na 2016, Zanzibar ilifanikiwa kuanza na matayarisho ya Sera ya Mafuta na Gesi na Sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia kwa kutumia wataalamu wake wa ndani kwa kushirikisha ngazi mbalimbali za Serikali na wananchi hususan Wawakilishi wa Wananchi.
Rais Dk Shein alisema Mwezi Septemba 2016, Sera ya Mafuta na Gesi ambayo ilisharidhiwa na Baraza la Mapinduzi ilikamilika na Baraza la Wawakilishi la Zanzibar lilipitisha rasmi Sheria ya Utafutaji na Uchimbaji wa Mafuta ya Zanzibar ambayo leo nimeitia saini kuwa sheria kwa kuanza kutumika.
No comments:
Post a Comment