Madaktari na wataalamu wengine wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kushirikiana na Tanzania Australia Society na
Rafiki Surgical Mission wakimfanyia upasuaji mgonjwa wa kuvuna mishipa
na misuli katika mguu wake wa kulia na kupandikiza katika sehemu yenye
uhutaji husika. Madaktari bingwa wa Muhimbili wanaofanya upasuaji huo ni
Dk. Ibrahimu Mkoma, Dk Edwin Mrema, Dk. John Tupa na Dk Frank Muhamba
ambaye anapitia mafunzo ya kuwa daktari bingwa wa upasuaji. Mwingine ni
daktari bingwa wa upasuaji, James Savundra na wataalamu wenzake kutoka
Australia.
Daktari
Bingwa wa upasuaji katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dk Edwin
Mrema akizungumza na waandishi wa habari Leo katika chumba cha upasuaji
ambako kumefanyika upasuaji huo.
……………………………………………………………………………..
Madaktari wa Hospitali ya Taifa Muhimbili leo kwa mara ya kwanza wamefanya upasuaji kwa kutumia darubini (microvascular surgery) wa kuhamisha misuli na mishipa ya damu kutoka kwenye mguu kwenda sehemu nyingine chini ya mguu (free gracilis muscle transfer).
Upasuaji
huu wa aina yake na ambao mara nyingi huchukua muda wa saa sita hadi
saba una lengo la kujenga uwezo kwa watalaamu wa ndani ili waendelee
kutoa huduma za ubingwa wa hali ya juu kwa Watanzania wengi zaidi na
vilevile kupunguza kasi ya kupeleka wagonjwa nje.
Mkuu wa Idara ya Upasuaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambaye pia ameshiriki upasuaji huo Dk Ibrahim
Mkoma amesema upasuaji huo unagharimu kiasi cha dola 40,000 za Marekani
nchini Australia ikiwa ni gharama ya upasuaji tu.
Lengo
kubwa la ushirikiano wa upasuaji huu ni wataalamu kutoka Australia
kuwaachia taaluma ya upasuaji huo madaktari MNH ili iweze kuendelea
kufanya upasuaji huo mbeleni.
Aidha
Dk Mkoma amesema kuwa kuanzia mwakani kutakuwa na utaratibu ambao
utaanzishwa Chuo Kikuu cha Tiba Muhimbili, wa taaluma maalumu ya kusomea
upasuaji wa aina hiyo ili kuweza kupata wataalamu zaidi kutoka nchini.
Amesema hakuna chuo chochote Tanzania kinachotoa taaluma hiyo ya plastic surgery kwa sasa.
Dk Mkoma amesema MNH inajivunia kushirikiana na madaktari bingwa kutoka Australia akiwapo Daktari bingwa James Savundra ambaye ni Rais wa Madaktari Bingwa wa upasuaji kutoka timu ya upasuaji nchini Australia.
Daktari bingwa wa upasuaji kutoka Australia, Dk James Savundra amesema upasuaji huo ni moja ya upasuaji ambao umekuwa ukifanyika kwa gharama kubwa.
“Nchini
Australia mgonjwa mmoja hufanyiwa upasuaji kwa dola 130 za Marekani kwa
dakika moja hiyo ikiwa ni gharama za chumba cha upasuaji ambazo ni kwa
ajili ya kuwalipa
madaktari wa upasuaji, madaktari wa usingizi, wauguzi na watalaamu
wengine waliohusuka katika upasuaji huo,” amesema Dk Savundra.
Amesema gharama hiyo haijumuishi huduma nyingine ambazo mgonjwa huyo anatakiwa kupata ikiwamo huduma ya wodini na kadhalika.
“Tumefanya
upasuaji huu kwa kushirikiana na madaktari Bingwa kutoka nchini
Australia kupitia mashirika yasiyo ya Kiserikali ya Tanzania Australia
Society na Rafiki Surgical Mission,”amesema Dk. Mkoma.
Mpaka
sasa wagonjwa wanaohitaji upasuaji wa aina hiyo Muhimbili ni watatu
mbali na sita waliofanyiwa upasuaji mbalimbali ukiwamo upasuaji wa
shavu, nyonga, mkono na ziwa.
Mapema
wiki hii, Muhimbili imeanza kambi maalumu ya upasuaji kwa wagonjwa
wenye kuhitaji upasuaji maalumu kwa kushirikiana na madaktari hao kutoka
nchini Australia.
Hospitali
ya Taifa Muhimbili iko kwenye mageuzi makubwa katika kuboresha huduma
mbalimbali ambapo Disemba mwaka huu inatarajia kuanza kutoa huduma za
upandikizaji wa kifaa cha usikivu kwa watoto wanaozaliwa na matatizo ya
usikivu. Wakati huohuo Januari mwaka 2017 Hospitali hii inatarajia
kuanza kufanya upasuaji wa kupandikiza figo kwa wagonjwa wenye matatizo
hayo
No comments:
Post a Comment