Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Bi.Halima Dendegu akizungumza jambo wakati wa ufunguzi wa semina ya siku moja ya mafunzo kwa viongozi wa mikoa ya Mtwara na Lindi kuhusuUratibu,usimamizi na ufuatiliaji wa utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwezeshaji wananchi kiuchumi ya mwaka 2004. Mafunzo hayo yamefanyika mkoani Mtwara na kuratibiwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji wananchi kiuchumi (NEEC).
Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) Bi.Beng’i Issa akifafanua jambo kwenye semina elekezi kwa viongozi wa mikoa ya Mtwara na Lindi kuhusu uratibu, usimamizi na ufatiliaji wa utekelezaji wa sera ya Taifa ya Uwezeshaji wananchi kiuchumi ya mwaka 2004. Kushoto kwake ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi, Bw .Ramadhani Kaswa. Mkutano huo umefanyika mkoani Mtwara jana na kuratibiwa na NEEC.
Viongozi wa mikoa ya Mtwara na Lindi wakifatilia mada katika semina ya mafunzo juu ya uratibu, usimamizi na ufatiliaji wa utekelezaji wa sera ya Taifa ya Uwezeshaji wananchi kiuchumi ya mwaka 2004. Mkutano huo ulifanyika jana Mkoani Mtwara na kushirikia Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri wa mikoa hiyo na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC)
Na mwandishi wetu, Mtwara
Viongozi wa Mikoa ya Mtwara na Lindi wametakiwa kutafsiri katika vitendo mafunzo kuhusu uratibu, usimamizi na ufuatiliaji wa utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi ya Mwaka 2004 kwa kuwajengea uwezo wananchi katika kuibua fursa zitakazowaletea maendeleo.
Akishiriki katika mafunzo ya siku moja mjini hapa jana juu ya utekelezaji wa sera ya uwezeshaji iliyoratibiwa na Baraza la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi(NEEC), Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Bi Halima Dendegu, aliwambia viongozi kwamba mkoa hiyo miwili imejaliwa mambo mengi na kwa hiyo wananchi wanayo fursa ya kushinda umaskini iwapo wataongozwa vizuri.
“Tukatekeleze kwa vitendo elimu tunayoipata kutoka kwa wezeshaji wetu na ikawe na tafsiri halisi kwa wananchi katika maendeleo,” alisema Bi.Dendegu aliyefungua mkutano huo.
Amesema wajibu wa viongozi hao ni kuwachachua kifikra wananchi katika maeneo yao ili wawe wabunifu katika kuibua fursa na kuzifanyia kazi na wajipatie maendeleo.
“Mafunzo haya yatajenga uelewa wa pamoja kwa viongozi na utekelezaji uwe wa pamoja katika mikoa yetu,” alisema na kuongezea kuwa mafunzo haya hayatakuwa na maana kama tafsiri yake haitaonekana kwenye ngazi ya jamii.
Bi.Dendegu alizitaja fursa zilizopo Mkoani Mtwara ambazo wananchi waongozwe kuzifaidi kuwa ni zao la korosho, gesi asilia, ardhi kwa kilimo, fukwe za Bahari ya Hindi, bandari na kiwanda cha cement cha Dangote , na kusema haya ni maeneo ambayo wananchi wanaweza kubuni miradi itakayoendana na fursa hizo.
Alisema serikali itahakikisha kuchagua masoko ya bidhaa zitakazozalishwa na wananchi zinauzika kwa bei nzuri kama ilivyo katika zao la korosho kwa mwaka msimu huu.
Alishukuru NEEC kwa mikoa ya Mtwara na Lindi na kuahidi kutoa ushirikiano ili kutimiza azma ya serikali ya kufikia uchumi wa kati.
Katibu Mtendfaji wa NEEC, Bi.Beng’i Issa, amesema madhumuni ya mafunzo haya ni kuwajengea uwezo Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri za mikoa hiyo miwili juu ya sera ya uwezeshaji wananchi kiuchumi.
”Viongozi wengi ni wageni katika nyadhifa zao; hivyo imetulazimu kutoa mafunzo haya ili kuwe na ushirikiano na waratibu wa madawati ya uwezeshaji katika ngazi za halmashauri,” amesema Bi.Issa
Amesifia mwitiko wa wajumbe katika mafunzo haya kwa kuwa viongozi wote wamehudhuria.
Mawazo ya wajumbe katika kuchangia mada yameboresha mikakati ya kuwawezesha wananchi kiuchumi, amesema na kuongeza kuwa ushirikiano wa viongozi na wananchi ndio njia pekee ya kufika malengo ya kumuinua mwananchi kutoka kipato cha chini na kufikia kipato cha kati.
Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Bi.Rukia Muwango, amesema mafunzo yatawasaidia viongozi kuwajengea uwezo wananchi juu ya dhana ya uwezeshaji.
Ameonyesha na kusisitiza umuhimu wa wananchi kutunza fedha na kujiwekea akiba na kuwekeza katika fursa mbalimbali ili kukuza vipato vyao.
NEEC itaendelea kufanya mafunzo haya kwa kanda tano nchini ili viongozi wote wawe na fafsiri moja katika dhana ya uezeshaji wananchi kiuchumi.
No comments:
Post a Comment